NA THOMAS CHIHONGAKI
Majonzi na Simanzi Vimetawala katika
Kijiji cha Lundo na Ngindo Kata ya Lipingo kutokana na tukio la dada yetu Neema
Kalanje(25) kupoteza maisha kwa kushikwa na kuuliwa katika Mto Lwika uliopo Kijiji
cha Lundo.
Dada yetu amekutwa na umauti
huo jana Saa 5 Asubuhi akiwa katika shughuli zake za ujasiriamali wa kuuza
Dagaa Nyasa aliowanunua Ziwani Asubuhi na kwenda kuwauza katika Kitongoji cha
Zambia katika Kijiji cha Ngindo.
Marehemu alipofika katika Kivuko
cha Mto Lwika kuna dalaja dogo la Mbao akaamua kunawa Maji ghafla mamba
akatokea na Kumkamata. Baadae Taarifa zilisambaa kijijini kwa mayowe na hatimaye Wananchi wakakusanyika
na kuanza kutafuta na kufanikiwa kuuona mwili wa Marehemu.
Eneo hilo ni hatari kwani mwaka
2015 palitokea ajali na kujeruhiwa kwa kijana Ignas Magic Kalenyula na kumuua
Thomas Nkoma. Rai yangu kwa Halmashauri kupitia Idara ya Maliasili kuangalia uwezekano
wa kuwasaka wanyama hao na kuwatokomeza kabisa.
Pia Idara ya Ujenzi Nyasa kutusaidia
kujenga daraja la kudumu katika eneo hilo. Picha za tukio nii kwa hisani ya C.Ngwata
Diwani wa Kata ya Lipingo (Chadema). Natoa pole zangu kwa Familia ya akina
Kalanje na Mdogo wangu Elisha Magunga kwa kumpoteza Mke wake Mpendwa...
RIP Neema
No comments:
Post a Comment
Maoni yako