NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Afya Duniani imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi kumi kinara kwa watu wake
kuugua ugonjwa wa kipindupindu. Mataifa mengine
yaliyotajwa ni pamoja na India ambayo ndio inayoongoza. Nyingine ni Haiti,
Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo, Tanzania, Bangladesh,
Uganda, Msumbiji na Kenya, ambayo
ilikumbwa na mlipuko mkubwa wa maradhi hayo kwa nyakati tofauti mwaka huu.
Katika ripoti yao iliyotolewa hivi majuzi, imesema kuwa sababu
kuu ya kuandamwa na maradhi hayo ni kukithiri kwa mazingira machafu katika
mataifa hayo.
Ripoti hiyo inasema kuwa watu bilioni 1.2 sawa na moja ya
sita ya watu wote duniani wako hatarini kukumbana na maradhi hayo hatari.Wakati Bara la Afrika likikumbwa na kadhia hiyo kutokana na
unywaji wa maji yasiyofaa, hali ni tofauti kwa
Ulaya na Amerika ya Kaskazini ambako mifumo imara ya maji taka
imeyafanya mabara hayo yawe huru na kipindipindu kwa miongo mingi sasa. Lakini watu zaidi ya bilioni mbili wamebakia bila maji safi
na mifumo ya maji taka.
Hivyo, kipindi pindu kinaendelea bila huruma kuathiri watu
masikini zaidi duniani na ndani ya kila nchi athirika. Kwa sababu hiyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limeunda
Kikosi Kazi cha Kudhibiti Kipindupindu Duniani (GTFCC), ambacho kinazileta
pamoja taasisi zaidi ya 50.
Lengo la GTFCC ni kuongeza juhudi za kuimarisha ushirikiano
wa kupunguza vifo kutokana na maradhi hayo kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2030. WHO limeeleza matumaini yake ya kupunguza kwa kiasi kikubwa
maambukizi ya ugonjwa huo na idadi ya vifo vitokanavyo ifikapo kipindi hicho.
Mkurugenzi anayehusika
na masuala ya dharura katika shirika
hilo, Dk. Peter Salama alipokuwa akizungumza na
waandishi habari mjini Geneva, Uswisi hivi karibuni, alisema
shirika hilo lingeweza kuchukua hatua
za haraka na
kutuma chanjo zaidi
ili kupambana na ongezeko
kubwa la maambukizi
ya ugonjwa wa kipundupindu nchini Yemen
mwaka huu.
Lakini pia ameeleza matumaini yake kwamba, ‘tunakaribia kufikia lengo,’ kuhusiana na ugonjwa huo
unaoweza kuzuilika, ambao
umefikisha maambukizi ya watu
700,000 na kusababisha
zaidi ya vifo vya
watu 2,000 mwaka huu.
Lengo ni moja kati ya malengo makubwa ya WHO kuutokomeza
kabisa ugonjwa huo ama kuupunguza
kwa kiasi kikubwa.Juhudi kama hizo tayari
zinafanywa dhidi ya ugonjwa
wa kupooza, malaria, surua, na Ukimwi.
Hivi sasa, ugonjwa wa
tete kuwanga ni pekee unaoelezwa umekwisha tokomezwa katika uso wa dunia na hivyo kubakia katika vitabu vya
historia.
India na nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara
Afrika zinakabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya kupambana na
kipindupindu.
Maeneo kama Yemen inayokabiliwa na vita, ama Bangladesh,
ambayo iliwapokea zaidi ya wakimbizi 500,000 Waislamu wa Rohingya kutoka Myanmar, inakabiliwa na
hali ambayo haitabiriki kwa urahisi.Kwa sababu hiyo, mpango
huo wa kimataifa unalenga katika
kupambana na maeneo yanakozuka mlipuko wa ugonjwa huo kila mara, ambako kila mwaka
katika wakati ule ule, ugonjwa huo hutokea.
Mpango huo unalenga
kuboresha usafi wa maji na mifumo ya maji safi na maji taka
pamoja na kutumia chanjo za kunywa. Mkakati huo
unaweza kusaidia kutokometa
kipindupindu katika mataifa 20
yaliyoathirika ifikapo mwaka 2030, kwa
mujibu wa WHO.
Hata hivyo, Shirika la WaterAid limeitaja nchi ya India kuwa imeathirika kwa kiasi kikubwa ikiwa na
zaidi ya kesi za
maambukizi 675,000 kila mwaka.
Pia ina idadi kubwa
ya watu wanaoishi
bila ya kuwa na uwezo
wa kupata maji safi na
salama na wengi wanaishi bila
kuwa na vyoo sahihi.
Maeneo ya mijini yakiwa na maji machafu, ambayo yanaweza
kuingia katika vyanzo vya maji na kusababisha magonjwa nchini Msumbiji,
Ethiopia na Nigeria,
ambazo zinafuatia katika nafasi ya pili na tatu pia zina
idadi ya juu ya pili na ya tatu ya
watu wanaoishi bila
maji safi.
Miongoni mwa waathirika walikuwa askari polisi zaidi ya 30,
ambao walijikuta wakilazwa hospitali baada ya kula kile kinachodaiwa chakula
xchenye mambukizo katika moja ya migahawa ya jeshi hilo
No comments:
Post a Comment
Maoni yako