Zanahati ya kijiji cha Mbangamawe Kata ya Gumbiro wilyani
Songea, imeshindwa kufanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili tangu ilipojengwa
kutokana na kukosa huduma ya choo. Hali hiyo inawalazimu wakazi 1350 wa kijiji
hicho kukosa huduma za afya tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho, hivyo
wanalazimika kufuata huduma katika kijiji cha Ngadinda umbali wa kilomita 12.
Kufuatia tatizo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet
Mgema, alifika katika kijiji hicho na kutoa mifuko 30 ya saruji kwaajili ya
ujenzi wa choo, ili kutoa nafasi kwa wakazi hao wapate huduma za matibabu.
©Nipashe, Feb.19/2017.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako