Na Pete Mhunzi, Marekani
Salaam zenu. Mimi kwa jina
ninaitwa Pete M. Mhunzi, Mmarekani, Mswahili wa buku. Nilisoma makala yako
kuhusu wanasiasa wakiwa pamoja na wajasiriasiasa. Kweli umenena lenye busara
kubainisha hulka za viongozi wengi dunia nzima. Nakushukuru.
Madhumuni ya barua hii zaidi ya
kupongeza ni kusema machache juu ya neno "jimbo" haswa linalotafsiriwa
kwa Kiingereza. Ulimtaja Rais wetu
Barrack Obama katika makala yako kuhusu CUF na kushindwa kwake huko mkoani
Tabora. Ulitaja mji wa Honolulu lakini haupo katika Chicago kwa sababu Chicago
pia ni mji.
Honolulu ni mji uliopo kwenye
kimojawapo cha visiwa vya Hawaii. Visiwa
hivyo vyote vinatambulika "jimbo".
Chicago ni mji uliopo bara katika jimbo la Illinois.
Kuna majimbo hamsini katika
taifa la Marekani kila moja likiwa na gavana.
Chini ya rais ambaye ana wadhifa ya taifa zima gavana anaongoza serikali
ya jimbo ambamo alichaguliwa katika upigaji kura.
Nimeongea kwa upana na urefu
juu ya neno hilo "jimbo" pamoja na diwani wa kata ya kati, huko
Arusha naye ni mjomba wa mke wangu, kwa jina anaitwa Abdulrasul Tojo. Tukagundua maana ya "jimbo" katika
mfumo wa siasa za Tanzania ni tofauti
sana na maana ya "state" katika mfumo wa siasa za Marekani, yaani
taifa la Marekani kwa vile kuna mabara mawili yanayoitwa Marekani.
Tukipima maana kwa ukubwa wa
eneo la ardhi la taifa, jimbo hufuata taifa zima halafu ndani ya jimbo kuna
"county" ama "province" (jimbo la Louisiana peke
yake).
Halafu miji ambayo huongozwa na
meya anayechaguliwa katika upigaji kura. Bado sielewi vizuri maana ya
"jimbo" katika mfumo wa siasa Tanzania! Nitatia nanga barua hii kwa kushukuru tena
mawazo yako ambayo yamenichemshia bongo isitoshe kuridhisha kiu changu cha
Kiswahili fasaha. Asante, asante sana.
Wakatabahu,
Pete M. Mhunzi
Retired Professor of History
petemhunzi@gmail.com
No comments:
Post a Comment
Maoni yako