Tanzania imechaguliwa kuwa
mwenyeji wa mazoezi ya siku 14 ya pamoja ya makamanda wa kijeshi wa nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki yanakayojikita katika kupambana na
matukio ya ugaidi. Mazoezi yatafanyika
katika kituo cha ulinzi wa amani cha jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ
Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Showing posts with label Malengo. Show all posts
Showing posts with label Malengo. Show all posts
December 06, 2017
MAZOEZI YA KIJESHI KUFANYIKA NCHINI
December 04, 2017
UJENZI BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BAY WAKARIBIA
NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ujenzi wa barabara ya lami nzito toka Mbinga wilayani Mbinga hadi mjini Mbambabay Wilayani Nyasa unatarajia kuanza hivi karibuni.
BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA RC MDEME
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ujenzi wa barabara ya lami nzito toka Mbinga wilayani Mbinga hadi mjini Mbambabay Wilayani Nyasa unatarajia kuanza hivi karibuni.
Mndeme amesema hayo wakati
akitoa taarifa ya kufungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Ruvuma,
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea Novemba 29 mwaka huu, wiki
iliyopita.
Madhumuni
habari,
maisha,
Malengo,
maswali magumu,
Nyasa
November 20, 2017
KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA FIDEL CASTRO
Jukwaa la Wajamaa Tanzania,
Taasisi ya Usomaji na Maendeleo "Soma" na Rastafarai United Front
wanashirikiana kuandaa kongamano la kumkumbuka El Commandante Fidel Castro siku
ya Jumamosi, tarehe 25/11/2017. Mahala itakuwa kwenye ukumbi wa Soma Book Cafe;
na muda ni saa 7 mchana hadi saa 12 jioni.
WOTE MNAKABISHWA. HAKUNA
KIINGILIO!
"Mwambie Comrade amwambie
Comrade"
November 02, 2017
KAMPUNI YA MKUKI NA NYOTA WAINGIA SOKO LA VITABU CHINA
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Mkuki na Nyota ambayo hujishughulisha na uchapaji wa vitabu imetanua wigo wa soko lake la uchapishaji na utangazaji wa vitabu baada ya kusaini makubaliano na Shirika la World Affairs Press (WAP) la nchini China.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano
hayo Mkurugenzi wa MNN, Mkuki Bgoya amesema kuwa wamesaini Makubaliano na Shirika
la World Affairs Press (WAP) ya China kufanya kazi pamoja katika miradi
mbalimbali ya kuchapisha na kuvitangaza vitabu ikiwa ni njia mojawapo ya
kutanua soko la kampuni hiyo barani Asia.
Mkuki na Nyota ni kampuni
mashuhuri kwa uchapaji wa vitabu ambayo ilianzishwa mwaka 1992 jijini Dar es
salaam. Mwanzilishi wa kampuni hiyo ni Walter Bgoya ambaye alitumia uzoefu wake
wa miaka 18 ya kuwa Meneja Mkuu wa Tanzania Publishing House.
Madhumuni
falsafa,
habari,
kazi,
kiswahili,
kitabu,
Maarifa,
Maendeleo,
maisha,
Malengo,
Mgodi Unaotembea,
Nyasa
October 21, 2017
FUAMBAI SIA AHMADU: MWANAMKE ANAYETETEA UKEKETAJI AFRIKA.
Na KIZITO MPANGALA
FUNAMBAI SIA AHMADU alizaliwa mwaka 1969 nchini Sierra Leone katika jamii ya kabila la Kono kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Alifanya kazi na UNICEF nchini Gambia.
Madhumuni
Malengo,
malezi,
mapenzi,
maswali magumu,
Nyumbani
February 04, 2013
CHOMBEZO: WEKA MALENGO MAISHANI
![]() |
| Markus Mpangala |
Ni mwenyezi Mungu anayetuweka hai kwenye hii dunia huku
wenyewe tukichukua jukumu la kujilinda dhidi ya hatari zozote. Leo ninapenda kukuelezea jambo lililonishangaza zaidi
ingawaje nilikwisha simuliwa nyakati fulani na baadhi ya wanazuoni, na lenye
elimu muwali. Jambo hili ndilo linalenga kukuuliza maswali haya; wewe ni
mfanyakazi kwenye ofisi fulani, hivi unafanya kazi ili iweje? Labda wewe huna kazi, unaishi ili iweje? Kwanini huna kazi
au shughuli yoyote? Lau umri wako mdogo au hujapata kazi, unadhani kuna umuhimu
wa kazi? Na kwanini unaona kuna umuhimu wa kuishi kama ulivyo?
Wengine ni wafanyabiashara na mengineyo; hivi katika maisha yako una malengo
gani? Yaani unaamka mapema, unakwenda kazini aidha kwa usafiri wako au wa jamii
(Daladala).
Unakwenda ofisini kufanya nini? Lengo lako hasa ni nini
kadiri mshale wa saa unavyokwenda hapa duniani? Unaishi ili kufanya nini?
Kwanini unadhani una haki ya kuishi na si yule au mimi? Lengo lako la kuishi liko wapi? Sababu yako ya kufanya kazi
iko wapi? Ndiyo, unapenda cheo, halafu iweje? Ukishakupata cheo hicho unalengo
gani na maisha yako?
Unadhani cheo chako kitaisaidia nini ofisi yako? Kwanini
wewe unapenda sana kupendelewa? Unapotaka kupendelewa je, wewe umewafanyia
upendeleo wenzako? Unadhani ukipendelewa wewe ni muhimu kuliko yule na mimi?
Lengo lako la kupendelewa ni nini? Unapenda kupewa kuliko wewe kutoa? Lengo
lako ni nini hasa?
Jiulize sana msomaji ili tuende sambamba nikupe jambo hili.
Tueleweshane hapa kwamba kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweka malengo katika
maisha yetu haya. Kama wewe huna ndoto basi hutafanikiwa. Kama wewe huna maono
maishani, basi una kazi kubwa kujitambua. Una kazi kubwa ya kutambua uendako. Ni lazima uanze kufikiri sasa, maana mtu mwerevu huzifikiria
hatua zake. Basi tusiende mbali msomaji mpenzi, nakupenda sana, tambua hilo.
![]() |
| Shaban akitimiza majukumu yenye malengo ofisini kwake |
Sikiliza sasa, Aprili 19 mwaka huu nilinunua kitabu cha
“Barrack Obama: Yes, We Can”, kimeandikwa na Lila Luce. Mambo yaliyomo kitabuni
ndiyo yananifanya nitafakari nawe leo kupitia safu hii. Rudi juu anza kusoma upya halafu uelewe zaidi. Kwenye kitabu
hiki kuna mambo ambayo sikujua kuhusu Rais huyu wa Marekani. Inachekesha na
kuelimisha, lakini ukweli maisha aliyopitia Barrack Hussein Obama (jina lake la
utani Barry O’Bomber) kuna mengi ya kujifunza.
Ukisema mitishamba, Obama amenyweshwa sana kule Kogelo,
Kenya. Ukisema Daladala, basi Obama amepanda sana pale Kenya (huita Matatu).
Obama alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya (teja) enzi za ujana wake, tafakari
hilo.
Obama ana kauli mbiu ya “Mabadiliko”. Mabadiliko ni dhana
ambayo ilitokana na aliyoona na kuishi maishani mfano Kogelo na Indonesia.
Tusione Obama anaongoza Marekani, alilumbana na mkewe (Michelle Obama) kwa wazo
la Urais. Michelle akamwita msaliti, hamwelewi anafikiria nini juu ya
familia, alimwambia; “mume wangu nitawezaje kulea mabinti hawa wawili (Natasha
na Malia) peke yangu?
Lakini Obama alimjibu mkewe, “tafadhali hii ni mara yangu ya
mwisho, kabla ya kuishi kwa utulivu mke wangu, niruhusu.” Msomaji unapaswa kutambua kuwa wakati anagombea kuwa Useneta
alitofautiana na mkewe, lakini aliruhusiwa kwa ahadi hatawania kiti kingine.
Obama anakufunza mengi; alifundishwa imani ya Ukristu na
akawa mkristu, akajifunza Uislamu alipokuwa Indonesia, kwahiyo dini zote
kazipitia kabla ya kufunga pingu za maisha kwa Mchungaji Jeremiah Wright. Alifundishwa mila na desturia za Wamasai. Alishatumia
Vibatari kule Kogelo, Kenya. Alitembea kwa miguu vijijini, hakika ni mengi mno.
Hata hivyo kauli aliyomwambia mkewe wakati anaomba amruhusu kuwani Urais ndiyo
inatuleta hapa leo msomaji.
Awali alisema, ‘Nimeona nafasi ya kushinda’. Hii ilitokana
na malengo yake aliyoweka ili kutimiza ndoto zake. Akamjibu mkewe, ‘hii ni
nafasi ya mwisho mke wangu. Nahitaji kuyafanyia kazi mawazo yangu kabla
sijatulia na kuishi kwa amani kwenye familia yetu.”
Hii inakuonyesha ndoto zake maishani. Inakuonyesha malengo
yake maishani. Inakupa mwanga wa kutengeneza sura mpya na kuacha ya kale. Inakupa
matumaini mapya ambayo lazima utayatendee kazi.
![]() |
| Rafiki yangu Shaban a.k.a Don King, akiwa ofisini kwake |
Lazima uwe na malengo maishani msomaji. Ujue dhumuni lako
maishani. Tambua hakuna aliyeandikiwa kufanikiwa au kupewa uhalali wa kukusanya
mafanikio yote. Hayupo binadamu aliyeshushiwa mafanikio kutoka mbinguni bila
kuweka mkazo kwenye malengo yake. Anza kutimiza ndoto zako kwa kuweka malengo
yafanyayo kazi. Amini juhudi zako na mawazo yako ni muhimu mno kwa jamii.
Jamii inahitaji mawazo yako ambayo unatakiwa kuyatendea
kazi. Fanya kazi kwa bidii ukiwa unajua dhumuni lako ni lipi. Tumia kipato
chako kwa uangalifu maana huwezi kujenga nyumba ukiwa mwingi wa starehe. Wapo wajinga wachache hawaweki akiba na kila kukicha
wanalalamika maisha magumu. Ndugu yangu kama huna malengo maishani ni bure.
Utaishi kulingana na mazoea tu yaliyomo.
Unakwenda kazini, mwisho wa mwezi ukifika mshahara wote
unalipa madeni. Halafu eti unataka kulingana na tajiri wa Mexico Carlos Slim au
Tokyo Sakswalle wa Afrika Kusini. Mafanikio hutengenezwa, katu mafanikio
hayakutengezi wewe. Ukitaka kufanikiwa lazima ujue njia zake halali na kubuni
mpya ambazo zitakupa sura mpya ya maisha yako. Ndoto zako zitakupa msukumo wa
kufanikiwa.
Anza sasa kupanga vipaumbele. Pima kipato chako kama kinakuruhusu
kufanya yanayokuzidi. Mawazo yako mazuri yakuongoze ili ufanikiwe. Tumia 80%
kufuatilia fursa zilizopo na mpya.
Madhumuni
amani na upendo,
kumbukumbu,
Malengo
Subscribe to:
Posts (Atom)







