1.Waziri wa Fedha wa Zimbabwe Ignatius
Chombo amekamatwa na Jeshi la Zimbabwe. Pia wanajeshi wameua walinzi watatu wa
waziri huyo. (Chanzo: PaZimbabwe).
2. Jeshi hilo pia lilitembelea nyumbani
kwa Profesa Jonathan Moyo ambaye ni waziri wa elimu ya juu, amekamatwa (Chanzo:
NewsDay)
3.Baadhi ya mawaziri
wameripotiwa kutoroka, wakiwemo Saviour Kasukuwere na Makamu wa rais Phelekezela Mphoko anayedaiwa
kukimbilia Afrika kusini.
4. Waziri wa mambo ya nje, Walter
Mzembi amekwenda Zambia kukutana na rais Edgar Lungu kwaajili ya kupata ushauri
(Chanzo: PaZimbabwe).
5. taarifa zinasema kuwa
kiongozi wa Umoja wa Vijana wa chama cha ZANU-PF, Kudzanai Chipanga ambaye
aliitisha mkutano na vyombo vya habari kulipinga Jeshi la nchi hiyo amechukuliwa
na Polisi akiwa nyumbani wake mjini Harare (Chanzo: NewsDay).
6. Viongozi watatu wa kundi la
G40 linalofanya kazi ndani ya chama cha ZANU-PF na kusababisha migogoro
wameripotiwa kukamatwa na Jeshi. G40 ndilo kundi lililosababisha kufukuzwa
makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa (Chanzo; NewsDay)
7. Wanajeshi wanaulinda pia
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Mugabe (Chanzo; NewsDay).
8. Jeshi limedhibiti barabara
ya Samora Machel na barabara ya Mtaa wa Sam Nujoma ambayo inakwenda moja kwa moja hadi nyumbani
kwa Robert Mugabe, marufu kwa jina la Munhu Mutapa (Chanzo: NewsDay).
IKUMBUKWE
Mkutano mkuu wa Chama cha
ZANU-PF ulitarajiwa kufanyika mwezi Ujao, ambapo pamoja na mengine ungetumika
kumchagua Makamu mpya wa rais.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako