NA. HONORIUS
MPANGALA
WAKATI aliyekuwa Rais wa awamu ya kwanza wa taifa
hili la Tanzania alikuwa kiongozi aliyewaunganisha watanganyika, sasa mambo
yamekuwa tofauti kiasi. Katika hili wako ambao wanashindwa kukemea kutokana na
mitazamo ya namna gani wataweza kuonekana mbele ya wenzao kiitikadi.
Hatuko kama majirani zetu kwasababuya
misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili ni mizuri na inayowafanya
wananchi wake kuwa na hofu ya mungu.
Ni jambo la kawaida sana kumkuta mtanzania wa
kabila la kisukuma akiwa na mifugo yake katika bondel la mto Lwika huko wilayani
Nyasa akiipa malisho mifugo hiyo. Ni kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na
waasisi wa taifa letu kwa kuondoa suala la ukabila miongoni mwa watanzania.
Tangu taifa hili liasisiwe hakuja wahi tokea
ugomvi wowote uliohusisha makabila moja na jingine. Hii ni kutokana na
kujaliana kwetu na kufuata ile misingi ya ugugu baina yetu kama taifa moja. Katika upande wa masuala ya kiimani iliwahi
kutokea mara moja katika utawala wa awamu ya tano,mgomo wa wakristo na
waisalamu ambao ulihusisha suala la kuchinja.
Wakristo walikuja na hoja ya kutaka kuchinja pia
huku wakihoji kwanini suala la kuchinja liwe kwa waislamu pekee. Mgogoro ule
haukuchukua muda mrefu kwani uliisha kwasababu ya ubora wa watatuzi wa masuala
ya kijamii na hata kuenzi ile tunu yetu kama taifa.
Viongozi wetu walifanikiwa katika sana katika
kutufanya watanzania kuwa watu tunao ishi kama ndugu.Lakini kwa miakamya hivi
karibuni kumekuwa na matukio au vitendo visivyo vya kawaida kutokea katika
taifa letu.
Siasa imekuwa sehemu ambayo watu wanaitafsiri
tofauti kulingana na matukio au mienendo yake katika taifa letu. Imefika wakati
wazazi wa kitanzania wakiona motto wao anajiingiza katika masuala ya kisisasa
basi huweza kukutana hata kauli za kutolewa maneno makali na mzazi kwani mvuto
wa kujiynga na masuala ya siasa umepotea. Kupotea kwa mvuto huo kwa wazazi
kunatokana na hofu yao juu ya matukio yanayohusisha wanasiasa katika asrdhi ya
Tanzania.
Katika mienendo isiyo ya kawaida Watanzania
wamefikia hatua hata ya kusaidiiana katika matatizo kwa kutazama ukubwa wa
tatizo kupitia chama cha kisisasa.Ni jambo la kawaida siku hizi kukuta katika
misiba wafuasi wa vyama vya siasa wakitinga sare zao misibani na kuendesha
msiba kwa kutazama marehemu alikuwa mfuasi wa chama gani.
Niliwahi shuhudia misiba iliyokuwa inahudumiwa na
wafuasia wa Chadema kwa kiasi kikubwa huku wakiwa wamevalia sare za chama chao.
Swali langu kwao lilionekana kama nawakejeri kwani nilikuwa nauliza “kuna
uhusiano gani wa msiba na chama cha kisiasa?” Lakini sikuweza kupata majibu
yaliyonifanya nitosheke.
Hali hii haikuwa kwa chadema pekee bali hata CCM
nao waliweza kufanya hayo katika misiba iliyowahusu wafuasi wao. Hivyo swali
kama nililowauliza wafuasi wachadema hata nwao niliwauliza lakini unakutana
majibu ya kushangaza sana kutoka kwa watanzania hawa.
Mra kazaa katika misiba inayomkuta mtu ambae
hayuko karibu sana na masuala ya kisiasa basi kinachotokea hapo ni michango
anayochangiwa mfiwa kuja kwa sura ya vyama vya siasa. Utakuta katika usomwaji michango unasikia chama
Fulani cha kisaisa kimetoa kimetoa mchango kiasi Fulani. Jmabo hili limeweza
kupenya katika ubongo wa watanzania na kufikia hatua ya kubaguana katika
masuala ya kijamii kama misiba.
Ukitokea msiba wa mfuasi wa Cuf basi unakuta
mfuasi wa CCM au Chadema akawa hana mwitiko mkubwa na tukio hilo labda awe
ndugu.
Kasumba hii ya kugawa watu kisiasa imekuja wakati
siasa za nchi hii zikiwa zimeshika kasi sana na mwitikio wa masuala ya kisiasa
ukiwa mkubwa pia.Kumekuwa na masuala yasiyo ya kiutu baina ya wafuasi wa vyama
vya siasa nchini.
Licha ya kwamba wale viongozi wakubwa wa vyama
vyao wamekuwa na mwonekano wa kuyakemea haya masuala yanayoendelea kwa wafuasi
wao lakini pia kwa namna moja ama nyingine bado hili suala halijapatiwa tiba na
linazidi mkuendelea baina ya wafuasi wa vyama vya siasa.
Kila inapotokea masuala ya kisiasa kama vile
kufanyika kwa uchaguzi mkuu au hata chaguzi ndogo ndogo za kuziba nafasi za
wagombea waliojiudhuru au kufariki, changamoto kubwa sana hutokea hasa katika
masuala ya ulinzi na usalama wa wafuasi wa vyama unakuwa sio wa kuridhisha.
Matukio ya kutekana au hata kuvamiwa na
kusababisha vifo vya baadhi ya wafuasi wa masuala ya siasa au viongozi
hujitiokeza sana. Na imekuwa kama tatizo sugu ambapo unakuja kusikia watenda
kosa au tukio kutopatikana ikiwa ni jambo ambalo linazidi kuwafanya watanzania
wengine kushindwa kuvielewa haraka vyombo vinavyohusika na masuala ya ulinzi na
usalama wa raia.
Leo hii ziko familia ambazo zimejenga chukiza wazi
dhidi ya wafuasi wa vyama fulani kutokana na yale wanayokutna nayo ndugu zao. Hata
kama itatokea umma ukataka kuaminishwa kuwa matukio haya hayana uhusiano na
masuala ya kisiasa unaweza kujikuta una umiza akili ili kujua ni masuala gani
mengine ambayo kiongzoi wa Chausta anaweza kukutana nayo na yakatoka katika
masuala binafsi na sio siasa anazofanya.
Tayari familia kama ya aliyekuwa katibu wa Chadema
Kata ya Hananasif mkoani Dar es salaam, Daniel John inashindwa kuelewa kwanini
ndugu yao alitekwa na kuteswa hadi kufa. Ni kipi ambacho kinaweza kikawa ni cha
nje ya masuala ya kisiasa na ikafanya aje kupata matatizo haya ya kutekwa?
Na mara nyingi masuala ya mihemko iliyo juu na
wafuasi kujifanya ni wako mstari wa mbele ili kutekeleza taratibu walizojiwekea
kama chama. Kila chama kikiwa na lengo la kushika dola
inahitajika utu na kuenzi tunu za taifa jambo ambalo linahitajika kufanyika ili
kuwafanya watanzania kuwa wamoja.
Nimewahi kushuhudia msiba wa mfuasi wa CCM vijsns
wengi katika eneo hilo la msiba walikuwa ni wafuasi wa Chadema basi waligoma
kwenda kuchimba kaburi kwasababu tu ya kumbukumbu zao juu ya familia ya
marehemu na marehemu kuwa wafuasi wakubwa wa chama cha mapinduzi. Unaweza
kuluiona kama jambo dogo lakini kwa jinsi linavyotafsiriwa na jamii ni tofauti
na linapanda mbegu mbaya miongoni mwa jamii.
Wanasiasa waacheni wafuasi wavyma vya siasa
wafanye siasa zao katika hali ya utulivu na amani. Vitendo vya vitisho na
kufikia hatua ya kuviziana kisa tu siasa itafika wakati tutashindwa kujua
tumlaumu nani,mamlaka au sisi kama jamii.
Siasa za kuviziana sio za kimaendeleo maana watu
husubiri wapi utaharibu ili wachukue hoja ya kuweza kuiongeza mbele yaw engine.
Maendeleo unakuja kwa ushirikiano uliopo baina ya jamii na viongozi wao wa
kisiasa,kitaalua na msiache mbegu mbaya au roho ya visasi ikataka kuota katika
mioyo hiyo. Yale yanayotokea leo yataweza kusishi kwa miaka mingi na kuwafanya
watu kuwa na roho za visasi.
Viongozi wa kisiasa wana kila sababu ya
kujitazama tena na kuona kama haya matukio yanayotokea wakati wa harakati
zakiuchaguzi ni kweli hayana mahusiano na siasa.Vyombo vya ulinzi na usalama wa raia wana kila
sababu ya kuwajuza watanzania namna gani wanafanikisha kukabiliana na matukio
yasiyo na utu katika nyakati za matukio ya kisiasa.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako