Na, Stephano Mango, Songea
Ni takribani miezi nane sasa tangu nianze kufuatilia uendeshaji wa chuo cha
Ualimu Songea kama kinaweza kuendana na kauli mbiu ya sasa ya Serikali ya Big
Result Now (Matokeo Makubwa Sasa).
Nimelazimika kukifuatilia Chuo hicho kutokana na mgogoro mkubwa uliopo kati ya
wafanyakazi (wakufunzi) na mkuu wao wa chuo Ubaya Suleiman.
Mgogoro huo umetokana na uongozi mbovu usiozingatia misingi ya uongozi na
Demokrasia katika vyuo vya ualimu Tanzania kwani Mkuu huyo wa chuo amekuwa na
lugha za matusi,vitisho kwa wafanyakazi na wanachuo, kutopokea ushauri kwa
washauri wake, mbinafsi, kutowaamini watendaji wake kwa nafasi alizowateua,
kufanya kazi kwa kutumia vyanzo visivyo rasmi,
Matumizi mabaya ya fedha za Serikali na vyombo vya usafiri. Pamoja na hayo mkuu huyo wa chuo amediriki kuwapeleka baadhi ya wafanyakazi
wake kwenye vyombo vya dola (polisi) (kuwatishia) akiwatuhumu kuwa wanataka
kumuua. Baada ya mgogoro huo kutopata suluhu kupitia vikao vya ndani, Jitihada
zifuatazo zilifanyika na wafanyakazi wa chuo hicho ili kuleta hali ya amani na
utulivu wa chuo;
Tarehe 27/04/2013 walifanya kikao na mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti,
tarehe 15/05/2013 na tarehe 01/06/2013 walifanya kikao na Bodi ya ushauri ya
Chuo, hata hivyo suluhu ya mgogoro huo haikupatikana.
Kutokana na hali hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa
Sifuni Mchome aliunda tume ya watu watano ikiongozwa na Mkaguzi Mkuu wa shule
na vyuo wa nyanda za juu kusini ambaye alifahamika kwa jina moja la Lyapambile,
kuja kufanya utafiti wa chanzo cha mgogoro, lakini mpaka sasa tume hiyo
haijatoa majibu ya uchunguzi wa jambo hilo
Tume hiyo haikuishia hapo tarehe 13/08/2013 wafanyakazi walifanya kikao na Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, ambaye baada ya kusikiliza mgogoro huo
aliahidi kuleta suluhisho la kudumu mapema iwezekanavyo ili kuleta amani na
utulivu(peace and Tranquility) chuoni hapo. Lakini cha kushangaza hadi sasa
yapata miezi mitatu hakuna kilichofanyika hali ambayo imeendelea kuwavunja moyo
wafanyakazi wa chuo hicho.
Licha ya jitihada zilizofanywa, Mkuu huyo wa Chuo Ubaya Suleiman anaendelea
kuwanyanyasa wafanyakazi wake na kusema pigeni kelele lakini wakuning’oa mimi
hapa hayupo na lugha zingine ambazo sio za ustaarabu anazitoa, na kuwafanya
wafanyakazi wenzake wahoji nguvu aliyonayo katika utendaji, mfano wa lugha zake
mbovu ni “kwani mizizi yangu ni mirefu”. Kitendo hicho kinawafanya wafanyakazi
wa chuo na wadau wengine watilie mashaka juu ya sifa za uteuzi wake kushika
nafasi kubwa kama hiyo.
Tunamuomba Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Shukuru Kawambwa na Naibu wake
Philipo Mulugo kumuondoa mkuu huyo wa chuo madarakani na kumtafutia shughuli
nyingine ya kufanya kwa ustawi wa chuo cha ualimu songea, taaluma ya ualimu
Tanzania na ili kuleta ufanisi wa kauli mbiu ya serikali ya Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (Big Results Now)
Sababu zinazopelekea hilo ni nyingi ila kwa sasa nitazitaja chache ili kuweka
kumbukumbu sawa, ya kwanza Novemba 1, 2013 Mkuu huyo wa chuo bila kuwasiliana
na Mtaaluma wake wa Chuo Maiko Luoga, alidiriki kuwaandikia Barua Wakufunzi
kuwataka watunge Mtihani wa Moko wa Ualimu viwango vya Baraza la Taifa la
Mitihani(NECTA) kwa lugha ya kejeri hali ambayo imesababisha maudhi na utulivu
wa akili miongoni mwa wafanyakazi katika kufanikisha utungaji wa mitihani hiyo
Kitendo hicho licha ya kuwa ni kinyume na utawala bora , lakini pia kimekiuka
maagizo ya Bodi ya Chuo ambayo yalitolewa tarehe 28/8/2013 (……. mambo yote
yanayohusu fedha yaendeshwe kwa uwazi na ushirikishwaji mkubwa miongoni mwa
wanaidara / taasisi kwani inaonekana mambo yanaenda kwa usiri mno).
Sababu ya pili amekuwa na vitisho vingi katika utendaji wake na maneno ya
kuudhi dhidi ya viongozi wenzake , mfano wa maneno yake ambayo anayatamka huku
akigonga meza kuashiria ubabe na kiburi cha madaraka ni kama vile,(…. Ukiingia
ndani ya kumi na nane zangu nakumaliza, Angalieni msije mkaumia wengine
tunambavu za chuma, Nipo tayari kuua inzi kwenye kioo cha TV hata kama
itavunjika potelea mbalimbali raha yangu ni kuhakikisha inzi amekufa, Mkitoboa
mtumbwi nitahakikisha kabla sijazama mimi nawazamisha ninyi kwanza, Angalia
wengine watakaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune, Amekuwa akitishia
kung’oa mtu kwa kumwendea (kumpandia)wizarani ndani ya siku mbili na
kumchukulia barua ya uhamisho kwenda vyuo vya pembezoni mwa Tanzania, Mimi
nafanya haya hata niking’olewa kwa muda mfupi potelea pote nitakuwa nimejenga
historia).
Sababu ya tatu ni kutokuwa na uwazi, ukweli na ushirikishwaji kwa njia ya
kidemokrasia miongoni mwa idara zake katika chuo hicho na hasa katika fedha
ambazo zinakuja kwa ajiri ya manunuzi ya vitu mbalimbali, fedha ya kuendeshea
mafunzo ya ualimu kwa vitendo(BTP)
Fedha hiyo licha ya kuchelewesha kuitoa kutokana na ufisadi wake lakini pia
hakuitoa yote na wala hakueleza kwa uwazi na ukweli, hali ambayo haikuwezesha
wakufunzi kwenda kufanya kazi stahiki kwenye maeneo kusudiwa ya kuwatahini
wanachuo ambao walikwenda kwenye shule mbalimbali kwa ajili ya mazoezi ya
kufundisha kwa vitendo.
Sababu ya nne ni uwezo wake wa kiuongozi kwani kumekuwepo na mashaka mengi
katika Wasifu wake wa kielimu na kiutendaji, hali inayopelekea kuendesha Chuo
katika misingi binafsi bila kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu za Wizara.
Kutokana na hayo yote Chuo hicho kimejikuta kikiingia kwenye mgogoro wa muda
mrefu na mkubwa na kupelekea shughuli zote za kiutendaji chuoni hapo
kutofanyika katika viwango vyenye ubora na kwa wakati na hasa pale anaposafiri
mambo huwa yanasimama, kwani mara nyingi utendaji wote anaufanya yeye mwenyewe
na wakati mwingine huwa anajiita Chief Accountant na kumuona Makamu wake kuwa
hana uwezo wala mamlaka ya kutoa maamuzi kwa mustakabali wa chuo
Ni mengi ambayo nimeyabaini na ushaidi upo wazi kuwa Mkuu huyo wa Chuo hafai
kuendelea kuongoza Chuo hicho kwani Wakufunzi, Wafanyakazi na Wanachuo hawana
imani nae, na wanafanya mambo mengi bila morari ya utendaji kutokana na
mazingira mabovu ya utendaji kazi katika chuo hicho
Nimefanya jitihada za kukutana na baadhi ya Wakuu wa Idara Chuoni hapo na
kupata majibu ambayo yanaonyesha ukataji wa tamaa kutokana na mazingira mabovu
ya kiutawala ambayo yanaonyeshwa na Mkuu wa Chuo hicho katika kufanikisha
mpango mkakati wa matokeo makubwa sasa,
Pia nimebahatika kuwauliza viongozi wa Bodi akiwemu Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya
Chuo ambaye amejitambulisha kwa jina la H,Lugome naye pia ameonyesha masikitiko
makubwa sana juu ya utendaji wa Mkuu wa Chuo hicho
Lakini pia Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti ambaye pia ameshiriki
kusuluhisha mgogoro huo katika kikao chake cha April 27, 2013 lakini ameshindwa
na kukata rufaa kwa kulipeleka swala hilo kwa Mkuu wa Mkoa ili aweze
kuliingilia kati
Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu Philipo Mulugo alipo tafutwa kupitia simu
yake ye kiganjani yenye namba hii 0754315922 alijibu kuwa swala hilo bado
halijafika mezani kwake na endapo likifika basi atachukua hatua stahiki za
kinidhamu na kisheria dhidi ya Mkuu yoyote wa Chuo ambaye atakwamisha malengo
na ufanisi wa kazi nchini
Kutokana na hayo na mengine mengi ni dhahiri kuwa utendaji wa kazi katika chuo
cha Ualimu Songea kilichopo eneo la Matogoro Mkoani Ruvuma wilayani Songea ni
mgumu miongoni mwa Wafanyakazi na kusababisha hali ya sintofahamu katika
Saikolojia zao na mustakabali wa Elimu ya wanachuo
Ni vema sasa mamlaka zinazohusika zikachukua hatua stahiki za kumaliza mgogoro
huo ikiwemo na kumuondoa Mkuu huyo wa Chuo ili kurudisha Amani na Utulivu
chuoni hapo miongoni mwa wanajumuia wanaokizunguka chuo hicho ili kuweza
kufanikisha mikakati mbalimbali iliyopo nchini ya kuhakikisha kuwa elimu bora
inafikiwa nchini hapa
Mwandishi wa Makala hii anapatika kwa 0755-335051 AU 0715-335051
Barua pepe,stephano12mango@yahoo.com
www.stephanomango.blogspot.com