NA MWANDISHI WETU, SONGEA
Afisa Kilimo wa Manispaa ya
Songea Mushoborozi Christian amesema Halmashauri hiyo imepokea barua toka NFRA
inayotoa maelekezo ya ununuzi wa mahindi katika awamu ya tatu msimu wa mwaka
2017/2018.
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma imepangiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA)
katika msimu huu kununua mahindi tani 400.
Picha kwa Hisani ya Manispaa ya Songea. |
Amesema katika Manispaa ya
Songea Kata saba tu kati ya Kata 21 zinaruhusiwa kununua mahindi katika kituo
cha NFRA ambapo wananchi wanatakiwa kupeleka mahindi kwa ajili ya kuuza.
Mushoborozi anazitaja Kata
ambazo zinahusika katika ununuzi wa mazao hayo kuwa ni Lilambo ambayo
imepangiwa kununua tani 100,Subira 100,Mjimwema 40,Ruhuwiko 60,Mshangano 40,
Matogoro 30 na Ndilimalitembo tani 30 hivyo kufanya jumla ya tani 400.
Hata hivyo Mtaalam huyo wa
kilimo amewaasa wananchi wote wanauza mazao hayo,kuhakikisha mahindi
wanayopeleka kuuza yasiwe na uchafu ili kuondoa usumbufu na kwamba wananchi
wanatakiwa kuuza mahindi kulingana na mgawo wa ununuzi kwa kila Kata husika.
“Kumekuwepo na tabia ya baadhi
ya Kata kutofikia malengo ya serikali ya kuuza mahindi NFRA,katika awamu hii
Afisa Mtendaji wa Kata atakayeshindwa kuhamasisha wakulima kuuza mahindi NFRA
atawajibishwa’’,anasisitiza Afisa Kilimo huyo.
Kulingana na Mtaalamu
huyo,Mkulima anaruhusiwa kuuza tani moja tu ya mahindi NFRA na kwamba bei ya
kilo moja ni shilingi 500 na kwamba zoezi la kupeleka mahindi NFRA linatakiwa
kukamilika Novemba 17.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako