Ni raia wa Afrika Kusini akiwa katika sehemu ya viunga vya
jiji la Johannesburg. Huwa anasoma vitabu na kuueleza umma maudhui na
mafundisho yaliyomo kitabuni, wapitao na kusikiliza humchangia fedha kadiri ya
ridhaa ya mchangiaji.
Ukimuadhima kitabu anasema ni bora akuuzie kwani yeye
ameshasoma hivyo anapenda ununue na ukakisome kwa uhuru zaidi kuliko kuwa na
mashaka ya muda wa kurudisha. Hivyo ndivyo apatavyo ridhiki.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako