Na Markus Mpangala, Dar es Salaam
Hatua
ya Serikali kufuta matokeo ya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2012
yamepokelewa kwa hisia tofauti. Baadhi ya wataalamu wa sekta ya elimu wanaona
serikali haikuwa makini kufanya uamuzi wa kufuta matokeo hayo, kwa madai uamuzi
ulichukuliwa kisiasa zaidi badala ya taalamu.
Baadhi
ya wataalamu wanatetea ufanunuzi uliotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la
Mitihani nchini, Dk. Ndalichako. Katika baadhi ya mitihani wanafunzi waliandika
mashairi ya nyimbo za muziki, wakachora picha za wachezaji mfano Lionel Messi
na wengine wakachora picha za filamu za Zombi.
Hali
hii iliwashtua wengi na kuona mwelekeo mbaya wa sekta ya elimu nchini. Pamoja
na wazazi kulalamikia hali hiyo bado wameshindwa kuchukua hatua stahiki dhidi
ya watoto wao hivyo kuendelea kuilalamikia serikali.
“Ni
mkanganyiko tu! Serikali inatoa ufafanuzi ambao ukiuchambua unaona hauendani na
hasira za Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani, Profesa Rwekaza Mukandala. Baraza
limefanya kazi yake kitaalamu, lazima tuheshimu. Ningewaona wa maana sana kama
wangekuja na suluhu ya kuondokana na matatizo mabovu. Viongozi wa sasa walipata elimu bora zamani,
lakini leo wanasimamia matokeo machafu, siasa na dini zinatuathiri katika
kuiangalia NECTA,”
Hayo
ni maneno mazito ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, James Zotto.
Hakuishia hapo, akaongeza kwa kuchambua zaidi uamuzi wa serikali juu ya
kubatilisha matokeo hayo.
James
Zotto alitoa mfano muhimu ambao unahusisha baadhi ya wahitimu wa Vyuo Vikuu
ambao waliwahi kuomba kazi, lakini hawkauwa na weledi wa kutosha licha ya kuwa
na matokeo mazuri sana katika vyeti vyao.
“'Msomi
mmoja alimaliza Chuo mkoa mmoja wa Kaskazini mwa Tanzania, akaomba kazi katika Idara
yetu. Siku ya usaili nikamweleza ataje vitabu vitano alivyosoma katika fani
yetu! Lakini cha kushangaza alishindwa kabisa. Nikamkumbusha tafiti za Walter Rodney, akasema anafahamu. Huwezi
amini nilimhoji tena, nikauliza What is the main thesis of the book? Akashindwa kujibu, nikabaki
kushangaa tu, nikajiuliza hivi hii elimu ikoje ambapo mtu ana matokeo mazuri
lakini uwezo wake ni mbovu? Nikamuuliza kwa Kiswahili swali jingine, ‘Paradigm'
gani ambayo Walter Rodney ameandika? Cha ajabu
akashindwa kujibu. Sikuchoka, maana nilitaka afahamu umuhimu wa kuielewa fani yake
sio matokeo yake kwenye vyeti tu, nikamuuliza kitabu gani anakipenda sana na kinamvutia? Hakika alishindwa kujibu, ina
maana hakuwa akisoma kitabu chochote, huku akijivunia matokeo mazuri kwenye
vyeti vyake. Msomi huyo alikuwa GPA ya 4.6.” anasema Zotto.
“Leo
hii serikali inafuta matokeo na kuwadekeza wanafunzi wavivu na wazembe kama
hawa. Wahitimu Wwengi
laiti kama wangekutana na usaili Upya kabla hata ya kuonesha GPA zao,
lazima wanataalamu tuone fedheha sana. Sisi wakati tunasoma tulikuwa tunataabikia
katafuta shahada zetu, hawa wanafunzi wa siku hizi wanacheza sana ten asana, na
hayo yaanzia huko chini ambako leo wanadekezwa na serikali nzima. Wanafunzi wa
siku hizi wanapewa swali halafu wanamfuata mwalimu ofisini kuuliza, hivi hili
swlai lina maana gani? Hawa wanafunzi wanauliza hivi wakati vitabu vipo lakini
wanaona tabu sana, unadhani kusahihisha upya matokeo kutashindwa kuwadekeza?,
anasisitiza Zotto.
Anaongeza
kuwa, “Iko wapi Lambart, ambacho ni mkate wa somo la Jiografia, Kozlov, Wadada
na Budere, na Walter Rodney? Sisi tulisoma haya yote tukiwa kidato cha tano na
sita na tulipoyaona Chuo hatukushangaa. Tuliweza kutoa mifano na kuthibitisha
hoja mbalimbali, ndipo tukaanza kukariri kurasa hadi kurasa eti leo wanafundisha
wanafunzi majibu na maswali, ndio vitabu vyao vya leo. Uwezo wa kufikiri kwa
kupambanua (Analytical thinking) umepungua sana,”
Alipotakiwa
kueleza ni kwanini anadhani kuna tatizo la kupungua kwa uwezo, akasema, “Nimesama
hayo kwakuwa nimejiuliza kwanini miaka ya hivi karibuni watu wamemaliza shahada
na wanarudi kuunganisha shahada ya pili. Wengne hata kazi hawataki, nikajiuliza,
je, ni hamu ya kuongeza elimu tu? Kazi ni shida? Ushindani mkubwa au kupanda
madaraja kirahisi? Nikagundua kuwa elimu yetu haijajitoleleza vizuri kutatua
matatizo. Je, hizo shahada za pili zimesaidia kutatua kama haya ya matokeo ya
wadogo na watoto wetu huko sekondari? Hapo jibu ni hapana,” anasema James
Zotto.
“Tumepoteza, the
purpose of education, ambayo Mwalimu Nyerere alituachia. Binafsi nilijiona
nimekamilika baada ya kumaliza kidato cha sita kuliko hata nilipomaliza Chuo
Kikuu, tuliandaliwa kujitegemea kujenga hoja na kufanya kazi, lakini sasa naona
kabisa kuna ombwe kubwa,” anasema Zotto
Anaongeza
kuwa, “Mwalimu Nyerere alitaka elimu yetu iwe imekamilika kila hatua na kila
hatua imsaidie mhitimu atatue matatizo
yake na ya jamii. Je, darasa la Saba la leo, Kidato cha Nne, cha Sita, Cheti, Stashahada
vinajitosheleza? Nafikiri tutasoma hata Uzamivu na itakuwa bado. Itabidi
tutafute elimu kubwa zaidi ya Uzamivu huenda ikatosha. Tujikague.”
“Labda
nikuulize swali la kizushi, ungesikia Dk Ndalichako katangaza daraja la kwanza
wamepata wanafunzi asilimia 80 na sifuri hakuna, kisha wengine wamepata asilimia
20 wapo katika, je ungempongeza Dk Ndalichako? Lazima niwe mkweli katika hili
la kufutwa mitihani kwa vile wanafunzi hawa wa siku hizi nawafahamu, pia
nafahamu kuwa Dk. Ndalichako ni mtu kati ya wachache wanaoheshimu taaluma zao, waliposema walikubaliana wapitishe
matokeo na NECTA ikatoa sahabu zake, mbina hatuambiwi waliyokubaliana ni yepi?
Je, ina maana kuna matokeo ya makubaliano na yaliyotolewa na NECTA? Ndugu yangu
tuna matatizo kwenye familia na uendeshaji wa elimu, siasa imeingia na dini
pia. Halafu wanafunzi wenyewe hawa wavivu na wazembe tutarajie nini kama kila
siku wanamfuata Mwalimu ofisini kuuliza maana ya swali wakati vitabu vipo?”
ansema Zotto.
Mimi hapa najiuliza, kosa ni la nani, ni nani kasabaisha hadi ifikie hapo, `mwanafunzi kuwa mzembe'...tuliangalia hilo kwa undani zaidi, maana huyo mtoto amekuwa mikononi mwa walimu, miaka saba ya primary, na miine ya sekondari,....hatimaye kwenye mtihani huyo mtoto anafanya hayo yaliyofanyika.
ReplyDeleteTunahitajika kuangalia matokea haya, kwa mbali zaidi,....najiuliza, mzazi na mwalimu walikuwa wakishirikiana vipi hadi huyu mtoto akafikia hapo, kama mtoto anatoka nyumbani saa kumi alifajiri, anafika kwenye daladla, anafukuzwa, mpaka apate usafiri, ni saa tatu, anafika shuleni kachoka....haya hatuyaangalii.
Haya anafika shuleni, mwalimu anapiga miayo ya njaa, hajui familia yake itakula nin, bado anatakiwa kuwasomesha hawa watoto, waelewe, na bado haruhusiwi hata kumchapa huyu mtoto mkorofi...
Hakuna vitabu, ...makampuni mazuri yanajulikana dunia, yamefungiwa, mavitabu yanaharibia kwenye magodown, watu wanaangalia, maslahi yao tu....kweli mitihani ndiyo tunaitizama kama kigezo cha `uzembe ' wa huyu mwanafunzi?
Mimi nahisi `uzembe' huu uwe ujumbe wa kuchimbua zaidi, tuangalia mizizi ya tatizo hili,....tusipozina ufa ....
Mkuu nimeandika ujumbe huu kwa haraka, naona makosa yapo mengi...si unajua tena kubana matumizi!
Delete