Timu ya Taifa, imeondolewa kwenye kinyang’anyiro cha michuano ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia nchini Brazil mwakani baada ya kufungwa mabao 4-2 katika dimba la Taifa, jijini Dar es salaam. Wakati Stars ikipoteza nafasi hiyo, timu jirani za Uganda na Ethiopia zinakaribia kufuzu katika hatua ya mtoano ambayo itajumuisha timu kumi.
Katika kundi C, Stars
inashika nafasi ya tatu kwa kujikusanyia pointi 7, huku Morocco ikiwa nafasi ya
pili ikwia na pointi 8. Ethiopia na Uganda zipo
kwenye nafasi nzuri kufuzu kwa hatua ya mtoano ambayo itafanikiwa kutoa timu
tano zitakazofuzu michuano ya Kombe la dunia.
Iwapo mambo
hayatabadilika kwa Ethiopia basi itakuwa imepiga hatua kubwa sana katika
michuano hiyo. Ethiopia imeingia matatani baada ya shirikisho la soka duniani (FIFA)
kuanzisha uchunguzi dhidi yake kwa tuhuma za kumpanga mchezaji asiyeruhusiwa.
Ethiopia ambayo
iliichapa Afrika Kusini mabao 2-1 wiki iliyopita katika pambano la kuwania
kufuzu inachunguzwa na Kamati ya Maadili ya FIFA, huku ikiwa imebakiza mchezo
mmoja katika kundi lake.
Ethiopia inachunguzwa
kutokana na mechi yake dhidi ya Botswana
iliyofanyika Juni 8 mwaka huu. FIFA pia
inazichunguza Togo kwa kosa la kumchezesha mchezaji asiyeruhusiwa kwenye mechi
yake ya Juni 9 mwaka huu.
Nayo Guinea ya Ikweta
inakabiliwa na adhabu kutokana na kosa kama hilo kwenye mechi yake dhidi ya
Cape Verde iliyofanyika Machi 24.
Naam, tukirejea pambano
la Stars na Ivory Coast tuliona tofauti fulani kati ya wachezaji wetu na wale
wa Ivory Coast. Stars ilijaribu kulitia msukosuko lango la Ivory Coast na kwa
hakika kikosi cha Kim Poulsen kinastahili pongezi kwa juhudi zao.
Hata hivyo kueondolewa
kwenye kinyang’anyiro hicho sio mwisho wa mashindano. Stars inakabiliwa na
mashindano ya CHAN ambayo yatafanyika nchini Morocco mwaka huu, hivyo pambano
letu dhidi ya Gambia nalo lina umuhimu mkubwa kama tulivyoanza mechi zingine za
Kundi C.
Michuano ya CHAN
inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani itakwua fursa nyingine ya
kuweza kujipa uzoefu wa mashindano ya kimataifa. Katika michuano hii
Stars italazimika kuongeza wachezaji wengine, badala ya Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengi wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo(DRC).
Mashindano ya CHAN yana
umuhimu mkubwa sababu yanafanikisha kuibua vipaji vipya vya soka. Tulishiriki
mashindano hayo nchini Sudan tulipokuwa chini ya Marcio Maximo, na tulionyesha
kila aina ya ujuzi mashindanoni.
Kim Poulsen ameonyesha
mwelekeo wake katika kukijenga kikosi cha Stars, na uhakika wa kuwa washiriki
wazuri wa CHAN ni mkubwa mno. Hebu tujikumbushe ni
kitu gani kilichotokea kwenye pambano letu dhidi ya Ivory Coast. Stars
ilifungwa bao la kwanza na Ivory Coast kwa sababu kubwa moja tu, kuzubaa.
Wakati safu ya ulinzi
ikianza kuekelea mbele huku tukitegemea kucheza ‘offside’, Yaya Toure aliingia
eneo la hatari haraka sana na kuvunja mtego wa kuotea.
Bao la nne la Ivory
Coast ni somo jingine kwetu. Wakati tukiwa tumeshampoteza Shomari Kapombe,
Kocha Kim Poulsen alijua hakuna sababu ya kujilinda, akamwingiza kiungo
mshambuliaji, kisha safu ya ulinzi ikabadilika na kucheza mabeki watatu.
Hii ilikuwa na maana
Erasto Nyoni alitakiwa kwenda kushoto, kisha Nadir Haroub na Kevin Yondani
wakigawana majukumu ya ulinzi. Cannavaro akilinda
kutoka eneo lake kwenda kulia huku Yondani akilinda kuelekea katiti hali ambayo
ilimfanya Frank Domayo arudi eneo hilo mara kwa mara kusaidia ulinzi katika
3-4-2-1.
Kwa mfumo wa mabeki
watatu ulikuwa mzuri, na Ivory Coast walituzidi jambo moja, uzoefu katika mbinu
husika. Walifahamu kuwa watacheza mashambilizi ya kushtukiza, na hilo
lilionekana tangu mwanzo wa kipindi cha pili.
Bila shaka Kocha wao
Sabri Lamouchi alifahamu ukali wa Stars.Wachezaji wote Stars walipigania
ushindi, walitaka timu yetu iibuke na pointi tatu, lakini mambo hayakwenda vile
ilivyotakiwa na tumeshidnwa kwenda Brazil. Kwa sasa hatuna sababu
ya kuendelea kulia machozi, bali ni kuangalia mashindano ya CHAN. Na huo ndio
mpango mzima.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako