Copenhagen, Denmark.
Chuo kikuu cha Copenhagen nchini Denmark kimeanza rasmi somo jipya ambalo linazungumzia maisha ya mwanamuziki Beyonce. Kwa mantiki hiyo utahitaji kusoma shahada ya kwanza pengine hadi shahada ya uzamili na udakitari wa falsafa katika maisha ya mwanuziki huyo.
Hii ni kama vile nchini Tanzania kungekuwepo na somo rasmi vyuoni ambalo linazungumzia maisha ya mwanamuziki pengine Diamond, Ali Kiba, Shilole, Harmorapa, Chid Benz, Fid Q, Mrisho Mpoto (Mjomba), TID, Lady JD, Harmonize, Dogo Janja, Mwana FA, Roma, Mr. Blue, GK, Juma Nature, Rich Mavoko, na wengineo. Huu ni mfano tu nchini mwetu.
Ni kama vile nchini Kenye kungekuwepo na somo rasmi vyuoni linalozungumzia maisha ya mchekeshaji Eric Omond. Au kama Nigeria ingelikuwapo hivyo kwa Davido, au Uganda kwaajili ya Jose Chameleon.
Ndivyo ilivyo huko Denmark.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako