Na Hance Forogo, Dar es salaam
Mzee wetu tunayempa Heshima leo alizaliwa mwaka 1938 katika
wilaya ya Mbulu iliyoko mkoa wa Arusha....hapa namzungumzia mzee John Steven
Akhwari!....akiwa kijana mdogo kabisa alianza kujiingiza katika mchezo wa
riadha na haikumchukua muda mrefu kuwa mwanariadha wa mbio ndefu wa kutegemewa
na Taifa la Tanzania akishiriki mashindano mengi ndani na nje ya Tanzania na
amewahi kuwa bingwa wa mbio ndefu wa bara la Afrika,pia mwaka 1970 alimaliza
mbio akiwa na 05 katika mashindano ya mbio ndefu kwa nchi za jumuia ya madola!....
Akitumia muda wa 2:15:05 wakati mshindi alitumia muda wa 2:09:28,inaaminika kuwa alikuwa ni mkimbiaji "World Class" mwenye hadhi ya dunia kati ya miaka ya 1960 na 1980!....
Akitumia muda wa 2:15:05 wakati mshindi alitumia muda wa 2:09:28,inaaminika kuwa alikuwa ni mkimbiaji "World Class" mwenye hadhi ya dunia kati ya miaka ya 1960 na 1980!....
Katika tukio la kihistoria,mzee Akhwari katika mashindano ya
Olimpiki mwaka 1938 nchini Mexico,katika mji wa Mexico akiwa wanafanya utani na
wakimbiaji wa kuviziana na wakimbiaji wengine ili kupitana na kuwania ushindi
alianguka ghafla akiwa amemaliza 19km kati ya 42km.
Baada ya kubanwa na misuli tatizo lililotokana na hali ya hewa kwani kabla hakuwa amefanya mazoezi katika mazingira yenye hali ya miinuko na hali ya nchi kama ya Mexico.
Kutokana na tukio hilo aliteguka goti na kupata jeraha kubwa pia alipata maumivu makali kwenye bega lake!.....hata hivyo aliendelea na mashindano na kumaliza wa mwisho akitumia muda wa 3:25:27 kati ya 57 waliomaliza mbio wakati wanariadha 18 hawakuweza kumaliza mbio huku mshindi Mamo Wolde toka Ethiopia akitumia muda wa 2:20:26!....baada ya muda mfupi kumaliza mbio zake,waandishi walimfuata na kumuuliza kwa nini aliendelea na mbio wakati alikuwa ameumia sana!?....

akajibu
kuwa "Nchi yangu(Tanzania) haikunituma kushiriki maili 5000,imenituma nije
kumaliza mbio za maili 5000" Jina lake linatumiwa na taasisi ya John Steven Akhwari
Athletic Foundation ambayo inatumika kuandaa wanamichezo wanaojiandaa kwa
mashindano ya Olimpiki,mwaka 2000 alialikwa kwenye mashindano ya Olimpiki
yaliyofanyika Sydney nchini Australia na baada ya hapo alichaguliwa kuwa balozi
wa heshima katika maandalizi ya mashindano ya Olimpiki jijini Beijing,China,pia
13/04/2008 alihusika na ubebaji wa Mwenge wa Olimpiki ulipokuja Tanzania katika
maandalizi ya Olimpiki!....
Licha ya kwamba mwaka 1983 mzee wetu alitunukiwa medal ya
heshima kama shujaa wa Taifa "National Hero Medal of Honor" hatuna
budi nasi pande hizi KUMPA HESHIMA ZAKE kwa juhudi kubwa na uzalendo alioufanya
kwa ajili ya nchi yake!....ameitangaza nchi kupitia mchezo wa riadha!.....
Huyo ndiye mzee John Steven Akhwari ambaye kwa sasa ni
mkulima stadi,hakika anastahili HESHIMA!....Thanx!...
No comments:
Post a Comment
Maoni yako