May 04, 2008
Janeti na Kumbukumbu Ya Safari Ya Nyasa
Hivi unakumbuka kile kisa cha Janeti kufika hapa Nyasa?Kama umesahau hebu soma tena kwani niliandika kwamba katua Nyasa na salamu yake ikawa neno moja tu 'inyahi'.Basi baada ya kuondoka Nyasa dada Janeti yupo huko mjini lakini anakumbuka Nyasa haambiliki,anasifia wanyasa wakarimu,wapole na wapenda kazi kwa manufaa ya maisha.Sasa dada Janeti anajua maneno lukuki ya lugha yetu ya hapa nyasa.Ngoja nikwambie ili ujue sitanii.Kanitumia ujumbe wa barua kama ujuavyo sisi simu tunasikia tu kwamba kuna mitandao lakini angalau kuna makampuni yameanza kujenga minara ya mitandano yao ila sikutajii msomaji,wewe nipige tu lakini sitaji ng'oo.Kaandika barua kwa mbembwe na mikogo ya hapa na pale,maneno ya kinyasa.Kifupi anakumbuka nyasa kwa kiasi kikubwa.Ndiyo maana niliandika wazazi kuwaacha watoto wao waishi bila kuwafundisha walikotokea ni makosa makubwa.Na kwa kutumia Janeti inajionyesha kwamba anapenda kujifunza jambo toka hapa kwetu nyasa ambako ametokea mzazi wake mmoja.Kwa mujibu wake kadiri barua yake alivyoandika,anaweza kusalimia na kuongeza/kurefusha mazungumzo kwa kutumia lugha ya hapa nyasa.Basi anachombeza kwa maneno ya kinyasa humo kwenye barua yake na kumalizia kwamba 'atarudi tena nyasa' kwani kwasasa ni kama nyumbani kwake yaani kama kavumbua dunia nyingine achilia mbali mchanganyiko wa makabila huko mijini.Lakini ni faraja sana kuthamini maisha yetu wanyasa.
Madhumuni
kumbukumbu,
mila na desturi,
Nyasa
WASIFU: Mwandishi wa Habari,Tawasifu,Mhariri na Mchambuzi wa Vitabu,Siasa, Utamaduni, Michezo,Afrika, Kimataifa,Mshauri wa Habari na Mikakati. TUWASILIANE: mawazoni15@gmail.com, lundunyasa@yahoo.com. WHATSAPP; +255 719226293/SMS; +255 764 936655
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako