TANZANIA:
Tumeelekeza
nguvu na akili zetu kwenye uchaguzi mkuu 2015.
Mpaka sasa hatuna mwafaka wa
uchaguzi huo kwamba tutumie Katiba ipi, ya zamani ama hii iliyoko kwenye hatua
ya Rasimu itakapokamilika.
Tukumbuke wanachama wa shirikisho la Muungano;
Zanzibar na Tanganyika watahitaji kutunga Katiba zao. Zanzibar wanayo Katiba
yao, je watakubali kutunga katiba mpya?
Je, mwanachama mwingine Tanganyika
atakubali kuwa yeye ni Tanzania Bara halafu kwa wakati huo huo akiwa mwanachama
wa shirikisho akatumia Katiba ya Tanganyika?
Ni Tanganyika ama Tanzania Bara?
Kama wewe unasoma RASIMU YA KATIBA, hakika kuna mengi unapaswa kuyatafakari kwa
maslahi ya nchi.
Nadhani tuitishe uchaguzi mkuu mwaka 2017, tujipange kwa
kuwekeza kwenye MUDA kukamilisha zoezi hili, sio jepesi hili, halihitaji 'fasta
fasta'.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako