NA VITUS MATEMBO, MBAMBA BAY
Mwonekano wa ufukwe wa Mkwakwa katika Ziwa Nyasa. |
Hii ni kweli hata kama ulikua hujui kubali tu, maana ndio
ukweli uliopo.
1. Mtu hufanya ishara nyingi za mikono akiwa anazungumza
ukweli. Azungumzae uongo mikono yake huwa imetulia zaidi.
2. Sikiliza kwa makini namna mtu anavyozungumzia watu
wengine akiwa na wewe, na ndivyo atakavyokuzungumzia wewe akiwa na watu
wengine.
3. Ndoto zako zinabeba ujumbe mhimu sana. Asilimia 70 ya
ndoto zako zina ujumbe wa siri.
4. Kwa kawaida watu huwa waaminifu na wakweli mwili ukiwa
umechoka, na ndio sababu hutubu na kutoa siri zao kwenye mazungumzo yatekeayo
usiku wa manane,
5. Ukihisi mtu au watu wanakuangalia, angalia saa au muda
kama unataka kujua wakati, watu wanaokutazama nao watatizama saa, hii ni kwa
sababu kuangalia wakati/mda huambukiza.
6. Kunywa maji ya baridi sana mapema asubuhi husaidia mwili
wako kufanya kazi vizuri hadi asilimia 25.
7. Kukumbatiana huondoa shauku, msongo wa mawazo na huongeza
kinga ya mwili.
8. Kushindwa kumtoa mtu akilini mwako imamaanisha kwamba
nawe upo akilini mwa mtu huyo.
9. Watu wenya akili yenye ubunifu hupata shida sana kupata
usingizi, hivyo hupendelea kuwa macho hadi usiku wa manane.
10. Kama utakataliwa na mtu ambaye kujali kwake ni muhimu
sana kwako, basi maumivu utakayopata katika ubongo wako ni kama maumivu ya
mwili yanavyokuwa.
11. Mtu ambaye ametendwa au ameumizwa kisaikolojia huwa na
hulka ya kukasirika pasipo sababu yeyote ya msingi.
12. Ukitaka kujua kama mtu unaezumguza nae anapenda kusikia
unayoyazungumza kunja mikono yako, kama anapenda na anafurahia mazungumzo nae
atakunja mikono pia.
13. Kama mtu anachekacheka tu bila sababu maalumu au
anacheka sana, basi mtu huyo ana huzuni kuu moyoni mwake, na kama mtu analala
kwa mda mrefu sana, mtu huyo ni mpweke.
14. Namna tunavyozungumza na watoto wetu ndivyo inavyokuwa
sauti katika mioyo yao.
15. Mtu akitokea katika ndoto unayoota, basi ni kwa sababu
mtu huyo kakuhamu (kakumiss).
16. Wa kwanza kuomba msamaha sikuzote ni mwerevu, wa kwanza
kusamehe ni mwenye nguvu na wa kwanza kusahau ni mwenye furaha.
17. Mashairi katika wimbo uupendao ni ujumbe ambao
unapambana kuufikisha mahala flani au kuwaambia watu flani.
18. Ukitumia mkono wako usiotumika mara kwa mara (wa kushoto
kwa wengi) itakusaidia kuwa na ‘self control’.
19. Kama mwanaume atasimama akiwa ametanua miguu yake wakati
akizungumza na mwanamke, ni ishara kwamba mwanaume huyo anampenda mwanamke kwa
dhati.
20. Mwanaume akiwa hajisikii huru au akiwa hana amani, basi
hushika kichwa au uso wakati mwanamke hushika aidha nywele, hereni, mavazi,
mikono au shingo.
21. Siku zote fuata wazo linalokuogopesha zaidi, sababu hili
ndili litakalo kujenga na kukuimarisha.
22. Aina mbili ya watu ambao hawatakuangalia machoni: mtu
anaejaribu kuficha uongo na mtu anaejaribu kuficha mapenzi/ upendo.
23. Wanasaikolojia wanasema mtu anataka kumfurahisha kila
mtu huishia kuwa mpweke zaidi.
24. Mtu anaekasirika kirahisi, kwa vitu vya kijinga,
inaonesha kwamba anahitaji upendo/kupendwa.
25. Sikuzote wanaoponda au kulalamikia wengine kwa
wanayofanya, ndicho kile wanachofanya wao au wanatamani kufanya wao- elewa
hili.
26. Kulia ni afya kwako. Huondoa bacteria wabaya mwilini
mwako, hukupunguzia msongo wa mawazo na kukuongezea kinga ya mwili.
27. Saikolojia inasema: Huogopi kupenda, unachoogopa ni
kutokupendwa (afraid of not being loved back).
28. Ukweli wa mambo: uko karibu zaidi na kufanikisha malengo
yako kama utayaweka kuwa yako pekee, yaani kuwa ni siri yako.
29. Saikolojia inasema: kujifanya mwenye furaha wakati una
maumivu ni mfano wa kuonesha ni jinsi gani wewe ni mwanadamu mweye nguvu.
(strong person).
30. Kabla ya kulala, asilimia 90 ya akili yako huanza
kufikiri mambo ambayo ungependa yatokee.
31. Watu wanaotembea kwa hatua za harakaharaka huonekana
kuwa wanajiamini na wenye furaha zaidi kuliko wanaotembea taratibu.
32. Watu wanaojua utani zaidi wanajua kusoma akili za watu
pia.
33. Ubongo wa mwanadamu alielala unaweza kuelewa mazunguzo
ya watu walio karibu eneo hilo.
34. Ukiwa uaongea na mtu, ongea huku ukitaja jina lake, hii
itasaidia kupendwa zaidi na mtu huyo.
35. Kufuatana na uchunguzi wa wataalam, kumtamani mtu
kingono hiushia miezi minne, zaidi ya hapo utakuwa ni upendo wa dhati.
36. Uchunguzi unaonesha kuwa watu wanaolala na mito mingi ni
wenye msongo wa mawazo na wapweke.
37. Umbo la ubongo wako hubadilika kila unapojifunza jambo
jipya.
38. Watu wakiwa katika kundi na ikatokea kuna kucheka, wale
walio na mahusiano ya karibu zaidi hutizamana.
39. Kwa namna mwandiko wa mtu unavyokosa mpangilio au kuwa
mbaya ndio kiashirio kwamba mtu huyo anafikiri haraka zaidi ya mikono yake
inavyoweza kuandika.
40. Kuna watu wana alama ya asili ya kuwaamsha muda
wanaotaka, hii ni kwa sababu wana homoni ya asili ya stress.
41. Haiwezekani kukaa na hasira dhidi ya umpendae kwa mda
mrefu. Hasira inayofika siku tatu au zaidi inamaanisha kwamba hauna upendo.
42. Chakula cha kwenya ndege hakina ladha sana sababu uwezo
wetu wa kutambua ladha hupungua kwa asilimia 20 hadi 50 tukiwa angani.
43. Kama urafiki utafikisha miaka saba, basi urafiki huo
utadumu milele.
44. Kama mtu akiongea na wewe halafu kwenye maongezi
akakungalia machoni kwa asilimia 60 ya maongezi basi umemboa mtu huyo. Kama
atakuangalia kwa asilimia 80 basi umemvutia mtu huyo na kama itafikia asilimia
100 basi mtu huyo anakutishia.
45. Katika sekunde tatu za mwanzo unapoamka, huwezi kumbuka
chochote.
46. Uoga waweza kuua. Hii ni kwa sababu mwili huzalisha
adrenalin ambayo ni sumu ikizidi. 47. Kawaida, mtu akianza kulia atakumbukaia
matukio mengine yaliyomsikitisha au kumchukiza ili kuongezea ubongo wake hamu
ya kulia.
48. Unapopiga chafya, unakufa kwa sekunde. 49. Unapotekenywa
hucheki, bali ni itikio na kupaniki (panic response). Huwezi jitekenya mwenyewe
kwa sababu mwili hauhisi hatari yoyote. Kawaida enzi za zamani kutekenya
ilitumika kama adhabu.
50. Kukosa usingizi husababisha ubongo kutokumbuka mambo
kiusahihi
No comments:
Post a Comment
Maoni yako