SERIKALI IMEKATA RUFAA KATIKA KESI ILIYOSHINDWA YA UMRI WA MTOTO WA KIKE KUOELEWA
DAR:
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali imekata rufaa kesi iliyoshindwa mwaka Jana Baada ya Rebecca Gyumi
Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative kufungua kesi ya Kupinga Ndoa za
umri mdogo.
Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inaruhusu mtoto wa kike
kuelewa akiwa na miaka 14. Rebecca Gyumi alifungua kesi hiyo Mwaka Jana kupiga
sheria hii Kandamizi dhidi ya watoto wa kike
walio chini ya umri wa miaka 18 kuolewa kwani wanakosa fursa ya kupata elimu
Mwaka jana Mahakama Kuu ilitoa amri Kwamba Serikali
ipeleke mswaada Bungeni kuondoa sheria hiyo, Kinyume chake Serikali imefungua
rufaa kupinga Uamuzi huo ikitaka sheria hiyo iendelee kuwepo ili watoto wenye
umri chini ya miaka 18 waolewe kama wenye zaidi ya miaka 18
Ndimi,
Ndahani N. Mwenda
No comments:
Post a Comment
Maoni yako