NAAM! Mara kadhaa
ninapotembelea jiji la Dar es salaam wengi hutuita wageni kama “watu wa mikoani”. Lakini
ninachokiona wakati mwingine ni kuzikali fursa ikiwemo ya kutembelea maduka
ya vitabu.
Wahenga wanasema ni heri
ukatekwa nyara, kushikiliwa mateka kwa muda fulani katika duka la vitabu kwani
unakuwa umehiari mwenyewe. Pia wanasisitiza kitabu ni silaha.
Siku hii nilitembelea Duka la
Vitabu la TPH (TPH Bookshop) lililopo maeneo ya Samora, jijini Dar es salaam. Nilitumia
dakika 45 kusaka vitabu mbalimbali. Waungwana nawaomba someni kwa furaha!
Katika ziara yangu nilivutiwa
na kitabu cha Historia ya Wahadzabe. Nimekipenda, napenda kusoma vitu
vinavyohusu Afrika na kama vinavyohusu dunia ujue ni vya sport. Mojawapo ni
kitabu cha mwandishi Michael Dean kiitwacho “World Cup”, nilikisoma kwa masaa
machache sana, sasa nimeweka kiporo kusoma Autobiography ya Geoff Hurst pale nyumbani. Nafikiri nilipokiona kile cha “Mbali
na Nyumbani” nilitamani mno, nikaja kuachwa hoi na kile “WHY MEN LOVES BITCHIES”
nilichoka looooh!
Ndiyo uhondo wa vitabu.
Wasalaamu watu wangu
Honorius Mpangala,
Kigoma, Tanzania
No comments:
Post a Comment
Maoni yako