September 30, 2014

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI BAADA YA SIKU 14.

*JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*
*WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI*
*TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI*

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anatangaza nafasi za
kazi zifuatazo katika Idara ya Uhamiaji kwa Raia wote wa Tanzania wenye
sifa.
*1. KOPLO WA UHAMIAJI Nafasi 114 - (Nafasi 100 kwa ajili ya Tanzania*
*Bara na Zanzibar na nafasi 14 maalum kwa ajili ya Zanzibar tu)*
A. SIFA ZA MWOMBAJI:
(i) Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 25 hadi 30.
(ii) Awe amehitimu kidato cha sita na kufaulu masomo ya Kiingereza,
Kiswahili, Historia, Jiografia, Kifaransa, Hisabati ambapo masomo mawili kati ya hayo yawe katika kiwango cha Principal 2.
(iii) Awe pia na mojawapo ya sifa zifuatazo:
Cheti cha Sheria;
Cheti cha Kompyuta;
Cheti cha Ufundi (FTC) kwenye fani ya umeme na mitambo
(iv) Waombaji wenye ujuzi wa mojawapo ya lugha zifuatazo (Kifaransa,
Kichina, Kijerumani, Kiarabu au Kihispania) watafikiriwa kwanza.
(v) Aidha, Mwombaji aliyepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa atapewa
kipaumbele.
B. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kusimamia upangaji wa majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji;
(ii) Kusimamia ufunguaji wa majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji
pamoja na majalada binafsi ya watumishi wa uhamiaji;
(iii) Kuandika hati mbalimbali za uhamiaji;
(iv) Kuwa viongozi wasaidizi wa makundi ya doria na ukaguzi;
(v) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za uhamiaji mahakamani pamoja na
wageni wanaofukuzwa nchini (Deportees)
4. ANUANI YA KUWASILISHA MAOMBI
Barua za maombi ya kazi ziwasilishwe kwa njia ya posta ndani ya kipindi
cha siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili kwa anuani zifuatazo:-
ΓÇó Waombaji wa nafasi 200 (100 Koplo na 100 Konstebo) ambazo ni kwa ajili
ya Tanzania Bara na Zanzibar wawasilishe maombi yao
kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM.
ΓÇó Waombaji wa nafasi 28 (14 Koplo na 14 Konstebo) ambazo ni maalum kwa Zanzibar wawasilishe maombi yao kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
C/O Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
S.L.P 1354,
ZANZIBAR.
Maombi ambayo hayatazingatia maelekezo tajwa hapo juu hayatashughulikiwa.
CHANZO: DAILY NEWS LA TAREHE 29 SEPTEMBA 2014

No comments:

Post a Comment

Maoni yako