Na Ezekiel Kamwaga
Nauli ya bei nafuu kabisa kutoka Dar-Luanda-Dar ni dola 1000
kwa kichwa. Simba imekwenda Angola pasipo kutembeza bakuli kwa mtu. Na wote
waliosafiri wakalipwa posho kwa USD (si kwa fedha za madafu). Fedha hizo ni
mara kumi ya zile ambazo wachezaji walikuwa wakilipwa miaka minne hadi sita
iliyopita wakiwa safarini na Simba....
Leo inazushwa kwamba eti Simba haina
fedha za kwenda Kagera ndiyo maana inapita Dodoma, Tabora, Shinyanga kucheza
ndondo!!!!!! Inachekesha. Gharama ya mafuta, kwa sababu Simba ina basi lake, haifikii
hata nauli ya mtu mmoja kwenda Angola... Sasa vije leo isemwe eti Simba haina
fedha za kwenda Mwanza? Yaani za kwenda Angola zipo ila za Mwanza hakuna? Kuna
sababu kubwa mbili kwanini timu inakwenda Kagera TARATIBU.
Mosi, zaidi ya nusu
ya wachezaji waliosafiri wanatoka TIMU B na wengine hawajawahi kufundishwa na
Patrick Liewig. Benchi la ufundi liliona ni vema hawa wapate nafasi ya
kujaribiwa katika mechi ya kirafiki ili wajue kocha anahitaji nini na kocha
awafahamu zaidi wachezaji wake. Ikumbukwe pia, kiufundi, Simba haikutakiwa kuwa
na mechi kwa wiki zaidi ya mbili kutokana na ratiba iliyozingatia ushiriki wake
kwenye Ligi ya MABINGWA.
Hiyo ni sababu ya kiufundi. Kuna sababu ya 2 ambayo ni
ya kimantiki. Kwamba Simba ni klabu ya Watanzania wote na si wale walioko Dar
es Salaam na mikoa yenye timu za Ligi Kuu. Kuna mikoa kama Tabora ambayo Simba
haijacheza kwa takribani miaka 10 lakini wapo Wana Simba ambao wangependa
kuiona. Vivyo hivyo kwa Shinyanga ambapo tulipata sapoti kubwa sana
tulipokwenda mwaka jana.
Tunahitaji kuwafurahisha wapenzi wetu wa kona zote.
Tunahitaji pia kutengeneza fan base kubwa zaidi hata kwa watoto ambao wataiona
Simba ikicheza Tabora.... Mwaka jana tulipeleka Kombe letu katika baadhi ya
mikoa. Mara baada ya kumalizika kwa ligi msimu huu, tuna mpango wa kwenda
kwenye mikoa ambayo Simba haijakwenda kwa miaka mingi... Mikoa kama vile Rukwa,
Kigoma, Singida, Mara, Iringa n.k...
Jamani huko kote kuna washabiki wa Simba
na watafurahi kuiona ikicheza mbele ya macho yao. TUNASUBIRI KWA HAMU pia
tuambiwe tunaenda kucheza ndondo wakati huo ! Watu wanafikiri Man United
inakwenda China kufanya mazoezi pekee!!!! Hapana, inakwenda kutangaza brand
yake ili wapate pa kuuza merchandise yao... Tutakwenda kote itakakowezekana,
INSHALLAH... Ili mradi Simba ikianza kufanya biashara huko tuendako, na wakati
huo utafika tu, tusianze kuulizana tulimtumia MGANGA gani kufanya biashara ya
merchandise yetu vizuri.... Hiki ndicho kile rafiki yangu John Shibuda huwa
anakiita kwa maneno mawili tu; FIKRA MCHAKATO....
No comments:
Post a Comment
Maoni yako