NA MWANDISHI WETU, MBAMBA BAY
UGONJWA wa Kipindupindu
umebisha hodi kwa mara nyingine kama ilivyokuwa mwaka jana wilayani Nyasa,
ambapo watu mbalimbali walikimbizwa hospitali kutokana na kuharisha na
kutapika.
Wauguzi katika Zahanati ya mbamba Bay |
Taarifa zinasema kuwa katika
maeneo mengi wilayani Nyasa kwa sasa kuna ugonjwa hatari wa kipindupindu
hususani vijiji vya Mwambao wa Ziwa Nyasa upande kusini mwa wilaya hiyo kuanzia Kwambe hadi
Liuli.
Taarifa hizo zinabainsha kuwa Kijiji
cha Kwambe watu watatu (3) wamefariki dunia hadi kufikia siku ya Jumanne wiki
hii. Mbali na hivyo, watu Ishirini (20) wamelazwa katika Zahanati ya Chiulu
hadi sasa.
AIdha, ugonjwa huo umeshika kasi pia katika Kijiji cha Lundo, kilichoko Kata ya Lipingo, pamoja na Chinula na maeneo mengineyo. Kata ya Lipingo inatajwa kuwa hali mbaya zaidi kwani hadi jnaa Jumanne jioni watu 6 wamefariki, hali ambayo imechochea kuongezwa wataalamu katika Zahanati ya Lundo, pamoja na vifaa vya tiba na magodoro ili kuongeza tija kwani kituo cha Afya cha Makwai kilichopo katika kijiji cha Lundo kimelemewa. Maeneo mengineyo nayo wagonjwa wamelazwa katika Hospitali ya Liuli.

ANGALIZO:
Tuweke mazingira yetu safi, Tusile
vyakula vya baridi (vimbala na michuzi ya maji na chumvi), tuache unywaji pombe
Kiholela hususani za Kienyeji (komoni na wanzuki - Viporomba). Matumizi mazuri
ya vyoo, kunawa kila utokapo chooni, kuosha maembe kabla ya kula, pia kunywa
maji safi na salama yaliyochemshwa.
MATIBABU : Ukiona dalili za
kuhara mfululizo au kutapika Basi wahi mapema Kituo cha Afya kilichoko jirani
nawe.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako