NA MARKUS MPANGALA
TUMESHUHUDIA bunge letu likigeuzwa sehemu ya kufanya mizaha isiyokwisha, kana kwamba wanehshimiwa wamekwenda pale kupiga ulabu na kadhalika. Staha ya kibunge inaelekea kutokeweka sababu hata kauli ya Mheshimiwa Ezekiel Wenje dhidi ya chama chenye mifumo na kuunga mkono Uliberali, ikidhaniwa alikilenga chama cha CUF haikuwa na staha.
TUMESHUHUDIA bunge letu likigeuzwa sehemu ya kufanya mizaha isiyokwisha, kana kwamba wanehshimiwa wamekwenda pale kupiga ulabu na kadhalika. Staha ya kibunge inaelekea kutokeweka sababu hata kauli ya Mheshimiwa Ezekiel Wenje dhidi ya chama chenye mifumo na kuunga mkono Uliberali, ikidhaniwa alikilenga chama cha CUF haikuwa na staha.
Tunapojadili masuala ya taifa
tunalazimika kuweka kando mzaha wowote ambao unasababisha tuonekana tuna wazimu
fulani. Sote tunaunga mkono mabadiliko katika nchi yetu.
Ukumbi wa Bunge letu |
Sote tunamhimiza Rais Kikwete
afanye juhudi kutekeleza ahadi zake ikiwemo kununua Meli katika Ziwa Nyasa
ambayo ni muhimu kumkumbusha. Sote tunafahamu kuwa ili tuweze kuyafikia
maendeleo lazima tuchukue hatua za msingi.
Kama Mbunge anayo hoja ya
msingi kuhusiana na chama fulani na inalenga kuwakumbusha wabunge na viongozi
wa chama husika kwamba mwenendo wao haupaswi kuigwa sababu unahatarisha ama
unasababisha hatari katika taifa.
Lakini kama Mbunge anakuja na
maelezo kuwa chama fulani kinafadhiliwa na chama fulani cha nje na ambacho
kinaunga mkono ushoga au usagaji, sidhani kama linaleta mantiki kwa wananchi.
Mbunge anapotamka maneno kama
hayo kisha Bunge zima linaahirishwa hakika huku ni kuchezea akili za
watanzania. Bunge linatumia gharama kubwa.
Tanesco inamwaga umeme bungeni.
Kuna wataalamu wanalipwa posho. Wabunge wanalipwa posho. Mafundi mitambo
wnaalipwa posho. Watumishi na wasaidizi mbalimbali wamepiga kambi yao Bungeni
katika kuhakikisha gurudumu la maendeleo ya taifa hili yanakwenda sawa.
Lakini hakuna kinachotia kinyaa
kama ile Bunge linaahirishwa kwa sababu za kitoto kabisa mbunge kuleta utoto. Hatukati
kwuapa changamoto washindani wako lakini jambo kubwa zaidi katika Bunge ni
majadiliano yenye kufuata taratibu husika.
Kama mbunge anaona hatendewi
haki taratibu zipo na tunazieleza hizo kwa wananchi ili wajue kinachoendelea
katika bunge letu sio vinginevyo.
Haiwezekani pesa za watanzania
zikatumia kuwafanya wabunge waketi na kuzungumzia mizaha kwamba mfadhili wa
chama fulani anahusudu mashoga ama la.
Jambo hili linaleta fadhaa
kubwa miongoni mwetu kwani halina maslahi yoyote kwa wananchi. Tatizo kubwa la
wanasiasa wanatuchukulia sisi wananchi kama watoto tusiweza kufanya tafakuri
jadidi.
Kila siku bunge letu linakuja
na taswira kanganyishi. Tunakubaliana kwamba yapo malumbano ya hoja na yenye
kulinda maslahi ya nchi.
Lakini kama lililotokea siku
chache zilizopita hadi Bunge kuahirishwa na mheshimiwa Naibu Spika, Job Ndugai,
hakika linakasirisha.
Inaelekea siku hizi ili uwe
mwanasiasa makini na hodari lazima uwe na hasira, kejeli, na ubabe fulani kama
akina Mohamed Ali ulingoni.
Bahati mbaya, badala ha
kujijengea ubabe wa kifikra na hoja tumejigeuza kuwa wababe wa maneno ambayo
yanalipiwa posho na hayana msaada wowote kwa taifa hili.
Tumeruhusu bunge letu liwe na
maneno yanayolipiwa posho wakati hayana msaada wowote kwa wananchi wanaopata
shida huko mitaani.
Tumeruhusu kukanganyana ndani
ya Bunge kwa sababu ya kulinda na kujigamba wka vyama vyetu kisha tunasahau
hivyo vyama pasipo kura za wananchi tusingelifika hapo.
Wananchi wanakaa na kuangalia
Bunge kwa kiwango cha juu sana. Wanasikia maneno yanayotolewa na waheshimiwa
Wabunge.Mjadala unapokuwa na mantiki
huku wabunge wakijadili masuala nyeti ya taifa bila shaka wananchi watawaunga
mkono zaidi na kuonyesha mapenzi yao kwa wawakilishi.
Wananchi watafurahia na kuamini
kuwa posho wanazolipwa wbaunge na watendaji mbalimbali walioko bunge zinafanya
kazi ipasavyo.Lakini tukiendelea kuruhusu
uchafuzi huu ufanyike ndani ya bunge huku kura zetu ndio zimewapa mamlaka ya
kutoa maneno yasiyo na staha mbele ya wageni pamwe na weenyeji hakuna shaka ni
aina fulani ya ukosefu wa heshima kwa wananchi.
Bunge ni sehemu ya kuisaidia
serikali na kuikumbusha namna ya kuendenda mambo ya msingi. Tumekuwa tukilalamika
wkamba serikali inafanya uzembe kwenye suala la sheria za gesi na mafuta,
lakini badala ya kuikumbusha na kuchambua mambo nyeti tumebaki kuelezeana
habari za mashoga na wasagaji ama vyama vya kiliberali vinavyosaidiwa na
waungaji ama wanaohimiza ndoa za jinsi moja.
Fedha za taifa zinateketezwa na
bunge linaahirishwa. Posho inaingia mfukoni mwa mbunge wakati hana lolote la
maana alilosema. Ni uchovu wa kufikiri kudhani kukishambulia chama fulani na
kuchungulia udhaifu wao ni moja ya demokrasia nzuri kuliko, lakini ikigeuzwa
kwako inakuwa nongwa.
Lazima tukatae siasa za namna
hii. Lazima tukemee matumizi mabovu ya fedha zetu kwenye Bunge ambapo mbunge
analipwa posho lakini anazungumza mambo yasiyoleta changamoto. Bunge sio kijiwe cha kahawa ama
kaya moja inayopiga soga baada ya kushiba. Ni uzandiki kuvumilia shughuli za
Bunge zinaahirishwa kwa sababu za kipuuzi. Ni ukosefu wa adabu kwa Wabunge
kudhani wnaanchi tumekuwa watu tusielewa kinachoendelea.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako