Ben Saaanane |
Na Ben Saanane, Dar es Salaam
Hebu tuone:Chama cha Patriotic Front cha
Zambia(Ninakifananisha na CHADEMA katika Historia na Harakati zake Kuchukua
Dola) kilichoanzishwa Mwaka 2001 kimeweza kuwa chama imara kwa kuwachukulia
hatua wasaliti bila kujali cheo au nafasi ya mtu.
Leo hii tunapoandika hapa waziri wa mambo ya nje Given
Lubinda anajiandaa kukutana na kamati ya Nidhamu ya chama hicho kwa tuhuma za
kukisaliti chama hicho na kushirikiana na vyama hasimu.
Akipatikana na hatia kwenye kamati kuu ya PF atafukuzwa
uanachama moja kwa moja.
Pia wakati huo huo kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema
wa chama cha UPND(nilishawahi kukifananisha na chama cha CUF) anakabiliwa na
mashtaka ya defamation huku chama Tawala cha Zamani cha MMD(CCM ya Zambia
iliyounda aliiance na UPND kuihujumu PF) kikipambana kujinusuru kisifutwe kwa
kukiuka sheria na kuhodhi mali za umma.Huu ni mfano mzuri wa kufuata misingi na
sio kufuata watu.
Hakuna aliyewahi kuwa juu ya chama.Chama cha ODM nchini
Kenya kilichoanzishwa mwaka 2005 kilionyesha njia kuwaondoa akina Ruto,Chama
cha MDC nchini Zimbabwe kilichoanzishwa mwaka 1999 kilionyesha njia kwa
kuwaacha akina prof.Arthur Mutambara,CCM Chini ya uenyekiti wa Mwl.Nyerere
kilifuata Misingi kwa kumfukuza Maalimu Seif akiwa waziri kiongozi(NASIZITIZA
CCM ya NYERERE)....CHADEMA leo kimefikisha miaka 20 Rasmi tangu kisajiliwe.
Tuendelee kufuata misingi kwa mifano hii.Happy Birthday
CHADEMA,Viva M4C
No comments:
Post a Comment
Maoni yako