NA HONORIUS MPANGALA
LICHA
ya kuwa mazingira mazuri na yenye kila aina ya vivutio lakini wafrika
tunashindwa kuwa wabunifu wa katika kuyafanya kama fursa.Mungu aliiumba Afrika
hivi ilivyo na kuweka jiografia ambayo nyakati zote watu Wa mataifa ya ulaya
wamekuwa wakivutiwa nayo.
Mmmoja wa Warukaji katika Jiwe la Pomonda, Ziwa Nyasa |
Iko
michezo mingi inayochezwa Ulaya na Amerika inatokana na jinsi wenzetu walivyo
makini katika kutumia mazingira yao katika kujipatia fursa ya maisha yao.
Nyakati zote mataifa ya wazungu yamekuwa na michezo mingi ambayo ina mashabiki
na wanafanya vyema,hakuna michezo ambao unakosa mashabiki Amerika na Ulaya.
Ni
huko tunakoona viwanja vya michezo kama ya magongo, tennis, mountain bike,
vikiwa na mashabiki kedekede wakishuhudia michezo hiyo ambayo barani Afrika sio
rafiki sana. Iko
michezo ya kuruka toka juu katika milima,Minara,Madimbwi,Bahari na hata Ziwa.
Michezo ile imegawanyika katika nyanja tofauti katika umbali na maeneo ya
urukwaji.
Iko
mitindo kama ya urukaji wa kupatanisha mitindo 'Synchronized Diving' ambo umekuwa maarufu sana katika michuano
mbalimbali ya olimpiki. Mitindo huu warukaji huwa wawili wakiwa timu moja na
huruka Kwa kufanana mitindo ya urukaji na hauchukui umbali mrefu. Pia
kuna ule urukaji wa mitindo wa mbayuwayu ambayo huitwa 'Swallow Diving' hufanyika katika Kwa maeneo yenye umbali wa futi
15 hadi 30. Mrukaji hujitupa tuka eneo la kuanzia kama ni milimani au katika
mnara na kuruka kama dege aina ya mbayuwayu.
Urukaji
mwingine ni ule wa kwenye majabali,miteremko mikali iliyoko katika kingo za
bahari au ziwa ambao huitwa 'Cliff Diving'
mrukaji huachia Kwa umbali wa mita 26 hadi 28 . Aina hii ya urukaji
katika michezo hii ya kujirusha ndiyo huwafanya kupatikana warukaji wazuri
katika michuano mikubwa ya olimpiki.
CLIFF DIVING |
Mfano katika miaka ya 1928 kamati ya
olimpiki iliamua kuufanya urukaji wa mitindo ya 'Plain Diving' yaani urukaji wa maeneo ya uwanda wa pwani na
maeneo ya tambarare na ule wa 'Fancy
Diving' yaani urukaji wa kibunifu na kufirahisha hadhira uwe kitu kimoja.
PLAIN DIVING |
Michezo
hii imekuwa maarufu sana katika mataifa ya Ulaya na Amerika tofauti na Afrika.
Katika nchi ya Canada kuna shirikisho la kuendesha mashindano ya urukaji
kupitia Diving Plangeon Canada DPC. Shirikisho hilo limekuwa likiendesha
mashindano hayo mwezi Februari hadi Julai Kwa kuanzia katika majimbo hadi ngazi
ha taifa.
Katika
nchi yetu ya Tanzania licha ya kuwa na maeneo mazuri kijiografia lakini
tunakosa uwekezaji katika michezo tukihofia mwamko wa mashabiki kutokuwa na
mvuto nayo. Hakuna kitu kinachojianzisha chenyewe bali huanzishwa na uvumilivu
na kukubali chngamoto ni sehemu ya kufanikiwa.
Katika
miteremko mikali ya kitonga katika milima ya Udzungwa ungeweza kusema ndiyo
maeneo ambayo wazungu tunawaona wakijiadai nayo Kwa michezo hiyo ya kuruka
katika majabali ya milima ya Alps na Himalaya na kuifanya michezo ya ujirushaji
kuwa katika ngazi ya kutoa ajira Kwa wanachi wao. Kwa
kuanzia sisi kama Tanzania tungeweza kufanya uboreshwaji wa maeneo kama ya
Forodhani pale visiwani Zanzibar na Pomonda katika wilaya Nyasa katika
kuuhamasisha michezo wa urukaji wa mitindo wa 'Cliff Diving'.
Ni
michezo ambao warukaji huweza kuanzia mita chache na kumalizia katika mita
zilizoanishwa kwani watu huruka hadi umbali wa mita 26 hadi 28. Katika
eneo la jiwe Pomonda kuna taklibali urefu wa mita 30 na waogeleaji wengi
hupenda kuogelea toka nchi kavu hadi lilipo jiwe hilo bila ya kutumia kifaa
chochote na hatimaye kupumzika halafu baadae 'Cliff Diving' huanza hapo.
Inafurahisha kuwatazama warukaji wanaporuka. Sasa katika kuwapatia ajira hapo pangefanyiwa mkakati wa kutengeneza mashindano na mwisho kuwapa warukaji ambao wangeweza kuwakilisha nchi katika michuano mikubwa ya Olimpiki. Kama ilivuokuwa mwanzo mgumu katika kuupenyeza michezo ya urukaji katika Olimpiki ndivyo itakavyokuwa changamoto ya kutooukubalika haraka kutokana na uelewa wa watu.
Inafurahisha kuwatazama warukaji wanaporuka. Sasa katika kuwapatia ajira hapo pangefanyiwa mkakati wa kutengeneza mashindano na mwisho kuwapa warukaji ambao wangeweza kuwakilisha nchi katika michuano mikubwa ya Olimpiki. Kama ilivuokuwa mwanzo mgumu katika kuupenyeza michezo ya urukaji katika Olimpiki ndivyo itakavyokuwa changamoto ya kutooukubalika haraka kutokana na uelewa wa watu.
FANCY DIVING |
Eneo
la jiwe pomonda limaweza kufumika vyema na warukaji au wakazi wa mwambao wa ziwa Nyasa Kwa kufanya mshindano hata
nyakati za mapumziko ya mwaka kama ilivyo Kwa desemba ili kuweka chachu ya
kuvutia watu kwenda kupumzika katika fukwe za Liuli ambako jiwe hilo lipo.
Kila
tukionacho kwa wazungu basi tunapaswa kutambua kiliwekezwa na kikavutia
mashabiki baada waanzilishi kutokataa tamaa na kuweka malengo mbele.
Warukaji
maarufu wa miruko hiyo huchukuliwa kama watu ambao wejitoa ufahamu kutokana na
ugumu wa mazingira lakini sio hivyo kwani kujibiididsha na kuondoa woga ndo
mafanikio ya kuweza katika michezo ya ujirushaji. Hii haina utofauti na wale
wanajirusha katika majengo marefu ila kinachotofautisha ni maeneo ya kufanyia
tukio. Kwa
asili ya wakazi wa Nyasa kwao kuruka katika jiwe kama la Pomonda haiwezi kuwa
jambo la kuwafikirisha kwani ni michezo ambayo huifanya hata wakiwa wangali
wako katika umri mdogo kutokana na malezi ya kimakuzi.
Katika
maazimisho ya utalii yanyifanyika kila mwezi desemba mwishoni katika fukwe za
Nyasa zingeongeza michezo huu wa kujirusha kwani itaongeza hamasa kwa watalii
kutoka pande zote duniani kuja kucheza michezo hiyo hapa nchini. Kama
walivyo wao wakiona tu basi hujikuta wakihitaji kutoa mchango wao ili kuboresha
mashindano.
Mazingira
tunayo tunachohitaji ni wabunifu wa kuanzisha vitu kama hivi na kusaidia Kwa
kiasi kikubwa kuwaepusha vijana ambao wangeweza kuwa washirika na matukio ya
unywaji wa pombe au mengine yasiyofaa. Inahitajika mawazo mapya ambayo
yatafanya kuinua uwekezaji wa masuala ya utalii kwa ukanda wa kusini hususani
fukwe za ziwa Nyasa.
TUWASILIANE: 0628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako