Wakazi
wa Wilaya mpya ya Nyasa wameiomba serikali kuanzisha kambi za Jeshi la Wananchi
nchini katika makao makuu ya wilaya hiyo, Mbamba Bay ili kukabiliana na hali
mbaya inayoweza kujitokeza hapo baadaye.
Wakizungumza
katika kongamano la Usalama wa raia, wakazi wa Wilaya ya Nyasa, wameiomba
serikali kuangalia uwezekano huo ili
kuimarisha ulinzi wa mji wa Mbamba Bay ambao ni lango kuu la kuingilia
kwa upande wa Tanzania kutokea kusini.
Wamesema
kuwa ingawa serikali imepiga hatua katika mazungumzo yake na serikali ya
Malawi, bado wakazi wa wilaya hiyo mpya wanaishi kwa hofu na wasiwasi mkubwa.
“Sisi
wakazi wa mpakani hasa hapa Nyasa tunaishi kwa wasiwasi, tunaomba Jeshi la
Ulinzi lije kuweka kambi maalumu hapa, tunafahamu wapo polisi, lakini wenyewe
hawatoshi kwani tunahitaji ulinzi zaidi,” alisema mkazi mmoja wa Mbamba Bay
Kaika
hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa wilaya Nyasa wamebainisha maoni yao kuwa ni
vema Katiba Mpya itakayopatikana hapo baadaye baada ya kuidhinishwa na Bunge la
Katiba, itamke waziwazi mipoaka ya nchi yetu.
Wakazi
hao wanasema kuwa pamoja na uhuru walionao kuingia nchi za Msumbiji au Malawi bado kunahitajika uwazi zaidi na
Katiba ya nchi yetu inalazimika kutaja mipaka ya nchi yetu ili kulinda mipaka
na kuwa mwongozo wake.
Wamesema
Katiba inatakiwa kuchukua nyaraka zote za mipaka na kubainisha mipakaya ndani
ya nchi, na nje ambako tunapakana na nchi mbalimbali.
Wakitolea
mifano Namanga, Sirari, Kasumulu, Tunduma, Mbamba Bay na mingine mkoani Kagera. Aidha,
walisema kuwa ni lazima Katiba itamke kuwepo kwa Vituo vya kudumu vya Polisi
katika vijiji vyote katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
NB: maoni ya wakazi wa vijiji vya
Tingi, Kingirikiti, Chiwanda, Kilosa, Mtipwili, Peramiho, na Mbamba Bay
No comments:
Post a Comment
Maoni yako