Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts
January 17, 2018
WASHINDI WA TUZO ZA USHAIRI NA FASIHI
January 12, 2018
SERIKALI YA BOTSWANA YAMKOROMEA RAIS TRUMP
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya Botswana kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imetoa taarifa ya kulaani matamshi ya rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji kutoka bara la Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara
hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari ilisema, serikali imeamua kumwita balozi
wa Marekani nchini humo ili kutoa ufafanuzi juu ya matamshi ya Trump na kueleza
nafasi ya Botswana katika kundi lililomaanishwa na rais huyo wa Marekani.
January 04, 2018
SALAMU KUTOKA MBAMBA BAY, ZIWA NYASA
![]() |
| Honorius Mpangala |
Miundombinu
ya Barabara mibovu, eneo la mlima wa Malongo, Kata ya Kihagara ni korofi na
sumbufu miaka nenda rudi. Ukifika baadhi ya maeneo ya kijiji cha Chinula
ukorofi wa mlima Malongo nao uko vilevile. Mvua ikinyesha tu ni shida hata
pikipiki kupandisha mlima haiwezekani. Utelezi uko eneo kubwa sana la Mlima Malongo
na kijiji cha Chinula.
Madhumuni
falsafa,
habari,
mawazoni,
mbamba bay,
Nyasa
NYASA YAKAMILISHA UJENZI WA BWENI YA WANAFUNZI
NA MWANDISHI WETU, NYASA
Bweni hilo ambalo linaonekana picha linatarajiwa kuchukua idadi ya wanafunzi Wanafunzi 312 hivyo kuondokana na tatizo la makazi ya wanafunzi katika wilaya hiyo. Ujenzi wa Bweni hilo umetokana na juhudi za ushirikiano na Mbunge wa Jimbo la Nyasa ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya pamoja na wadau mbalimbali.
HALMASHAURI ya Wilaya Nyasa
inamilisha ujenzi wa Mabweni ya Wasichana katika Shule ya Sekondari ya Mbamba
bay (Mbamba Bay High School) iliyopo mjini Mbamba ikiwa ni njia ya kukamilisha
mpango wa elimu bora kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Bweni hilo ambalo linaonekana picha linatarajiwa kuchukua idadi ya wanafunzi Wanafunzi 312 hivyo kuondokana na tatizo la makazi ya wanafunzi katika wilaya hiyo. Ujenzi wa Bweni hilo umetokana na juhudi za ushirikiano na Mbunge wa Jimbo la Nyasa ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya pamoja na wadau mbalimbali.
January 01, 2018
HERI YA MWAKA MPYA 2018! NGUVU YA HABARI
“Kama
habari zozote ziwe nzuri au mbaya za sehemu yoyote hazisemwi au kutangazwa
maana yake ni upenyo kwa wenye mamlaka “kutojali” kwasababu watasema, “nani
atajua”. Kama habari mbaya zikisemwa maana yake inawazindua wenye mamlaka au
watu wengine kufahamu kinachoendelea sehemu hiyo.
"Kama habari nzuri zikisemwa maana yake zinavutia wengine kama fursa na mwelekeo mpya wa kijamii au kiuchumi. Tumia nyenzo yoyote kuhabarisha hata ikiwafikia marafiki zako watano tu inatosha sana kwasababu nguvu zake kubwa kuliko kubaki na fikra duni kuwa "nani anazitaka".
"Kanda ya kusini ingali na nguvu ndogo sana katika habari. Mkondo wa habari Kanda ya kusini umekuwa duni kwasababu zifuatazo: wapashaji habari wachache wenye nguvu katika taasisi, wapashaji habari binafsi hawaoni umuhimu (sawa na kusema nina mambo yangu nyeti), miundombinu hafifu, kutojali au baadhi kukosa nyenzo. Lakini suluhisho lipo; hizi ni zama za Uandishi wa raia (Citizen Journalism), ambapo mitandao ya kijamii (Blog, Facebook, Instagram, Twitter, Tagged, Badoo, LinkedIn, Vk, Connect, YouTube, Vimeo, Skype, Tumblr,Flickr, WhatsApp, inachukua mkondo mkubwa wa habari kama ilivyokuwa Blogu miaka ya mwanzoni mwa 2000.

December 06, 2017
MAZOEZI YA KIJESHI KUFANYIKA NCHINI
Tanzania imechaguliwa kuwa
mwenyeji wa mazoezi ya siku 14 ya pamoja ya makamanda wa kijeshi wa nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki yanakayojikita katika kupambana na
matukio ya ugaidi. Mazoezi yatafanyika
katika kituo cha ulinzi wa amani cha jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ
Kunduchi jijini Dar es Salaam.
December 04, 2017
MELI YA ABIRIA YAENDELEA KUUNDWA
MWANDISHI WETU, KYELA
KAZI ya kuunda meli mpya ya abiria itakwayokuwa na uwezo wa kubeba abiria
200 pamoja na tani 200 za mzigo imefikia asilimia 60 tangu ilipoanza kutengenezwa mapema mwaka huu katika Bandari ya Kiwiwara wilayani hapa.
Taarifa kutoka wilayani hapa zinasema kuwa kazi hiyo inafanywa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kupitia kampuni ya kizawa ya Songoro. Kampuni hiyo ndiyo ilikamilisha meli mbili za mizigo, MV Ruvuma na MV Njombe
zinazofanya shughuli zake ndani ya Ziwa Nyasa.
Meli hiyo mpya inayoundwa inatarajiwa kusaidia kupunguza
matatizo ya usafiri katika Ziwa Nyasa pamoja na Wilaya ya tatu za Nyasa
(Ruvuma), Ludewa (Njombe) na Kyela (Mbeya) ambazo zimekuwa na shughuli nyingi za maendeleo lakini usafiri ulikuwa wa shida.
UJENZI BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BAY WAKARIBIA
NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ujenzi wa barabara ya lami nzito toka Mbinga wilayani Mbinga hadi mjini Mbambabay Wilayani Nyasa unatarajia kuanza hivi karibuni.
BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA RC MDEME
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ujenzi wa barabara ya lami nzito toka Mbinga wilayani Mbinga hadi mjini Mbambabay Wilayani Nyasa unatarajia kuanza hivi karibuni.
Mndeme amesema hayo wakati
akitoa taarifa ya kufungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Ruvuma,
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea Novemba 29 mwaka huu, wiki
iliyopita.
Madhumuni
habari,
maisha,
Malengo,
maswali magumu,
Nyasa
December 01, 2017
RASMI: MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018
Madhumuni
habari
November 16, 2017
MV NJOMBE INAVYOFUNGUA FURSA KWA WAKAZI ZIWA NYASA.
![]() |
| Honorius Mpangala, 0628994409 |
AKIWA katika kampeni za urais mwaka 2005 Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete katika ardhi ya Kyela Mkoani Mbeya alihaidi meli. Alirudia tena kauli hiyo alipokuwa katika ardhi ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma. Baada ya kipindi cha utawala wake hatimaye meli alizoahidi tayari zimeonwa na Wanyasa.
MV Njombe imekamilika na kufanikiwa safari moja ya majaribio kutoka Bandari ya Itungi
hadi Mbamba Bay. Yapo mambo ambayo ni
fursa kwa wakazi wa Nyasa kutokana Meli hii. Kama inavyoitwa ni meli ya mizigo
ni chombo kitakachoweza kuwainua kiuchumi wakaza wa Nyasa kama watakitumika
ipasavyo. Kuinuka kiuchumi kutatokana na kujikita katika shughuli ambazo wakazi
wake watajishughulisha na shughuli kama ilivyo kilimo biashara na hata ufugaji
wa kisasa na wenye tija katika maisha ya leo.
Kilimo
cha biashara ni moja ya ujasiriamali ambao watu wengi wamekuwa
wakijishughulisha nao. Katika mwambao wa Ziwa Nyasa hususani wilaya Nyasa yapo
mabonde ambayo yanaweza kufanyika kilimo cha mazao ya muda mfupi na kwa mfumo
wa kilimo cha umwagiliaji, na kile cha kutegema mvua na kuleta tija.
Madhumuni
ajira,
Biashara,
habari,
Imani,
Kilimo,
Linda,
liuli,
Matenje,
Mbaha,
mbamba bay,
Nyasa,
Uchumi
November 15, 2017
G40 HOI. GRACE MUGABE AKIMBIA NCHI
Madhumuni
diplomasia,
habari
TAARIFA FUPI YA MWENYEKITI WA SADC
Madhumuni
habari
MANISPAA YA SONGEA KUNUNUA MAHINDI TANI 400
NA MWANDISHI WETU, SONGEA
Afisa Kilimo wa Manispaa ya
Songea Mushoborozi Christian amesema Halmashauri hiyo imepokea barua toka NFRA
inayotoa maelekezo ya ununuzi wa mahindi katika awamu ya tatu msimu wa mwaka
2017/2018.
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma imepangiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA)
katika msimu huu kununua mahindi tani 400.
![]() |
| Picha kwa Hisani ya Manispaa ya Songea. |
TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA ZIMBABWE
GOOD MORNING/AFTERNOON
Fellow
Zimbabweans, following the address we made on 13 November 2017 which we believe
our main broadcaster, ZBC and The Herald were directed not to publicise, the
situation in our country has moved to another level.
Firstly,
we wish to assure the nation that His Excellency, The President, of the
Republic of Zimbabwe, Head of State and Government and Commander in Chief of
the Zimbabwe Defence Forces, Cde R.G Mugabe and his family are safe and sound
and their security is guaranteed. We are only targeting criminals around him
who are committing crimes that are causing social and economic suffering in the
country in order to bring them to justice.
HALI YA ZIMBABWE MCHANA HUU
1.Waziri wa Fedha wa Zimbabwe Ignatius
Chombo amekamatwa na Jeshi la Zimbabwe. Pia wanajeshi wameua walinzi watatu wa
waziri huyo. (Chanzo: PaZimbabwe).
2. Jeshi hilo pia lilitembelea nyumbani
kwa Profesa Jonathan Moyo ambaye ni waziri wa elimu ya juu, amekamatwa (Chanzo:
NewsDay)
3.Baadhi ya mawaziri
wameripotiwa kutoroka, wakiwemo Saviour Kasukuwere na Makamu wa rais Phelekezela Mphoko anayedaiwa
kukimbilia Afrika kusini.
Madhumuni
habari,
Sayansi na Teknolojia,
siasa,
siasa.
MFAHAMU NDEGE ANAYEJENGA NYUMBA NA KUPANGISHA
NA
MWANDISHI WETU
KAMA
ulidhani ni binadamu pekee anajenga nyumba na kupangisha utakuwa unajidanganya
kwa kuwa mwambao mwa ziwa Nyasa katika Kijiji cha Mtupale kata ya Chiwanda,kuna
aina ya ndege anayeitwa Fundichuma (Hamerkop) ambaye anajenga nyumba na
kupangisha kwa ndege na viumbe wengine kama mijusi.

Afisa
Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe ambaye pia ni mzaliwa wa
mwambao mwa ziwa Nyasa anasema ndege huyo anapenda kuishi jirani na ziwa au mto
kwa sababu chakula chake kikuu ni samaki.
HALI YA ZIMBABWE LEO
Madhumuni
habari
November 13, 2017
ASKARI WA BARABARANI NI KIBOKO. TAZAMA FAINI YAO
Madhumuni
habari
LULU ATUPWA JELA MIAKA MIWILI
"KILA mchezo huwa na
kanuni zake. Kama mapenzi ni mchezo basi wivu ni moja ya kanuni zake. Kama mshitakiwa
alijua kuwa marehemu alikuwa na wivu uliokithiri, basi alipaswa kuishi naye
kutokana na hali hiyo"...
JAJI S RUMANYIKA.
Mahakama kuu leo. 13. 11. 2017.
NB:…Pole sana Lulu. Umepitia
mambo mengi makubwa kuliko umri wako.
![]() |
| ELIZABETH MICHAEL "LULU" |
Madhumuni
habari
KWANINI SEKRETARIETI YA AJIRA HAINA MATAWI NCHINI?
NA MARKUS MPANGALA
MIAKA kadhaa iliyopita nilishindwa kuwaelewa kabisa watendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) hapa nchini. Nilikuwa siwaelewi kwa sababu siku moja niliwahushudia wafanyabiashara fulani kutoka Songea mkoani Ruvuma, wakizunguka vyumba vya ofisi vya taasisi hiyo kwenye jengo la Ushirika liliko Barabara ya Lumumba, Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kwa madhumuni ya kusajili kampuni yao.

| Jenista Mhagama |
Pili,niliwahi kumsaidia rafiki
yangu, Albert Nyaluke Sanga, ambaye ni mfanyabiashara mkubwa mkoani Iringa, ili
apate leseni ya biashara. Haikuwa leseni yake binafsi, bali aliamua kumsaidia
kijana mmoja aliyekuwa na ndoto za kuwa mfanyabiashara, lakini alikosa pa
kunzia.
Rafiki yangu huyo anapenda
kuwasaidia vijana wanaojishughulisha na ujasiriamali kwa sababu anaamini hiyo
ndiyo njia pekee ya kuwakomboa, badala ya elimu yao na kuondokana na matembezi
ya kusambaza bahasha za kuomba nafasi za kazi.
Madhumuni
afya,
ajira,
amani na upendo,
Digitali,
elimu,
habari,
jamii,
Katiba,
kazi,
mafundisho
Subscribe to:
Posts (Atom)