Showing posts with label Tangazo. Show all posts
Showing posts with label Tangazo. Show all posts
February 16, 2018
DK. SLAA ATEULIWA KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI SWEDEN
January 17, 2018
WASHINDI WA TUZO ZA USHAIRI NA FASIHI
January 05, 2018
TANZIA; MWANAHABARI WA SERIKALI AFARIKI DUNIA
Madhumuni
Tangazo
October 21, 2017
MBUNGE WA CHEMBA AONDOA HOJA YA KUONGEZA MUDA WA UBUNGE
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MBUNGE wa Chemba Juma Nkamia (CCM)amesema ameondoa kwa
muda kusudio lake la kutaka kuwasilisha muswada binafsi wa mabadiliko ya Katiba
unaohusu kuongeza ukomo wa Bunge.
![]() |
| JUMA NKAMIA |
Nkamia ambaye aliwasilisha kusudio hilo katikati ya mwezi uliopita mjini Dodoma kwa mujibu
wa kanuni ya 81(2) ya kanuni za Bunge toleo la 2016,kupitia barua yake aliyoisaini
Septemba 12 iliyokuwa ikipendekeza
kuongeza muda wa bunge kutoka miaka mitano hadi saba na kupunguza wa uongozi wa
vijiji kutoka
miaka mitano hadi minne.
Kupitia ujumbe mfupi aliouandika
katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp,alisema ameamua kuondoa kusudio hilo baada ya mashauriano na maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM).
“Ndugu viongozi wenzangu
naomba kuwataarifu kuwa baada ya mashauriano na maelekezo ya viongozi wa juu wa chama(CCM) na hali ya
kisiasa katika nchi kadhaa za
Afrika Mashariki nimelazimika kuondoa kwa muda hoja yangu
binafsi ya ukomo wa Bunge niliyokusudia kuiwasilisha katika bunge lijalo,”aliandika
Nkamia.
Mbali na andiko hilo gazeti
hili pia lilimtafuta Nkamia kupitia simu yake ya kiganjani ili kumuuliza
kama na sababu nyingine zaidi ya
alizozitaja kupitia ujumbe huo mfupi na
lini atakuwa teyari kuwasilisha tena muswada huo alisema.
“Naomba ibaki hivyo hivyo kama
ilivyo kwenye meseji sina cha
kuongeza,kuhusu ni lini nitapeleka tena nayo subiri kwa sababu nimesema
nimesitisha kwa muda maana yake nitawasilisha tena nitakapokuwa teyari,”alisema
Nkamia.
Hoja
ya Nkamia ambayo ilianzia katika Bunge lililopita ilikuw aikipingwa na
wanazuoni pamoja na wanasiasa wakongwe akiwemo Spika Mstaafu wa Bunge Pius
Msekwa.
Msekwa
ambaye alikuwa akiongea na televisheni ya Azam
mwishoni wa wiki hii alisema
chama cha CCM hakiwezi kukubaliana na maoni au mpango wa
kuongeza muda wa kiongozi yeyote kutoka kipindi cha miaka mitano kilichopo
kikatiba kwa sasa.
Msekwa alisema kwa uzoefu wake
bungeni tayari anaona kuna tafakari nyingi zilizofanywa kabla ya Taifa kuamua
kipindi cha utawala kuwa miaka mitano na si vinginevyo.
Alisema hoja hiyo inabidi
iangaliwe kwa umakini mkubwa kutokana na ukweli kuwa, iwapo kiongozi atakuwa
mbaya, maisha yanaweza kuwa ya mateso kupitia kiongozi huyo na kuongeza kuwa
hilo hata Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere aliliona hilo.
“Ni kwamba miaka kumi tu
inatosha, ili kama mtu ni mbaya tuvumilie kwa hiyo miaka kumi, na siyo kwamba
haikufikiriwa. .na sidhani kama CCM itakuwa na nafasi ya kujadili hilo kwa
sasa” alisema Msekwa. Mbali na Msekwa wasomi
wakiwemo Dk.Benson Bana nao walimpinga huku akisema kuwa lengo lake lilikuwa ni
kujipendekeza kwa Rais Dk. John Magufuli ili ampe uwaziri.
November 05, 2013
DC MUHINGO: TAMASHA LA HANDENI NI FURSA YA KIMAENDELEO
Na Mwandishi
Wetu, Handeni
MKUU wa wilaya Handeni, DC Muhingo Rweyemamu,
amewataka wananchi wa Handeni, mkoani Tanga kulitumia Tamasha la Handeni
linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mjini hapa kwa ajili ya kutafuta fursa za
kimaendeleo na kuwapatia maisha bora Watanzania wote kwa kupitia sekta ya
utamaduni.
Akizungumza jana mjini Handeni, Muhingo alisema
kutokana na tamasha hilo kufanyika mwisho wa mwaka, Desemba 14, itakuwa chachu
ya kuwaunganisha watu wote, sanjari na kujadili changamoto zinazoikabiri
Handeni na Tanzania kwa ujumla.
Muhingo alisema kuwa tamasha hilo lina umuhimu
mkubwa kutokana na kuandaliwa maalum kwa ajili ya Watanzania kwa ajili ya
kuangalia ngoma na matukio mbalimbali ya kijamii.
“Wakati napongeza kwa dhati kuandaliwa kwa tamasha
hili wilayani hapa, pia nawaomba watu waje kwa wingi kushuhudia namna gani
Handeni imepiga hatua kimaendeleo na kuangalia namna gani wanaweza kusonga
mbele.
“Naamini tutafikia hatua nzuri kwa kushirikiana na
wadau wote, hivyo wale wanaoishi mbali na Handeni pia ni wakati wao kurudi
nyumbani mwishoni mwa mwaka kujifunza mambo ya utamaduni wao, sanjari na
kufanya juhudi za kupiga hatua kimaendeleo,” alisema.
Tamasha hilo linaloandaliwa na Mratibu wake Kambi
Mbwana, hadi sasa limedhamiwa na Phed Trans, Clouds Media Group, Grace
Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles &
Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country
Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.
Wengine ni duka la mavazi la Chichi Local Ware,
Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia
kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog,
Jiachie Blog na Taifa Letu.com, huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi hadi
saa 12 za jioni.
Madhumuni
kumbukumbu,
Tangazo
November 04, 2013
TAMASHA LA UTAMADUNI HANDENI NA MIPANGO KABAMBE YA KIMAENDELEO
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ILI kujenga jamii bora na yenye
kujua tamaduni zao, kunahitajika kuandaliwa matamasha muhimu yenye dhamira ya
kweli katika kona mbalimbali za nchi yetu. Huo ni mpango mzuri na wenye tija.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo
Rweyemamu, pichani.
Katika suala hilo, wale wadau
wanaotarajia au waliowahi kuandaa matamasha ya aina hiyo ni dhahiri wanatakiwa
waungwe mkono badala ya kukatishwa tamaa.
Kwa sasa, tamasha ambalo linatajwa
katika vinywa vya watu wengi ni lile la Handeni, linalotarajiwa kufanyika
Desemba 14, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Tamasha hilo la utamaduni na michezo
linatambulika kwa jina la ‘Handeni Kwetu,’ jina lililotokana na mtandao ‘blog’
ya Handeni Kwetu.
Mratibu wa Tamasha la Handeni, Kambi
Mbwana, pichani.
Vyovyote litakavyotajwa na wadau wa
matamasha duniani kote, ili mradi linatimiza na kutoa majibu halisi ya namna ya
kutangaza na kukuza utamaduni wa Tanzania, si vibaya na njia ya kulitangaza
mbele ya jamii.
Katika mazungumzo yaliyofanyika
mapema wiki hii, mwishoni mwa wiki iliyopita, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo,
Kambi Mbwana, anasema kuwa lengo la kuandaa tamasha hilo ni kushirikiana na
serikali na wananchi wote kujua mbinu imara za kuutangaza utamaduni wetu.
Mbunge wa Handeni na Waziri wa
Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda, pichani.
Anasema kwa maeneo kama Handeni na
kwingineko, kumekuwa na changamoto kubwa za wananchi kuacha utamaduni wao na
kufuata wa wenzao jambo linalotakiwa lipingwe vikali.
“Nilikaa chini na kutafakari namna
gani ya kuwaunganisha watu wote katika tukio moja na kuwa sehemu ya wao
kuangalia ngoma zetu, nyimbo zetu na mbinu za kijamii kwa ujumla wake.
“Naamini katika umri wa taifa letu
la Tanzania, kuna mengi yametokea na yaliwahi kutokea hasa wakati wa ukoloni,
hivyo naamini siku hiyo tutajua ni kiasi gani watu wa asili ya Handeni walikuwa
na mchango kwenye jamii yao,” alisema Mbwana.
Mbwana ambaye ni mwandishi wa habari
na mmiliki wa ‘blog’ ya Handeni Kwetu (www.handenikwetu.blogspot), anasema
kwamba kwa kukutana watu wote ni sehemu ya kuangalia namna ya kulitumikia taifa
letu la Tanzania na kubuni mbinu za kujikomboa kiuchumi.
Mdau huyo wa mambo ya utamaduni,
michezo na sanaa kwa ujumla wake ukiwamo muziki, anasema kwamba Handeni ni
miongoni mwa wilaya zenye changamoto kubwa hivyo kuna haja ya wadau wote
kukutana kwa pamoja na kuangalia namna ya kuzitatua, hasa kwa kupitia tamasha
hilo.
“Huu si wakati wa kuangalia Mkuu wa
Wilaya (DC) Muhingo Rweyemamu anafanya nini au Mbunge Abdallah Kigoda na
viongozi wote wa serikali, ila jambo la muhimu ni kushirikiana nao kuleta
maendeleo.
“Mtu wa kwanza katika maendeleo ni
mwananchi mwenyewe, hivyo naomba kuwakaribisha Watanzania na hata wale wasiokuwa
Watanzania kukutana pamoja na sisi kwenye tamasha hili,” alisisitiza Mbwana.
Aidha, Mbwana anatumia muda huo
kuwaomba wadau wote, wakiwamo viongozi wa serikali, mashirika na kampuni
kujitokeza kudhamini tamasha hilo litakalokuwa la aina yake. Tamasha la Utamaduni la Handeni
Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza, likipangwa kuanza saa tatu asubuhi hadi
saa 12 jioni, ambapo vikundi mbalimbali vya sanaa vitashiriki.
Ili kuleta hali ya kimkoa, Mbwana
anasema juhudi zinafanyika kupata vikundi katika baadhi ya wilaya za Mkoa wa
Tanga ili kuimba nao, kucheza nao na kushiriki nao katika jambo la kimaendeleo. Mdau huyo wa habari anasema kwamba
hadi sasa wadau kadhaa wamejitokeza kudhamini tamasha hilo linalotikisa katika
maeneo ya Handeni na Tanzania kwa ujumla.
Anawataja wadau hao kuwa ni pamoja
na Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho kwa kupitia
Kampuni yake ya Yusuphed Trans, yenye magari yanayotoka Dar es Salaam kwenda
Mkata, wilayani Handeni, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa
Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist,
Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.
Wengine ni duka la mavazi la Chichi
Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa
kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason
Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.
Mbwana anasema kwamba kwa kupitia
tamasha hili, wadau wote watapata fursa ya kutangaza biashara zao, ukizingatia
kuwa tamasha hili linatarajia kukutanisha watu wengi zaidi sehemu moja. “Tunaomba udhamini kwa watu wote ili
tushirikiane katika kufanikisha tamasha hili la kihistoria, huku tukiamini kuwa
wenzetu wa Kilindi, Korogwe tutakuwa nao pamoja.
“Maandalizi yanaendelea kuhakikisha
kuwa tunafanya kitu cha tofauti katika tamasha hilo, nikiamini kuwa mguso huu
utaendelea kushika kasi na habari hizi njema kuenea nchini kote,” alisema. Mbwana anasema kwamba wazo la
kufanyika kwa tamasha hilo limepewa baraka na viongozi wote, akiwamo DC
Rweyemamu na Mbunge, Abdalah Kigoda, ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na
Biashara.
Anasema kuwa kwa kufanyika kwa
tamasha hili ni muendelezo wa mipango mingi mizuri ya kimaendeleo
itakayoandaliwa kwa kushirikiana na Watanzania wote, hususan wananchi wa Handeni. Mwisho kabisa Mbwana alitumia muda
huo kuwakumbusha wafanyabiashara mbalimbali wilayani Handeni na Tanga kwa
ujumla, kuingia moja kwa moja katika tamasha hili la aina yake.
Madhumuni
kumbukumbu,
Tangazo,
utamaduni
January 02, 2013
TAARIFA KWA WAWEKEZAJI WAPYA KATIKA KILIMO CHA MITI YA MBAO, KARATASI NA NGUZO.
Fresh Farms & Tours (T), biashara tanzu ya Anesa Co.,Ltd
(Nyaluke Business Empire); inajishughulisha na upandaji, utunzaji na
uendelezaji wa mashamba ya miti ya mbao, karatasi na nguzo-mkoani Iringa.
Vilevile inahusika na uvunaji na usambazaji wa mazao ya miti, (mbao na nguzo za
umeme) sambamba na ufugaji.
Fresh Farms ilianzisha programu maalumu, mapema
mwaka jana; inayolenga kuwawezesha watanzania wengine kuwekeza katika kilimo
cha miti kwa urahisi. Tayari makumi ya watanzania wamechangamkia fursa hii.
Fresh Farms & Tours (T) tunapenda kuwaarifu wale wote wenye nia ya kuwekeza
nasi; KWAMBA kuanzia tar 1, Feb, 2013 kutakuwa na mabadiliko ya bei na gharama
za uendeshaji kwa mashamba ya miti.
Mashamba tunayoyauza laki sita kwa sasa;
bei mpya itakuwa milioni moja; na yale tunayouza laki nane gharama yake itakuwa
milioni moja na nusu. Bei hizi hazitawaathiri wateja wa awali na wale ambao
wamekwisha wasilisha oda zao. Fresh Farms & Tours (T) tunaendelea kuboresha
huduma, taarifa na usaidizi kwa wote wanaowekeza nasi.
Fresh Farms & Tours
(T) tunakutakia heri ya Mwaka mpya wa 2013 na tunakukumbusha ile salamu
yetu (motto); "Greening the world and Feeding People".
IMETOLEWA NA:
Albert Nyaluke Sanga
Mtendaji Mkuu-Fresh Farms & Tours(T), (C) 2012
Madhumuni
Tangazo
Subscribe to:
Posts (Atom)




