NA MWANDISHI WETU, SONGEA
NAIBU Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Mànyanya ameshauri kupanuliwa kwa bandari
ya Mbamba Bay iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma ili
kufungua milango ya uwekezaji katika ukanda wa kusini.
Mhandisi Manyanya ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nyasa, mkoani hapa alizungumza hayo katika kikao cha Bodi ya
Barabara Mkoa wa Ruvuma, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea
wiki iliyopita.
Naibu waziri huyo amesema
bandari ya Mbamba Bay ikipanuliwa itatumika na nchi tatu za Tanzania, Malawi na
Msumbiji hali ambayo itakuza uchumi na biashara hasa katika kipindi hiki cha
kuelekea Tanzania ya uchumi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako