NA DOKTA PAULO MATEMU
1. Mimba kutoka ( miscarriage ) ni ile hali ya mimba kutoka
bila RUHUSA YA mjamzito. yaani mjamzito anataka mtoto lakini mimba inatoka
Sababu za mimba kutoka ( miscarriage ).
2. Mji wa uzazi kushindwa kuhimili mimba, kawaida shingo ya
uzazi hufunga kabisa kipindi cha ujauzito mpaka uchungu wa kujifungua unapoanza
ndio hufunguka kuruhusu mtoto apite.
Ikitokea misuli ya shingo ya uzazi kushindwa kukaza ipasavyo
mimba hutoka. Hii yaweza kutokana na matibabu mbalimbali eneo hilo, au kuumizwa
kutokana na vitu vinavyoweza kuingia. Ikigundulika mapema... Daktari anaweza kuifunga ( operation
ndogo ) na akaja kuifungua muda wa kujifungua. Mjamzito atahitaji uangalizi wa
karibu wa dokta.
3. MATATIZO YA KISAIKOLOJIA...
Hii nilishasimulia sana, mwanamke akiwa na stress mimba
inaweza kutoka japokuwa hana tatizo lingine lolote lile.
Matibabu... Waume wawapende wake wao, na wajawazito
wasijistress kwa mambo ambayo sio bora kuliko mimba waliyo nayo.
4. MATATIZO YA KIJENETIC
Mtoto hutungwa kwa kuchukua vijinasaba 23 vya mama na 23
vya kutoka kwa Baba. Ikitokea tatizo ktk vijinasaba hivo matokeo huwa ni kwa
mtoto, na baadhi ya matatizo husababisha mimba itoke.
Mara nyingi hakuna matibabu ya hii.
5. Mimba kutunga nje ya mji wa uzazi. Kawaida yai
likisharutubishwa husafiri kwa siku 5 na kujipachika kwenye ukuta wa mji wa
uzazi... Ikitokea mimba ikajisahau na kujipachika sehemu ingine, haitakua na
hutoka.
6. Mimba kutungwa bila kukamilika. Hii ni mimba ambayo
haina vijinasaba vyote, hii haitakuwa na kutengeza mtoto... Hivyo hujikuta
inatoka.
Nb mimba hizi zikikua ndio wanapatikana watoto wasio na
viungo au watoto "wa ajabu"
USHAURI... Hapo sio kosa la baba au mama, ni asili tuu.
Nchi za wenzetu mimba huangaliwa kwa Ultra Sound mara 3 (
lazima ) kama ikionekana mimba ina shida Daktari humweleza mjamzito na mimba
hutolewa.
7. Matatizo yatokanayo na uvutaji sigara, kunywa pombe,
madawa ya kulevya, machemikali makali, mionzi etc hii huathiri mimba na ukuaji
wake, na hatimaye inatoka...
8. Matatizo ya homones... Kikawaida mimba inakua kwa
kusimamiwa na homones, ikitokea homones zikawa na shida mimba haikui na hutoka.
Hapa ndio tunawaomba wadada wasitumie machemikali ya ajabu ajabu kama mercury,
benzene, cadnium, formaldehyde etc hizi nyingi zipo kwenye vipodozi
vilivyopigwa marufuku . Magonjwa yahusuyo homones yanatika.
9. Magonjwa ( kisukari, presha, stress na ya zinaa )
Nb mama akitibiwa na mme atibiwe hasa ya zinaa.
TAFADHALI fahamu kwamba mimba inaweza ikamletea mwanadada
kisukari au presha wakati wa mimba na akijifungua vyote vinaisha. Magonjwa
niliyojadili hapo ni yale ambayo alikuwa nayo msichana kabla ya mimba
10. Uvimbe ( fibroids ) hizi ni uvimbe tuu zinazokua maeneo
ya mji wa uzazi.
Share ili umsaidie mtu kuzuia mimba kutoka.
#Thinking_loud
©Paulo Matemu
No comments:
Post a Comment
Maoni yako