NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Afya Duniani(WHO) linabainisha kuwa kuna watu
bilioni 1.3 ambao ni moja ya tano ya watu wote duniani wanakosa maji safi na
salama ya kunywa. Mwenyekiti wa Baraza la Maji Duniani Loic Fauchon anakiri
hivi sasa hali ya upatikanaji wa maji duniani ni mbaya na kwamba watu wengi
wanaweza kuangamia kwa kukosa maji safi na salama kutokana na uchafuzi wa
vyanzo vya maji unaoendelea duniani kote.
"Leo tunajadili suala la maji ambalo linawatia watu
wasiwasi, na linaweza kusababisha migogoro na vita vya kugombania maji vya
Dunia. Hivi sasa rasilimali ya maji ipo hatarini kutoweka,binadamu wanakabiliwa
na uhaba mkubwa wa maji'',anasema Fauchon.
Kwa mujibu wa WHO,Watu waliokufa mwaka 2014 kutokana na
uchafuzi wa maji, ni mara 10 ya waliokufa kutokana na vita. Nchi ya Somalia inakabiliwa na ukame wa kutisha ambapo watu
milioni sita kati ya milioni kumi wapo katika vita ya kugombania maji na
chakula baada ya vyanzo vingi vya maji kukauka na kusababisha njaa katika
maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Matumizi ya maji duniani yameongezeka mara sita zaidi kati
ya mwaka1900 na 1995 zaidi ya mara mbili ya kiwango cha ongezeko la watu na
huendelea kukua kadri kilimo viwanda na matumizi ya nyumbani yanavyoongezeka.
Kilimo hutumia takribani asilimia 70 ya matumizi yote ya maji duniani.
Ripoti ya Water Aid ina inazitaja nchi ambazo zina hali
mbaya zaidi katika huduma ya maji kuwa ni Papua New Guine, Msumbiji ,
Madagascar na Angola ambayo inangoza ikiwa na asilimia 71 ya wananchi wake wa vijijini
wakikosa maji safi na salama.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako