NA PROF. MARK
MWANDOSYA, MATEMA BEACH, KYELA.
UKIKAA ufukweni
Matema wakati Ziwa Nyasa likiwa limetulia, kwenye upeo, kwa mbali kabisa
unaweza kuona umbile kama vile moshi unaobaki nyuma kama meli imepita. Mara ya
kwanza nilibishana na wenyeji wangu nikiwaambia meli ya MV Songea ilikuwa
ikipita kwa mbali kutoka bandari ndogo zilizo mwambao wa Ziwa.
