MWANDISHI WETU, KYELA
KAZI ya kuunda meli mpya ya abiria itakwayokuwa na uwezo wa kubeba abiria
200 pamoja na tani 200 za mzigo imefikia asilimia 60 tangu ilipoanza kutengenezwa mapema mwaka huu katika Bandari ya Kiwiwara wilayani hapa.
Taarifa kutoka wilayani hapa zinasema kuwa kazi hiyo inafanywa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kupitia kampuni ya kizawa ya Songoro. Kampuni hiyo ndiyo ilikamilisha meli mbili za mizigo, MV Ruvuma na MV Njombe
zinazofanya shughuli zake ndani ya Ziwa Nyasa.
Meli hiyo mpya inayoundwa inatarajiwa kusaidia kupunguza
matatizo ya usafiri katika Ziwa Nyasa pamoja na Wilaya ya tatu za Nyasa
(Ruvuma), Ludewa (Njombe) na Kyela (Mbeya) ambazo zimekuwa na shughuli nyingi za maendeleo lakini usafiri ulikuwa wa shida.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako