September 21, 2017

UCHAGUZI WA KENYA SASA KUFANYIKA OKTOBA 26



NAIROBI, KENYA
 Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya imetangaza tarehe 26 Oktoba kuwa siku ya uchaguzi mpya wa urais nchini humo. Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika  Oktoba 17 mwaka huu ikiwa ni siku chache baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya urais kutokana na kukubaliana na pingamizi la Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, NASA. 


Mahakama ilikubali kuwa uchaguzi huo ulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni. Majaji wanne kati ya 6 walipiga kura ya kuamua uchaguzi urudiwe, huku majaji wawili wakisema uchaguzi usirudiwe. Kutangazwa kwa tarehe mpya kutamaliza malumbano ya wiki kadhaa kati ya chama cha Jubilee na Muungano wa NASA wakiongozwa na Raila Odinga. Tarehe ya uchaguzi mpya imetangazwa hivi leo na Mwenyekiti wa Tume hiyo, IEBC Wafula Chekubati.


No comments:

Post a Comment

Maoni yako