Na.
HONORIUS MPANGALA
Nilikuwa
nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo April 4, 2015 siku ya pasaka. Kulikuwa
na mchezo wa wa mtoano kuelekea kwenye makundi klabu bingwa Afrika kati ya Tp
Mazembe wenyeji dhidi ya Orlando Pirates. Mitaani kila uliyemwona alikuwa
amevalia jezi ya Mazembe na akizungumza kuhusu Mazembe huku wakielekea uwanjani
Estadio de Mazembe.
Nilimuuliza
mlinzi wa eneo nilioenda kuhusu mashabiki FC Lupopo hawawezi kwenda uwanjani?
Akanijibu hata Mimi ni Lupopo lakini inapokuja uwakilishi wote tunakuwa wamoja.
Akanieleza hata uwanjani huioni jezi ya Lupopo. Mechi ile ilimalizika kwa TP
kupata matokeo ya goli tatu kwa moja yaliyofungwa na Ranford Kalaba,Mbwana
Samata na Rogers Asale.
SIMBA |
Nilikaa
na mlinzi yule tukisikiliza matangazo ya redio kwa lugha ya kifaransa naye
alinitafsiria kwa kiswahili cha kikongo. Wakati magoli yote yanaingia katika
lango la Orlando alikuwa akisimama na kushangilia. Huo ndio utofauti wetu na
wao inapokuja suala la michuano ya kimataifa.
Sababu
ya pili ambayo inapelekea timu zetu za kitanzania kuwa na wakati mgumu ni kwa
upande wa wachezaji. Upande Huu unatokana na ile hali ambayo wachezaji
wanaichukulia katika mchezo. Huweza kuingia uwanjani wakiwa wamejiamini sana
lakini ni kelele za dakika chache toka kwa mashabiki wanao wafahamu zitawafanya
wachanganyikiwe.
Maisha
ya wachezaji wa kitanzania yako kawaida sio jambo geni kumwona mchezaji yuko
mtaani akiwa amekaa na jamaa zake ambao ni marafiki. Sasa ikitokea marafiki
wako uwanjani wanamtazama jamaa yao ,itatokea mchezaji hata taka kukosea
achezapo. Lakini kama zitasikika sauti toka kwa anaowafahamu itazidi
kumchanganya na kumfanya apotee kabisa katika mchezo.
Simon
Msuva baada kurejea katika timu ya taifa alikiri ameshangazwa na ushangiliaji
wa mashabiki wa Morocco. Akasema wana ushangiliaji tofauti kulingana na hali ya
mchezo.
Kama
wanataka kusawazisha bao watakuwa na aina yao ya kushangilia au kama watahitaji
matokeo watakuwa na ushangiliaji wao na hata kama timu inaongoza kwa magoli na
muda unayoyoma wataimba na kushangilia kwa aina yake kama kuwatia hamasa ya
kutopoteza mchezo.
Hili
lilimshangaza sana kwani alizoea kutazama hapa Nyumbani kama Yanga ikicheza na
Mbeya City basi mashabiki wa Simba watakuwa Mbeya City na kama watakuwa
wanacheza nchini ya kiwango wataishia kuzomewa sana. Yeye ni mwathirika wa
kuzomewa na mashabiki wake wakati anachezea Yanga ndio maana alilishangaa hili
huko Morocco.
Mara
kadhaa baada ya Yanga kucheza hatua ya makundi katika michuano ya shirikisho
mwaka 2016 walikiwa na malalamiko kuwa TFF haiwasaidii katika michuano ya
kimataifa. Hili limefanya kuwashangaza hata klabu ya Simba kule Misri walipoona
ushiriki wa viongozo wa chama cha Soka cha Misri wakati wanaenda kupambana na
wapinzani wao wa El Masry.
Msimu
wa uliopita wakati Yanga walipangwa na Zanaco ilikuwa kama wangeitoa klabu hiyo
ya Zambia. Ingefanya idadi ya uwakilishi kwa msimu huu iongezeke moja baada ya
kuonekana maendeleo mazuri ya klabu hiyo kwani wangeingia katika makundi misimu
miwili mfululizo katika mashindano mawili yaani michuano ya shirikisho na ile
ya shirikisho.
YANGA |
Nadir
Haroub Ally 'Cannavaro' alipohojiwa baada ya mchezo dhidi ya Township Rollers
alisema hizi mechi zinawahitaji kutumia vyema uwanja wa nyumbani. Timu
inahitajika kupata matokeo mazuri ikiwa nyumbani kwani kutegemea ugenini ni
kitu ambacho ni kigumu sana.
Wakiwa
Angola mwaka 2016 walikutana na manyanyaso ya akili toka kwa watu wa ulinzi na
usalama nchini Angola. Na nyakati zote ukiona mambo yasiyokuwa ya kimchezo
yakafanyika basi ujue hata wasimamizi wa mchezo husika ni kama wanakuwa
wamepangwa kuto toa ripoti itakayo waingiza matatani.
Wenyeji
wa Yanga baada ya kufungwa magoli mawili Tanzania wakafanikiwa kupata ushindi
wa goli moja wakiwa Angola. Lakini matukio ya ndani mchezo yalisababisha kupatikana
kwa penati ambayo haikutarajiwa kulingana na mzingira yake. Lakini bahati ikawa
kwao golikipa aliipangua.
Kabla ya kupigwa penati hiyo wachezaji wa Yanga
walimzonga mwamuzi hali iliyopelekea Askari kuingia na virungu uwanja na kutaka
kutumia nguvu kutuliza ile hali.
Sasa
Cannavaro anaposema huko ugenini kuna changamoto basi tumwelewe katika
mazingira hayo. Watanzani hatujawa watu wa mipango mipango ili kufanikisha timu
zetu kupata matokea katika michuano ya kimataifa. Hali hii imekuwa tofauti
tunapoenda ugenini.
Moja
vitu ambavyo Ismail Aden Rage hataki kuvikumbuka ni marudiano ya mchezo kati DC
Motema Pembe ya DRC na Simba ya Tanzania. Mchezo ambao ulimfanya asitamani
kwenda tena katika jiji la Kinshasa kwa Yale manyanyaso ya akili na mwili
waliyokutana nayo.
Ni
katika mechi hii ambapo mwandishi mmoja wa kike kutoka Tanzania alifanyiwa
vitendo vya unyanyasaji na mashabiki wa DC Motema Pembe. Licha ya uwepo wa watu
wa usalama lakini mwandishi yule alichokutana nacho alipofuatwa na mashabiki
hao anajua yeye na Mungu wake.
Wakongo
wa klabu hiyo waliamini kuwa wapinzani wao katika soka la Kongo klabu ya AS
Vita wamewapa 'dumba' Simba ili wawafunge, sasa janga likamkuta mwandshi yule
akiwa ameenda kujisaidia. Inasikitisha.
Kama
hatutaki kuamini kuwa mchawi namba moja ni sisi wenyewe katika kuendekeza mambo
ya kipuuzi timu zinapokuwa zinawakilisha nchi basi tukubali kuumia milele. Kama
pia viongozi hawatatambua na kutoa elimu kwa mashabiki kuwa michuano ya
kimataifa ndiyo inayoweza kutuongezea idadi ya timu kushiriki basi tumsubili
yesu kuja kutujuza.
Kama
tutashindwa kutambua umuhimu wa kuto waingiza wachezaji wetu matatani wawapo
katika kuwajibika. Basi tumsuli mtume aje kutushika msikio na kutuambia wapi
tunakosea. Maana katika mtazamo wa kawaida tunashindwa kutambua umuhimu wa
vipaumbele vya soka letu ili liweze kujualikana kimataifa na hatimaye kuja kuwa
kitalu kizuri cha kuuza wachezaji.
0628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako