KWA muda mrefu Wilaya ya Nyasa haikuwa na Shule ya sekondari yenye kidato cha tano na Sita. Wanafunzi na wazazi walilazimika kutumia gharama zao kutafuta shule za sekondari binafsi nje ya Wilaya hiyo. Kma inavyofahamika Wilaya ya Nyasa bado ni changa, hivyo inakabiliwa na changamoto ya shule za sekondari binafsi, kutokana na watu kutowekeza kwa kiwango cha juu.
Kutokana na hali hiyo sasa Ujenzi wa Shule ya sekondari ya Kidato cha tano na sita unaendelea mjini Mbamba Bay. Ni mojawapo ya hatua za nzuri za maendeleo. Shule hiyo ni ile iliyopo katika kijiji cha Ndengele kilichopo katika Kata ya Mbamba Bay.
Ujenzi unaendelea, shule hiyo itakuwa na jengo la ghorofa moja.
Baadhi ya majngo ya shule hiyo.
Mandhari ya shule hiyo.
Ujenzi unaendelea katika shule hiyo kuonmgeza madarasa kwa mtindo wa ghorofa ili kuwezesha kuchukua wanafunzi wengi kulingana na mahitaji na kupatiwa elimu.
PICHA ZOTE; VITUS MATEMBO.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako