Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts

March 22, 2018

WODI ZA KULALA WAGONJWA ZA ZAHANATI YA MTAKATIFU RAPHAEL KIJIJI CHA LUNDU

 

February 23, 2018

AFYA: WATANI ZETU WANA NACHINGWEA, SHIRIKINI KATIKA ZOEZI LA MATIBABU YA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA

February 19, 2018

HATUNA UWEZO HATA WA KUJENGA VYOO KWENYE ZAHANATI ZETU?

Zanahati ya kijiji cha Mbangamawe Kata ya Gumbiro wilyani Songea, imeshindwa kufanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili tangu ilipojengwa kutokana na kukosa huduma ya choo. Hali hiyo inawalazimu wakazi 1350 wa kijiji hicho kukosa huduma za afya tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho, hivyo wanalazimika kufuata huduma katika kijiji cha Ngadinda umbali wa kilomita 12.

Kufuatia tatizo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema, alifika katika kijiji hicho na kutoa mifuko 30 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa choo, ili kutoa nafasi kwa wakazi hao wapate huduma za matibabu.

©Nipashe, Feb.19/2017.

February 01, 2018

WATANZANIA MNAKARIBISHWA KWENYE ZOEZI LA KUTOA ELIMU NA UCHUNGUZI WA SARATANI ZA AINA MBALIMBALI

January 28, 2018

UTAFITI: SIGARA MOJA HUSABABISHA UGONJWA WA MOYO NA KIHARUSI

WATU watu wanaovuta Sigara angalau moja kwa siku wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa asilimia 50, huku wengine wakiwa na uwezekano wa kupata ugonjwa wa Kiharusi kwa asilimia 30 kuliko wale wasiovuta kabisa.
 
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya Chuo Kikuu cha London, umeonyesha kuwa hakuna kiwango cha usalama kati ya uvutaji wa sigara na kupata magonjwa tajwa. lakini umeeleza kuwa mtu anayeachana na uvutaji wa sigara hayupo katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo au Kiharusi.
Wamesema, asilimia 48 ya vijana wanaovuta sigara wanakabiliwa na magonjwa ya kuganda damu, kuharibu mapafu, pamoja na matatizo ya mishipa mwilini.  Magonjwa hayo yanayotokana na uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mtu yeyote kwani husababisha hata kifo.

January 12, 2018

BENKI YA DUNIA YATOA MSAADA WA KUBORESHA KITUO CHA AFYA MKILI

NA MWANDISHI WETU
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wametoa msaada wa shilingi milioni 400 kwa Kituo cha Afya cha Mkili kilichopo Kata ya Ngumbo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma bora za Afya kwa wananchi kwa ujumla.

December 27, 2017

MAMBO YA UFUKWE WA ZIWA NYASA. UTALII MZURI SANA

Honorius Mpangala

Honorius Mpangala, France Timbwili Mangova9katikati), na Herman Ndomba Kahokonyo

Honorius, Markus na Benedict Mpangala

NYASA; DISEMBA 20 ILIPONIREJESHA MIAKA 13 ILIYOPITA

NA HONORIUS MPANGALA, LUNDU
TULIANZA safari yetu na dadangu kijijini kwetu Lundu na kuelekea Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mbamba Bay. Changamoto za barabarani hazikukosa kwasababu ya mvua zinazonyesha. Tukifika na kukamilisha yaliyotupeleka huko. 

Saa kumi jioni nilipofika kituo cha mabasi cha Mbamba Bay sikukuta gari ya kugeuza kwenda kwetu Lundu. Ikatulazimu tupande ya kuishi njiani, gari iliyotoka Mbinga kwenda Kihagara. Nikiwa nawaza namna ya kutoka Kihagara hadi Lundu lakini nikapanga jambo kuwa bodaboda ziko kila eneo sikuhizi,na sikutoa nauli ya yangu na Dada nikamwambia waambie natoa Mimi. Nikamwambia konda natoa Kihagara kuna mtu anatusubiri,nilifanya Kwa maksudi.

December 07, 2017

CHANGIA DAMU YAOKOE MAISHA YA WATANZANIA WENZAKO

December 02, 2017

SOMO LA LEO: UKIMWI



"Wanaume na nyinyi muwe na maadili, wanaume wakubwa mnahisi labda wakubwa wenzenu wamechuja hawana ladha ile ambayo mngependa kuipata, kwa hiyo mnahamia kwa wototo wadogo, huu si mwendo mzuri, hawa ni watoto wetu, hili ni taifa la kesho," 

-Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza siku ya Maadhimisho ya Ukimwi Duniani.

December 01, 2017

MACHO VITABUNI


NAAM! Mara kadhaa ninapotembelea jiji la Dar es salaam wengi hutuita  wageni kama “watu wa mikoani”. Lakini ninachokiona wakati mwingine ni kuzikali fursa ikiwemo ya kutembelea maduka ya vitabu.

Wahenga wanasema ni heri ukatekwa nyara, kushikiliwa mateka kwa muda fulani katika duka la vitabu kwani unakuwa umehiari mwenyewe. Pia wanasisitiza kitabu ni silaha. 

November 30, 2017

UGONJWA WA KIPINDU PINDU UMEINGIA WILAYA YA NYASA

NA MWANDISHI WETU, MBAMBA BAY
 
UGONJWA wa Kipindupindu umebisha hodi kwa mara nyingine kama ilivyokuwa mwaka jana wilayani Nyasa, ambapo watu mbalimbali walikimbizwa hospitali kutokana na kuharisha na kutapika.
Wauguzi katika Zahanati ya mbamba Bay

Taarifa zinasema kuwa katika maeneo mengi wilayani Nyasa kwa sasa kuna ugonjwa hatari wa kipindupindu hususani vijiji vya Mwambao wa Ziwa Nyasa  upande kusini mwa wilaya hiyo kuanzia Kwambe hadi Liuli.
Taarifa hizo zinabainsha kuwa Kijiji cha Kwambe watu watatu (3) wamefariki dunia hadi kufikia siku ya Jumanne wiki hii. Mbali na hivyo, watu Ishirini (20) wamelazwa katika Zahanati ya Chiulu hadi sasa. 

November 24, 2017

JIWE LA POMONDA NA FORODHANI PANAWEZA KUTUPATIA WATU WA 'DIVING' KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI.

NA HONORIUS MPANGALA

LICHA ya kuwa mazingira mazuri na yenye kila aina ya vivutio lakini wafrika tunashindwa kuwa wabunifu wa katika kuyafanya kama fursa.Mungu aliiumba Afrika hivi ilivyo na kuweka jiografia ambayo nyakati zote watu Wa mataifa ya ulaya wamekuwa wakivutiwa nayo.
Mmmoja wa Warukaji katika Jiwe la Pomonda, Ziwa Nyasa
Iko michezo mingi inayochezwa Ulaya na Amerika inatokana na jinsi wenzetu walivyo makini katika kutumia mazingira yao katika kujipatia fursa ya maisha yao. Nyakati zote mataifa ya wazungu yamekuwa na michezo mingi ambayo ina mashabiki na wanafanya vyema,hakuna michezo ambao unakosa mashabiki Amerika na Ulaya.

November 13, 2017

KWANINI SEKRETARIETI YA AJIRA HAINA MATAWI NCHINI?

NA MARKUS MPANGALA
MIAKA kadhaa iliyopita nilishindwa kuwaelewa kabisa watendaji wa Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) hapa nchini. Nilikuwa siwaelewi kwa sababu siku moja niliwahushudia wafanyabiashara fulani kutoka Songea mkoani Ruvuma, wakizunguka vyumba vya ofisi vya taasisi hiyo kwenye jengo la Ushirika liliko Barabara ya Lumumba, Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kwa madhumuni ya kusajili kampuni yao.  
Jenista Mhagama

Pili,niliwahi kumsaidia rafiki yangu, Albert Nyaluke Sanga, ambaye ni mfanyabiashara mkubwa mkoani Iringa, ili apate leseni ya biashara. Haikuwa leseni yake binafsi, bali aliamua kumsaidia kijana mmoja aliyekuwa na ndoto za kuwa mfanyabiashara, lakini alikosa pa kunzia.
Rafiki yangu huyo anapenda kuwasaidia vijana wanaojishughulisha na ujasiriamali kwa sababu anaamini hiyo ndiyo njia pekee ya kuwakomboa, badala ya elimu yao na kuondokana na matembezi ya kusambaza bahasha za kuomba nafasi za kazi.

November 04, 2017

VITA YA KUGOMBANIA MAJI DUNIANI INAKUJA



NA MWANDISHI  WETU

SHIRIKA la Afya Duniani(WHO) linabainisha kuwa kuna watu bilioni 1.3 ambao ni moja ya tano ya watu wote duniani wanakosa maji safi na salama ya kunywa. Mwenyekiti wa Baraza la Maji Duniani Loic Fauchon anakiri hivi sasa hali ya upatikanaji wa maji duniani ni mbaya na kwamba watu wengi wanaweza kuangamia kwa kukosa maji safi na salama kutokana na uchafuzi wa vyanzo vya maji unaoendelea duniani kote.

TANZANIA YATAJWA KUONGOZA KWA MARADHI YA KIPINDUPINDU


NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Afya Duniani imeitaja Tanzania kuwa  miongoni mwa nchi kumi kinara kwa watu wake kuugua ugonjwa wa kipindupindu. Mataifa  mengine yaliyotajwa ni pamoja na India ambayo ndio inayoongoza. Nyingine ni Haiti, Jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya  Congo, Tanzania, Bangladesh, Uganda,  Msumbiji na Kenya, ambayo ilikumbwa na mlipuko mkubwa wa maradhi hayo kwa nyakati tofauti mwaka huu.

October 21, 2017

TABASAMU NA KITABU


Ragin Mmbanga (kushoto) na Markus Mpangala (Kulia)
Huyu ni rafiki yangu. Anaitwa Ragin Mbaga, ila tuwapo farashani hupendelea kumwita "Mzee wa bustani ya usomaji". 

October 17, 2017

MAONI YA MHARIRI: KWA WILAYA YA NYASA DUNIA HAIJABADILIKA?

Majuzi nimeona picha ya mwanadada mashuhuri katika mtandao wa Instagram, Mange Kimambi akionyesha majengo ya hospitali ya Lumeme wilayani Nyasa ikiwa na mazingira mabaya ya kufanyia kazi na ukosefu wa huduma muhumu. Pamoja na jengo lenyewe kutokamilika, lakini limekuwa likitumika hivyo hivyo.

Kwangu mimi ile ilikuwa habari kubwa sana kwa wilaya yetu ya Nyasa. Kama mwanahabari naamini kuripotiwa matukio au masuala yasiyofaa  ndani ya jamii ambayo haitoi habari za kutosha ni njia mojawapo kubwa ya kubadili mwenendo.

HAPA CHINI kuna Blogu ya JIMBO LA NYASA. Lakini habari za Jimbo husika ziliwekwa mara ya mwisho Januari mwaka huu. Nimejiuliza wasaidizi wa Mbunge wanafanya nini kama hawawezi kutoa taarifa za ofisi ya mbunge? Najiuliza hivi hatuoni umuhimu wa habari zetu zikiwa hadharani bila kujali mbaya au nzuri?

Je waanzilishi wa blogu ya JIMBO walikusudia tamasha au nini? BONYEZA HAPA KUTAZAMA.  Kimsingi habari za Jimbo la Nyasa ni lazima zitolewe wala kwa wananchi. Pili inadhihirisha "kuamini" kuwa NYASA ni ileile ambayo inaishi pasipo kuwa na habari zozote. Mtazamo huo si sahihi ndio maana wahusika wanaona "bora liende tu" huku wakisahau na kushindwa "KUMUUZA" mbunge. 

Nimejiuliza hadi leo hata kutengeneza ukurasa wa habari za mbunge kwenye mitandao hatuwezi kweli?  Hivi mahusiano ya mbunge na wapigakura wake yana maana gani? Naandika hapa kwasababu naamini wapo wahusika wanaofikisha ujumbe. Ningependa kuwakumbusheni kuwa "kutomuuza mbunge" katika ulimwengu wa kidigitali ni uzembe. Labda tunaweza kutembelea wananchi kila kona ya jimbo, lakini tunapawa kuelewa kuwa taarifa za huko ziwekwe sehemu maalumu kutunza kumbukumbu sio mambo ya "MASJALA" tena (hizo ni zama za kale mawe).

Kwa heshima nawakumbusha wasaidizi wa mbunge, kutoitendea haki blogu, kutozungumzia hata utalii ambao ni chachu ya kukuza mzunguko wa fedha wilayani kwetu ni UDHAIFU unaopaswa kurekebishwa.
Ninawatakieni majukumu mema. 
HABARI NI BIASHARA. HABARI NI UCHUMI.

MARKUS MPANGALA,
Oktoba 17/ 2017
Dar es salaam

UTAMU WA WIMBO WA TAIFA UKO KOMBE LA DUNIA.

NA. HONORIUS MPANGALA
 
ILIKUWA miaka Sita ya Ubabe wa soka barani Afrika kuanzia mwaka 2006 hadi 2012. Kila mpenzi wa soka alimfahamu Hassan Shehata,kila mpenzi wa soka alimfahamu Waile Gomaa. Ilikuwa nyakati za Misri kunyanyasa mataifa mengine ndani ya bara la Afrika. Ilimchukua Kameruni miaka tisa kulipiza manyanyaso aliyopata toka kwa Misri ya kiumeni mwaka 2008 pale Ghana.
Ni Misri ambayo iliipa hasara CAF kuunda kombe lingine la Afcon baada ya kulibeba lile awali Mara nne Mfululizo. Mwaka 2006 fainali zilizoandaliwa na Misri wakikutana na Ivory coast ya Didier Drogba.
KIKOSI CHA MISRI

Fainali ile iliisha kwa matuta na wenyeji kutwa taji. Licha ya kuwa na kikosi ambacho kilikuwa na vijana taklibani Saba wakitoka kikosi cha Al Ahly ambayo ilikuwa moto wa kuotea mbali. Hapa nawazungumzia Mohammed Barakat,Saeed Moward,Essam El Hadary,Ahmed Hassan,Hossam Hassan,Mohammad Mido,Mohammed Aboutrika na wengineo. Ilikuwa ni kikosi kilichojaa vipaji kikiwa na hamasa kubwa kutoka kwa kocha mzawa Hassan Shehata kiliwafanya wapinzani wafikirie Mara mbili zaidi.

October 09, 2017

RUVUMA: WANANCHI WAKERWA KUUZIWA KONDOMU

Wanawake wa kijiji cha Lumecha wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuweka ratiba ya kudumu ya utoaji huduma za uzazi wa mpango bure kwenye vijiji vya pembezoni ili kuwasaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi usio salama.

Wananchi hao wamekerwa na kitendo cha kutozwa fedha mbalimbali za vipimo ikiwamo kuuziwa mipira ya kiume, kuweka vipandikizi, kuchoma sindano na kupima watoto kliniki.