Honorius Mpangala, 0628994409 |
AKIWA katika kampeni za urais mwaka 2005 Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete katika ardhi ya Kyela Mkoani Mbeya alihaidi meli. Alirudia tena kauli hiyo alipokuwa katika ardhi ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma. Baada ya kipindi cha utawala wake hatimaye meli alizoahidi tayari zimeonwa na Wanyasa.
MV Njombe imekamilika na kufanikiwa safari moja ya majaribio kutoka Bandari ya Itungi
hadi Mbamba Bay. Yapo mambo ambayo ni
fursa kwa wakazi wa Nyasa kutokana Meli hii. Kama inavyoitwa ni meli ya mizigo
ni chombo kitakachoweza kuwainua kiuchumi wakaza wa Nyasa kama watakitumika
ipasavyo. Kuinuka kiuchumi kutatokana na kujikita katika shughuli ambazo wakazi
wake watajishughulisha na shughuli kama ilivyo kilimo biashara na hata ufugaji
wa kisasa na wenye tija katika maisha ya leo.
Kilimo
cha biashara ni moja ya ujasiriamali ambao watu wengi wamekuwa
wakijishughulisha nao. Katika mwambao wa Ziwa Nyasa hususani wilaya Nyasa yapo
mabonde ambayo yanaweza kufanyika kilimo cha mazao ya muda mfupi na kwa mfumo
wa kilimo cha umwagiliaji, na kile cha kutegema mvua na kuleta tija.
Meli
yetu inahitaji mizigo ya kutosha. Kwa maeneo kama ya Liuli katika mashamba
yaliyoko Nkalachi ni eneo ambalo ustawishaji wa mananasi na matikiti unaweza
kuwa wenye tija zaidi. Maeneo ya Mango kuna uzalishaji mkubwa wa
Manchungwa,machenza na mananasi pia.
Bonde
la Lundo ni eneo ambalo tangu zamani wakazi wa maeneo hayo walilima mahindi
wakati wa kiangazi na hata mazoa kama miwa hulimwa. Bonde lile kama sio siasa
basi Leo hii tungeona kiwanda cha utngenezaji wa sukari katika kijiji cha
Lundo.
Maeneo
ya Ndesule katika mji wa Mbamba bay ndiko uzalishaji wa mpunga unakofanyika
pamoja Taambachi. Katikati ya vijiji vya Kilosa,Likwilu na Linda kuna eneo
ambalo hufanyika uzalishaji mkubwa wa mpunga karibu na Ndecha. Undu na Matenje
wekuwa wakulima wakubwa wa tumbaku katika Bonde la mto Ruhekei. Zoole ni eneo
maarufu kwa kijiji cha Chiulu katika kilimo cha mpunga.
Maeneo
ya uzalishaji yamekuwa mengi na makubwa hata Kwa ukanda wa Lituhi pia.Kama
inavyofahamika vijiji vyake vyote vimekuwa vikilima sana zao la muhogo na kuwa
la chakula. Lakini kupitia kilimo biashara unaweza kuufanya muhogo ukawa zao la
chakula kulingana na watu wenyewe kama watataka kuyafikia masoko.
Ziko
nchi za jirani zenye uhitaji mkubwa wa mazoa toka Tanzania. Tangu zamani wakazi
wa Nyasa walisafirisha mihogo na mahindi kupeleka Malawi. Iliwahi kutokea
wakati Jakaya Kikwete akiwa mgombea wa Urais alitumia mamlaka yake ya uwaziri
wa mambo ya nje kuhoji juu ya Mizigo wa mahindi alioukuta Bandarini Mbamba bay.
Swali lake alitaka kujua ni wapi mahindi Yale yanapelekwa,swali ambalo Said
Kalembo aliyekuwa mkuu wa mkoa alishindwa kulijibu.
Moja
ya makosa yanayifanyika Kwa wakazi wa Nyasa ni kuamini uvuvi ni shughuli pekee
ambayo wanaweza kuifanya na kuwainua kiuchumi. Katika dunia ya sasa ambapo kila
taifa lina pambambana kujiimarisha kiuchumi linahitaji watu wachapa kazi katika
kufikia malengo ya kujiinua wao wenyewe na taifa Kwa ujumla. Baada ya shughuli
za kilimo Kwa msimu wa masika ni vyema watu wakatambua wanahitajika kuendelea
na kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yenye vyamnzo vizuri na vya uhakika vya
maji.
Unaweza
kuwa mzalishaji mzuri wa karoti, kabeji na hata tangawizi na kutafutiwa soko
katika maeneo tofauti na yale ya uzalishaji. Meli yetu itahitaji mizigo kutoka
maeneo mbalimbali na kufikisha sokoni mazao ya biashara. Kujikita katika
shughuli za kila siku lazima kutapunguza ulevi uliokithiri wa Wanzuki na watu
kutumia fursa ya uwepo wa meli ya mizigo katika kuzalisha na kifikisha mazao
sokoni.
Kama
ilivyo kwa wakazi wa maeneo ambayo reli imepita wamekuwa wakiitumia garimoshi
katika kusafirisha mizigo na kufikisha sokoni. Ukiwa Morogoro ni rahisi kuona
mizigo ya Asali ikishushwa katika kituo cha garimoshi. Ni asali inayotoka
Kigoma na kusafirishwa hadi Morogoro.
Pia
Utaona Mikungi ya ndizi inashushwa maeneo kama Dodoma ikitokea Kilosa ambako
imelimwa maeneo ya usagara. Watu wamekuwa wakitumia njia za usafirishaji katika
kujipatia fursa na kujiinua kiuchumi baada ya kutambua wapi yaliko masoko.
Ni
lazima tubadili mitazamo yetu katika kutambua tunahitajika kupambana ili kuinua
uchumi wa maeneo yetu Kwa kufanya kazi. Nchi za Malawi na Msumbiji na hata nchi
za maziwa makuu tunaweza kuzitumia katika kufikisha mazoa yetu na kufanya
biashara na kutambua umuhimu wa kilimo biashara.
Yapo
mazao ambayo hayajozoeleka sana katika ulimwaji wake na ni mazoe yenye tija.
Mazao kama ya Tangawizi, Karoti na hata Ufuta ni mazao ambayo watu wanaweza
kulima na kufanikisha soko la mazao hayo kutambulika ni wapi hupatikana. Ili
kufanikisha biashara ya mazao ambayo itafanya meli ya mizigo kupata mizigo ya
kufikisha katika eneo ambalo kuna uwezekano mkubwa wa kufanya biashara.
Raha
ya hii meli itakuwa nzuri sana kama itapita katika vituo vyake kama vya Lundu, Mkili,
Nsinsi, Ifungu, Rumbila, Lupingu, Manda Njambe na kupakia mizigo ya kutosha na
kufikisha maeneo mengine kwa ajili ya kufikishwa sokoni.
0628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako