Na Mwandishi Wetu,Cologne, Ujerumani
Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania Wanaoishi Ujerumani ,
chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) Waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno
"MUUNGANO" lina maana
kamili kwa maisha ya
mtanzania na binadamu wengine.
Sherehe hizo zilizowakusanya watanzania na marafiki wa
Tazania kutoka kila kona ya ujerumani,
ziliutingisha mji wa koloni katika Usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49
ya muungano wa Tanzania.
Mhe.Ali Siwa naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani
alikua mstari wa mbele akiwaongoza watanzania katika Muungano Day,
|
Dada Nashe Mvungi akionyesha bidhaa za Tanzania kwa wageni |
|
Dada Tabia Mwanjelwa(mwenye) gitaa akiwa na wasanii wenzie jukwaani |
|
hakubaki mtu nyumbani |
|
maana ya muungano yakubalika na watoto wa kimataifa !ngoma inogile |
|
Mh.Ali Siwa,mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania,Berlin akitoa hotuba ya Ufunguzi, |
|
Mh.Ali Siwa wa Ubalozi wa TZ Berlin,akizungumza na Mzee.Katabalo (mtumishi mstaafu wa UN) |
|
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shah Smooth akiwarusha wageni |
|
Muungano oyeeee! huyu dogo naye ndani ya nyumba |
|
wageni mbali mbali wakiipongeza Tanzania, mwenyekiti wa UTU Mh. Mfundo aliyevaa shati la kitenge akiongoza shughuli |
|
Mhe.Ali Siwa akiwa Msanii John Gambula kutoka Bagamoyo |
|
Msanii Dada Joanita Henry(Mwenyeji wa muungano Day Koloni) akiwa na msanii mwenziwe kutoka Zimbabwe |
|
Watanzania Ujerumani wakiduarika ktk Sherehe za muungani,mjini Koloni |
|
wasanii wa kitanzania wakiepeperusha TZ katika maigizo n.k |
|
wasanii wa kikundi cha Wabantu group wakiipeperusha TZ |
|
wageni wakijichagulia Bidhaa za Tanzania |
Wasanii mbali mbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha
vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na
kamati yake wameahidi
kufanya mambo makubwa na kuitangaza Tanzania kwa hali na mali chini ya Umoja
wa watanzania Ujerumani(UTU)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako