WEWE ni mtanzania umefundishwa mambo
mengi kutoka kwa wazazi,walezi na walimu wako. Jitahidi kuyakumbuka
unayofundishwa na uyalete katika maisha ya kila Siku. Wale waliokufundisha mambo mbalimbali walikupa
msingi wa jengo tu. Sasa ni jukumu lako kumaliza nyumba, paa na sakafu. Tumia
akili yako kuyaendeleza uliyofundishwa na jamii yako na darasani.
Elimu yetu lazima iwe halisi na yenye kugusa hisia, tukifanya hivo tutafika kule tunakotaka kufika, lakini kwa elimu hii ya kukariri na umombo sioni kama ni kwa namna gani tutafika huko. Tunajichelewesha wenyewe kwa kuendekeza na kuaminishana kuwa ili uwe msomi mzuri lazima ujue kimombo.
Ni wakati wa kuamua Kiswahili kitumike katika ngazi zote za elimu kama lugha ya kufundishia kama kweli tunahitaji wataalamu wanao endana na elimu zilizo andikwa kwenye vyeti. #1820.
©Nishani MEDIA
Songea,
Juni 21, 2017
No comments:
Post a Comment
Maoni yako