September 16, 2017

MIAKA 33, YANGA KASHINDA MARA MOJA UWANJA WA MAJIMAJI.

Na. Honorius Mpangala.
Labda kama ulikuwa hujui mpenzi wa soka la Tanzania. Toka mwaka 1984 hadi sasa mwaka 2017 klabu ya Yanga imepata ushindi katika uwanja wa Majimaji Mara 1 . Ni kaseke aliyeifunga Majimaji msimu uliopita goli moj.

Tangu zama za wachezaji waliopita klabu hiyo kama kina SHAIBU KAMBAGA,MBOPA LUOGA(NAHODHA) ,SELESTINE SIKINDE MBUNGA,MADARAKA SELEMANI,FRED MBUNA,ABDALLAH KIBADENI,PETER TINO, STEVEN MAPUNDA,ODO NOMBO,JUMA MPOLA (ZIZOU) na wengine wengi. Majimaji imefungwa Mara Moja.

Nyakati zote kwa miaka hiyo yanga aliambulia kipigo au sare ya magoli au isiyo ya magoli. Historia iko na inavunjwa pia lakini lazima vijana waendeleze kuweka ngumu kwasababu hatutaki mazoea.
                                                Bendera ya timu ya Majimaji



 
Kikosi cha Timu ya Majimaji ya Mjini Songea mkoani Ruvuma ambacho leo kitapepetana na bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ya Dar es salaam.

KIKOSI CHA MAJIAMJI

1.Andrew Ntara
2.Tuma Salamba
3.Mpoki Mwakinyuke
4.Kennedy Kipepe
5.Tumba Lui Sued
6.Paulo Maona (maestro)
7.Seleman Kassim Selembe
8.Hassan Hamis
9.Macrel Bonaventure
10.Jeryson Tegete
11.Danny Mrwanda ( nahodha)
AKIBA;  Nina,Humud,Aziz Sibo,Yakubu Kibiga,Peter Mapunda,Lucas Kikoti,Hashim Mussa,Six Mwasekaga.

Wachezaji wa Majimaji wakifanya mazoezi

No comments:

Post a Comment

Maoni yako