NA HONORIUS MPANGALA
+255628994409
KATIKA makuzi ya kila mtoto katika familia,kitu
cha kwanza ambacho mtoto ataiga ni yale matendo ya mama au baba. Wako watoto
ambao wanajifunza hata kwa kificho kuvuta sigara kama mzazi wake anavuta na
anamwona avutapo. Huku kunaitwa kujifunza kwa kuona katika makuzi ya
mtoto baada ya kuzaliwa kama inavyoelezwa na wanasaikolojia wa masuala ya elimu
ya awali kama muitaliano Maria Montessori.
Himid licha ya kuwa ninja kama aitwavyo lakini
akiwa ninja nje ya filamu. Yeye ni kijana wa kizazi cha soka kakua na kujifunza
kwa kuona kama ilivyo nyanja za ujifunzaji wa watoto akamwona baba Mao mkami
akipendelea mpira nyakati zote. Mazingira hayo mtoto hakwepi kuiga anachofanya
mzazi. Katika soka lake Himid amekuwa kiraka kwa kutumika katika nafasi nyingi
uwanjani. Hii ni aina ya watu wanaopenda kujifunza Mara kwa Mara na kujaribu
Mara kwa Mara.
Mwandishi wa makala haya akiwa na nahodha wa Azam FC, Himid Mao katika viwanja vya Jakaya Kikwete, Jijini Dar es salaam.
Awali nilimwona akiwa kama kiungo mkabaji katika
timu za vijana. Lakini akaja kucheza nafasi zote za beki hasa kulia na kushoto
pamoja na kiungo mchezeshaji na kiungo wa pembeni pia. Akiwa kama kijana aliyepita katika njia stahiki ya
vituo vya kulelea watoto yaani Academy. Huko ndiko unakopata mafunzo mengi
yanayohusu soka ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Mchezaji utawezaje kuishi
katika jamii inayokuzunguka.
Licha ya kuwa na jina la utani la kibedui huyu
bwana ni kama kiongozi aliyeandaliwa tangu angali chini ya miaka 17. Hivyo hata
Uninja wake humfanya apunguze makeke akiwa kama kiongozi awapo uwanjani. Himid kapita katika ngazi tofauti za uongozi kwa
wachezaji wenzake. Mwaka 2008 alikuwa nahodha wa Serengeti Boys timu ya taifa
ya chini ya miaka kumi na saba.
Mwaka 2009 akawa nahodha wa Ngorongoro Heroes timu
ya taifa chini ya miaka ishirini licha ya kuzidiwa umri na baadhi ya wenzake
lakini alipewa unahodha. Haikuishia hapo katika msimu wa ligi kuu 2011/12
Azam fc wakaamua kumpa unahodha msaidizi nafasi aliyoitumikia chini ya Ibrahim
Shikanda na John Raphael Bocco.
Katika msimu wa 2017/18 Himidi anakuwa
Nahodha mkuu wa Azam akipokea majukumu toka kwa swahiba wake aliyetimukia Klabu
ya Simba. Katika timu ya taifa Kocha Salumu Mayanga aliona
Mchezaji huyo awe msaidizi wa Mbwana Ally Samatta.
Himid ni kiongozi aliyepita katika ngazi zote za
kiuongozi. Wakati wakiwa Ngorongoro, Mbwana alikuwa chini ya Himid na sasa
Himid yuko chini ya Mbwana. Unaweza kusema kuimba kupokezana lakini katika soka
hakuna jambo geni katika masuala ya utawala na uongozi. Kuna wakati ambapo namwona kabisa Ninja akitamani
kuonyesha uhalisia wa jina hilo ila 'usinga' unamfanya awe mpole zaidi.
Katika kumbukumbu zangu hakuna kazi chafu ambazo
nazikumbuka kama zile Tanzania dhidi ya Malawi nyumbani na ugenini.Katika dimba la Chichiri pale Malawi mwaka 2015
pamoja na Tanzania dhidi Algeria nyumbani na ugenini mechi zote hizo akiwa na
Mwenzake Mudathir Yahya.
Miongoni mwa muunganiko ambao kila mwanafamilia ya
soka akikumbuka kiungo cha Himid na Mudathir anatikisa kichwa kwani kilitoweka
kama kiungo cha Frank Domayo na Sureboy Salum Aboubakari. Mbuyu Twite anamkumbuka kwa mengi kila
walipokutana eneo la kati ilikuwa Mzee mzima lazima apate huruma wa mwamuzi.
Anacheza soka lote liwe la shoka au la kiungwana 'aste aste au nainai'.
Makuzi ya kiuongozi yanamfanya Ninja awe na maneno
mazuri na yenye staha kama anahojiwa na waandishi kuzungumzia mchezo aliocheza.
Ni manahodha wachache sana wanaoweza kuongea mbele ya kamera.Kwa bahati Ninja ameishi na kuona kupitia wengi
kama ilivyo Nahodha wa zamani wa Tanzania na wa sasa wa Yanga Nadir Haroub Ally
'Cannavaro' wanautulivu mkubwa mbele ya kamera.
Wakati haya ya kiuongozi yakimwondoa kwenye
uhalisia wa jina la Ninja yako ambayo yatabaki kufanya jina liwe lake hasa
akiwa uwanjani. Baada ya Bocco kupishana na 'Standing ovation'
pale chamazi lakini naiona kesho ya Himid itakayopambwa na mabango ya kumwagia
sifa kemkem. Kesho ya kila mmoja huandaliwa leo japo maandiko yanasema
"iache kesho itajihangaikia yenyewe".
Yako mengi ambayo Himid anayahitaji akiwa
Azam,moja na kuu ni kunyanyua kwapa kama ilivyofanyika kwa mtangulizi wake
Bocco. Baada ya mchezo dhidi ya Simba nilimwambia kuna kitu nakiona rohoni
mwako.Ilikuwa morali inayoonyeshwa na Azam inaanzia
kwake kama kiongozi. Nasubiri siku kuona kwapa akizinyanyua na ule wimbo mtamu
ambao wachezaji wa Azam hupenda kuimba niusikie, “popote tunakanyanga”. Tusubiri kuiona Azam ya Ninja anayecheza soka
akiwa na usinga badala ya filamu na akawa na jambia.
+255628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako