Na Vitus Matembo, Mbamba Bay
MBOLEA YA RUZUKU: Wakulima wengi wa Nyasa hawaitumii mbolea
ya Ruzuku ya Serikali, na kuwaachia watu toka Mbinga kuja kuichukua. AJABU, Mtu
akitumia na akapata mavuno mengi. Wanafikiria ni WIZI WA KISHIRIKINA.
UVIVU: Namnukuu Mkuu wa Wilaya, Mh.ERNEST KAHINDI, huwa
anasema daima "Wakulima wengi ukanda wa Ziwa Nyasa ni Wavivu kwakuwa
hufanya kazi kwa muda mfupi, yaani toka saa 12.00 asubuhi hadi saa 3:00
asubuhi. Tofauti na maeneo mengne wanaotegemea Kilimo".
NYANYA TOKA NYASA HAZINA UBORA NA HUOZA MAPEMA: Wakulima
wengi wanajitahidi kulima Nyanya ila kutozihudumia ipasavyo na madawa
husababisha wafanyabiashara toka Nyasa kununua Nyanya toka Mbinga na Songea.
Wakati Nyasa kuna mito na ardhi nzuri.
KILIMO CHA KOROSHO: Nakumbuka Meja Generali Mstaafu
S.S.KALEMBO aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alihimiza sana Wanyasa tulime zao
la Korosho kwakuwa ardhi ya Nyasa ni nzuri kwa kilimo hicho kama ilivyo
Tunduru, Lindi na Mtwara. Ila sijajua tatzo nini?.
KILIMO CHA MIWA NA KIWANDA CHA SUKARI LUNDO JAMANI
KIMEKUFAJE.
KILIMO CHA TUMBAKU SIJUI KIMEFIA WAPI KULE RUHEKEI.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako