WATU watu wanaovuta Sigara
angalau moja kwa siku wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa
asilimia 50, huku wengine wakiwa na uwezekano wa kupata ugonjwa wa Kiharusi kwa
asilimia 30 kuliko wale wasiovuta kabisa.
Wamesema, asilimia 48 ya vijana
wanaovuta sigara wanakabiliwa na magonjwa ya kuganda damu, kuharibu mapafu,
pamoja na matatizo ya mishipa mwilini. Magonjwa
hayo yanayotokana na uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mtu yeyote kwani
husababisha hata kifo.
Utafiti huo umeongeza kuwa asilimia
kubwa ya watu wazima nchini Uingereza wanaovuta sigara imepungua, lakini idadi
ya watu wanaovuta sigara moja hadi tano kwa siku imeongezeka.
Uchambuzi wa utafiti wa taasisi
hiyo uliochapishwa baada ya kuwachunguza watu 141, unaonyesha tabia ya uvutaji
wa sigara kwa siku 20 inasababisha watu saba kuugua ugonjwa wa moyo au kiharusi
katika kundi la watu 100 wenye umri wa kati. Lakini iwapo wataachana na
uvutaji wa sigara kwa siku moja unaweza kusababisha watu watatu pekee kuugua
magonjwa hayo.
Watafiti wamesema wanaume wanaovuta
sigara moja kwa siku wana uwezekano wa asilimia 48 kutengeneza dalili za
ugonjwa wa moyo na asilimia 25 ya ugonjwa wa kiharusi. Kwa upande wana wanawake,
watafiti wamesema ni asilimia 57 ya wanaovuta sigara wapo kwenye hatari ya
kuugua ugonjwa wa moyo na asilimia 8=31 wataugua ugonjwa wa kiharusi.
Profesa Allan Hackshaw wa
Taasisi ya Saratani ya Chuo Kikuu cha London ambaye aliongoza timu ya utafiti,
aliliambia Shirika la habari la BBC, “Utafiti unaonyesha zipo nchi chache zenye
kupunguza kiwango kikubwa cha uvutaji wa sigara, hilo ni jambo zuri, ambalo linaweza
kuzuia magonjwa kama Saratani. Lakini upo uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa
hayo mawili (Moyo na kiharusi) kuliko saratani. Wanapaswa kuacha uvutaji wa
sigara,”
Watafiti hao wamesema kuwa wana
matarajio makubwa kuona idadi ya wavutaji wa sigara ikipungua ili kuepusha
magonjwa, kwani pia hata takwimu zao zinaonyesha kuwa ugonjwa saratani ya mapafu
unachangiwa na uvutaji wa sigara.
Hata hivyo wamebaini kuwa
wanaume wanaovuta sigara moja kwa siku wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa
moyo kwa asilimia 46 na asilimia 41 ya ugonjwa wa kiharusi kwa wavutaji wa
sigara 20 kwa siku.
Ni asilimia 31 ya wanawake wanaovuta
sigara moja kwa siku wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na asilimia
34 ugonjwa wa kiharusi.
Profesa Hackshaw amesema hatari
ya magonjwa hayo inatokana na muda mrefu wa kuishi, lakini upo uwezekano wa
kuyapata iwapo mtu atavuta sigara kwa miaka michache tu.
Amesema habari njema ni kwamba
wote wanaoacha kuvuta sigara wana uwezekano wa kupunguza hatari ya kupata
magonjwa nyemelezi.
CHANZO; TOVUTI YA BBC. IMETAFSIRIWA NA MARKUS MPANGALA
No comments:
Post a Comment
Maoni yako