UN-High Level Advisory Board on Mediation ni nini?
Siku ya tarehe 13/09/2017 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ndugu Antonio Guterrez alitangaza kuanzisha bodi mpya ambayo inaitwa Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Upatanishi ya Umoja wa Mataifa-UN.
BODI HII NI NINI HASA?
High Level Advisory Board on Mediation ni bodi iliyoanzishwa kwa lengo la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya juhudi za upatanishi sambamba na kumpa mrejesho juu ya upatanishi duniani.
Bodi hii inaundwa na wajumbe 18 wakiwemo viongozi wa sasa na wastaafu, maafisa wa ngazi za juu na wataalamu mbalimbali kwa lengo la kuunganisha uzoefu, mbinu, maarifa na mawasiliano.
Wajumbe wake ni hawa wafuatao;
(1) Rais Michelle Bachelet wa Chile.
(2) Radhika Coomaraswamy-Mwanasheria wa Kimataifa wa Sri Lanka.
(3) Leymah Gbowe-Mshindi wa Nobel toka Liberia
(4) Jean-Marie Guehenno-Mwanadiplomasia wa Ufaransa
(5) Tarja Halonen-Rais wa kwanza mwanamke wa Finland 2000-2012
(6) David Harland-Mkurugenzi Mtendaji Centre for Humanitarian Dialogue.
(7) Noeleen Heyzer-Mjumbe Bodi ya wadhamini Chuo Kikuu cha Singapore 2013-to date.
(8) Nasser Judeh-Seneta Bunge la Jordan.
(9) Ramtane Lamamra-Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria 2013-2017.
(10) Graça Machel-Mpigania Uhuru wa Msumbiji...
(11) Asha-Rose Migiro-Balozi wa Tanzania UK
(12) Roden Muhammad Marty Muliana Natalalegawa-Indonesia
(13) Olusegun Obasanjo-Rais Nigeria 1999-2007.
(14) Roza Otunbayeva-Rais Mstaafu Kyrgyzstan.
(15) Michel Pierre-Louis- Haiti
(16) Jose Manuel Ramos-Horta- Timor ya Mashariki
(17) Gert Rosenthal-Ujerumani
(18) Justin Welby-UK
Ni imani yetu kuwa migogoro mingi itapata upatanishi wa haraka na wa kudumu.
©Uwanja wa Diplomasia.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako