Na Kizito Mpangala
Zolile Hector Pietersen
alizaliwa tarehe 19/08/1963 mjini Soweto nchini
Afrika Kusini wakati falsafa ya ubaguzi wa rangi ikiwa imepamba moto. Falsafa
ya ubaguzi wa rangi ilikuwa ikijulikana kama Apartheid, ambayo ilikuwa ikiendeshwa na makaburu waliokuwa
wakitawala nchi ya Afrika Kusini.
Zolile Hector Pietersen akiwa amebebwa na Mbuyisa Makhubo baada ya kupgwa risasi. kushoto ni Antoinete Sithole, dada yake Zolile Hector Pietersen akilia. |
Jina halisi la ukoo wake ambalo
lilikuwa likitumika na familia yake ni Pitso,
lakini fdamilia hiyo ililazimika kubadili na kuwa Pietersen ili kuendana na falsafa ya Apartheid, na kujihisi kama wao ni makaburu ilhali wakiwa ni weusi.
Familia hiyo iliamaua kufanya hivyo ili kukwepa dhuruma za makaburu. Hata jina
la Zolile lilifutwa kwa muda ili apate nafasi ya kusoma.
Zolile Hector Pietersen alikuwa
akihudhuria shuleni kwa taabu hasa alipokuwa akipita sehemu mbalimbali ili
kuelekea shuleni. Alipita kwa wasiwasi mkubwa akiwa na hofu ya kufyatuliwa risasi.
Baadae alizoea hali ya milio ya risasi mara kwa mara katika mji wa Soweto. Alikuwa akienda shuleni mara
nyingi akiambatana na dada yake Antoinete Sithole pamoja na rafiki yao kipenzi
Mbuyisa Makhubo. Mbuyisa Makhubo alimtangulia Zolile Hector Pietersen miaka
mitano kuzaliwa, hivyo alimchukulia kama kaka yake. Watatu hao walikuwa na
furaha wanapokutana na kuzungumza pamoja na vilevile wakati wa shida hawakukosa
kuwa pamoja ilipobidi.
Serikali ya Makaburu nchini
Afrika Kusini iliweka utaratibu wa 50/50 katika
mitaala yote hasa katika elimu ya msingi na sekondari. Kulikuwa na masomo
muhimu zaidi ambayo yalikuwa yakifundishwa kwa lugha ya kiingereza, na yale
ambayo hayakuwa na umuhimu sana yalikuwa yakifundishwa katika lugha ya
Kiafrikaan. Na mitihani ilikuwa ikitolewa kulingana na lugha husika inayotumika
kufundishia katika somo husika.
Tarehe 16 mwezi Juni mwaka 1976, Zolile
Hector Pietersen, Antoinete Sithole pamoja na rafiki yao kipenzi Mbuyisa
Makhubo walipokuwa shuleni wakihudhuria masomo walifikwa na wakati mgumu
walipoanza kugoma kufundishwa masomo kwa lugha ya Kiingereza badala ya lugha
yao mama ya Kiafrikaan. Ndipo polisi wa makaburu walipoanza vurugu ya
kuwashambulia wanafunzi pamoja na watu wengine.
Wanafunzi walikusanyika pamoja
kwa amani na kueleza kile walichokuwa wakikipinga katika taaluma. Muda mfupi
baadae, mkusanyiko wa wanafunzi hao wakiwemo Zolile Hector Pietersen, Antoinete
sithole na Mbuyisa Makhubo, ulishambuliwa mara tu polisi walipowasili shuleni
hapo. Ndipo wanafunzi hao walianza kuokota mawe na kuwarushia polisi wa
makaburu waliofika kuwatawanya kwa risasi.
Mkusanyiko wa wanafunzi hao
ulikuwa na wanafunzi yapata 13,000 pamoja na wafanyakazi
weusi wa shule hiyo ambapo katika wafanyakazi wa shule hiyo, wawili waliuawa
kwa kupigwa risasi na polisi wa Makaburu. Kwa ghadhabu, wanafunzi waliaongeza
fujo ili kutetea haki ya kitaaluma waliyokuwa wakiidai na vilevile kulinda utu
wao. Walichoma magari kadhaa moto na majengo. Pia walilishambulia jengo la
kiengo cha Elimu mkoa wa Transvaal.
Wanafunzi 30
walikusanyika nje ya shule ya sekondari ya Phefeni wakiwa wanaimba wimbo mkuu
wa Kisotho. Polisi walipowasili katika shule hiyo, mkusanyiko huo nao
ulishambuliwa na polisi hao ambapo wanafunzi nao walikuwa wakiwarushia mawe
polisi. Polisi walifyatua mabomu ya gesi inayoumiza macho na kutoa machozi kwa
wanafunzi hao. Haijulikani nani alitoa amri ya kuatumika kwa risasi za moto
kuwafyatulia mkusanyiko ule wa wanafunzi. Wanafunzi hao walianza kukimbia na
kutawanyika ovyo ili kuokoa maisha yao. Wengine walikuwa wakigalagala
barabarani wakilalamika maumivu baada ya kupigwa risasi.
Zolile Hector Pieterson
alilipotiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza kufariki baada ya kuwasili katika
zahanati akiwa na majeraha ya risasi. Lakini pia mwanafunzi Hasting Ndlovu
alilipotiwa kufariki kutokana na majeraha ya risasi alizopigwa na polisi wa
Makaburu. Lakini kutokana na kutokuwepo kwa picha iliyopigwa ya Hastings
Ndlovu, imehesabiwa kuwa mwanafunzi aliyewapa simazi watu wengi nchini Afrika kusini
ni ZOLILE HECTOR PIERTERSEN.
Zolile Hector Pietersen
alipopigwa risasi akiwa na dada yake pamoja na rafiki yao kipenzi Mbuyisa
Makhubo, alidondokea katika kona ya nyumba moja mpakani mwa mtaa wa Moema na
mataa wa Vilakazi aliinuliwa na Mbuyisa Makhubo akiwa na dada yake Antoinete
Sithole.
Zolile Hector Pietersen akiingizwa kwenye gari la mwandishi wa habari na mpiga picha, Sam Nzima ili kupelekwa Zahanati, ambapo alifariki muda mfupi baada ya kuwasili Zahanati. |
Zolile Hector Pietersen
alibebwa na Mbuyisa Makhubo mpaka kwenye gari la mwandishi wa habari mweusi
bwana Sam Nzima na kumuingiza garini bila hata kuomba. Sam Nzima alipoona
ujasiri wa Mbuyisa Makhubo akiwa na dada yake Zolie, alitoa kamera yake na
kuwapiga picha walipokuwa wakisogea kwenye gari lake na kuamua kuwasaidia.
Ndipo Zolile Hector Pietersen alipokimbizwa katika Zahanati ya Phenfeni. Gari
lilikuwa likiendeshwa na mwandishi wa habari Sophie Tema ambaye aliambatana na
Sam Nzima. Muda mfupi baada ya kumkabidhi Zolile Hector Pietersen kwa wahudumu
wa afya ilitangazwa kwamba amefariki.
Mbuyisa Makhubo na Antoinete
Sithole walilazimika kujificha kwa kuwa polisi walifika hadi zahanati hapo ili
kuwavuruga kutokana na kitndo cha kumuinua Zolile Hector Pietersen na kumpeleka
Zahanati hapo. Polisi hao pia walimuandama mwandishi wa habari na mpiga picha,
Sam Nzima na kumpekua ili kuangalia picha alizopiga. Kwa bahati njema kama
alivyosema yeye mwenyewe kwamba picha ya Zolile Hector Pietersen baada ya
kupiga alichomoa mkanda na kuuficha kisha akaweka mkanda mwingine kwenye kamera
yake. Ndipo polisi walipokosa walichokitaka. Polisi walikuwa wakizuia kupigwa
picha yoyote katika tukio la mauaji hayo.
Muda mfupi baadae picha hiyo
ikawekwa wazi na ikawa maarufu sana hasa nchini Urusi ambapo Sam Nzima
alipongezwa, lakini polisi wa Makaburu hawakuwa na furaha ndipo walipoanza kumsaka
Sam Nzima. Sama Nzima alisakwa na polisi wa Makaburu mara tu picha hiyo
ilipotokea katika gazeti mojawapo nchini Urusi. Polisi waliamua kumsaka Sam
Nzima kutokana na hasira dhidi ya Urusi kulisaidia silaha kundi la UMKONTHO WE SINZWE lilikuwa likipinga
ubaguzi wa rangi nchini humo.
Watalii wakiwa katika makumbusho ya kumbukumbu ya Zolile Hectror Pietersen wakitazama picha inayomwonysha Zolile Hector Pietersen akibebwa na Mbuyisa Makhubo. |
Zolile Hector Pietersen na
Hastings Ndlovu walizikwa katika eneo moja mabalo hadi sasa limekuwa eneo
maarufu kwa ajili ya makumbusho ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo.
Eneo hilo linaitwa HECTOR PIETERSON
MEMORIAL AND MUSEUM. Makumbusho hayo yapo katika mji wa Orlando Magharibi,
barabara ya Khumalo nchini humo.
Zolile Hector Pietersen
alipigwa risasi na kufariki akiwa na umri wa miaka 13 tu. Tukio
la kupigwa risasi Zozile Hector Pieterson limekuwa alama muhimu ya kuheshimu
watoto wa Afrika.Kaburi la Zolile Pietersen |
Zolile Hector Pietersen
alifanywa kuwa mwakilishi wa wanafunzi wote waliofikwa na udhalimu wa polisi wa
makaburu siku ya tukio tarehe 16/06/1976.
Kutokea hapo, kila mwaka barani Afrika hufanyika kumbukumbu ya siku ya mauaji
hayo ya kimbari. Na kwa kuwa waliofikwa na madhila hayo wengi wao ni wanafunzi,
basi siku hiyo ikaitwa SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ambayo hufanyika 16/06 kila
mwaka kwa kauli mbiu mbalimbali. Siku hiyo pia, cnhini Afrika Kusini hujulikana
zaidi kama SIKU YA UDHALIMU WA FALSFASA YA APARTHEID. Lakini kwa ujumla imekuwa
siku ya kuwaheshimu watoto wa Afrika na kusikiliza mahaitaji yao.
Mwaka 2002
makumbusho ya kumbukumbu ya Zolile Hector Pietersen yalifunguliwa na kupewa
jina la HECTOR PIETERSEN MEMORIAL AND
MUSEUM. Eneo hilo lilifadhiliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii nchini
Afrika Kusini kwa kiasi cha fedha Rand milioni 16 kwa
kusaidiana na Halamshauri ya jiji la Johannesburg ambayo ilichangia kiasi cha
Rand milion 7.2. Antoinete Sithole, dada ya Zolile Hector Pietersen ambaye ndiye aliyenyosha mkono katika picha ya siku ya tukio la ghasia za mjini Soweto. |
HECTOR
PIETERSEN MEMORIAL AND MUSEUM kwa sasa ni kivutio kikubwa cha
utalii nchini Afrika Kusini ambapo mwanzoni mwa makumbusho hayo yaani eneo la
mwanzo kuingia imewekwa picha maarufu nchini humo ikimuonyesha Mbuyisa Makhubo
akiwa ambmbeba Zolile Hector Pietersen akiwa pamona na dada yake, Antoinete
Sithole. Na dada yake Zolile Hector Pietersen ambaye yumo katika picha hiyo
maarufu, ni mafanyakazi katika makumbusho hayo akiwa kama kiongozi wa kuongoza
watalii.
© Kizito Mpangala (0692
555 874)
23/01/2018
No comments:
Post a Comment
Maoni yako