September 15, 2017

SHAIRI: MREMBO


NA KIZITO MPANGALA

Wako wapi wanaume,
Mrembo wamchukue,
Kipimoni jipimie,
Ni mrembo alo bora.
Wako wapi wanaume,
Mrembo mparamie,
Kwa uloho na makeke,
Kwake yeye mjigambe.
Ninakutanieni tu,
Mrembo ninaye huku,
Analindwa kwa mtutu,
Mtimani kaningiya.
Omuhimba ndio yeye,
Utazame urembowe,
Ovahimba waheshimiwe,
Warembo walotukuka.
Mchaga sio mchaga,
Pengine awe Muhaya,
Mndendeule hapana,
Pengine awe Mnyasa.
Mrembo ananichosha,
Wala siyo Msukuma,
Sio Mnyaturu bwana,
Omuhimba atakuwa.
Sizingatii kabila,
Hata kama Mnyakyusa,
Nitamfata Mwanjelwa,
Mrembo alotukuka.
Mrembo wangu jamani,
Kumuacha sitamani,
Niachieni jamani,
Mrembo wangu mekoni.

© Kizito Mpangala

No comments:

Post a Comment

Maoni yako