Serikali ya Kenya imepiga marufuku kusafiri nje ya nchi
bila idhini maafisa wake. Kupitia taarifa rasmi kwa maafisa wa serikali ambayo
TUKO.co.ke imesoma, Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua alisema Mawaziri,
Makatibu wa Wizara, Maafisa katika Wizara, Wakuu wa Mashirika na maafisa wao
hawaruhusiwi kusafiri nje ya nchio bila ya idhini kutoka kwa Rais.
Nakala za barua hiyo zimetumwa katika wizara muhimu
zinazohusika na uhamiaji ikiwa ni Wizara ya Ndani na Ushirikishi wa Serikali ya
Kitaifa na Wizara ya Mambo ya Nje. ''Hii ni kufahamisha kuwa, imekubaliwa
kwa,mba, hadi kuamliwa vinginevyo, hamna Afisa wa Serikali atasafiri nje ya
nchi bila ya kibali kutoka kwa Rais. Ili kuondoa, maafisa hao ni pamoja na
Mawaziri, Makatibu wa Wizara na Maafisa kutoka Wizara, Maafisa Wakuu wa
Mashirika na Maafisa wao, na Wakurugenzi wa Mashirika ya Serikali." Barua
hiyo ya Jumatano, Septemba 13 2017, ilisema.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako