NA SAMWEL CHITANYA
MOJA kati ya nchi za Afrika
ambazo raia wake wanapenda sana mchezo wa kandanda duniani ni Tanzania. Watanzania wanaupenda
sana mchezo Wa kabumbu. Ni mchezo unaopendwa na watu wengi duniani kote.
Unaongoza kwa kupendwa.
Bahati mbaya sana pamoja na
Watanzania kuupenda mchezo huu bado hawana mipango madhubuti ya kuufanya mchezo
huu uwe wenye tija kwao. Mipango yao mingi ni yakucheza mpila na Siyo Mpira
kama wenzetu wanavyo Fanya.
Timu yetu ya taifa huwa
inashiriki katika kupigania nafasi ya kushiriki mashindano mbalimbali kama vile
Kombe la dunia, kombe la mataifa Afrika na kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji Wa ligi za ndani.
Timu yetu hushiriki kikamilifu
katika kuwania nafasi zote hizo. Tunajiamini kuwa Tuna timu bora ambayo inaweza
kufanikiwa kufuzu mashindano yote hayo. Kujiamini siyo jambo baya lakini
jitazame na uwezo wako kwanza.
Mara ya mwisho Tanzania kushiriki
fainali za kombe la mataifa ya Afrika ilikuwa mwaka 1980. Miaka thelathini na
saba(37) sasa imepita tangu tushiriki mashindano makubwa zaidi ya soka katika
bara letu.
Tangu wakati huo hadi Leo hii
tumebaki kuwa wasindikizaji tu ambao tunakamilisha ratiba tu. Hatujiulizi
kwanini tunashindwa kufuzu tena kucheza fainali hizo. Kupanga ni kuchagua tusidharau
maneno ya wahenga. Walio fanikiwa wote walipanga na baadae wakachagua kufanya
moja ya Yale waliyoyapanga kwa utaratibu na hatimaye kufikia lengo. Ndio maana
wahenga walisema kupanga ni kuchagua.
TFF wanaweza kupanga sasa na
kuamua wapi tuelekeze nguvu zetu katika mashindano haya matatu, Kombe la dunia,
Kombe la mataifa Afrika(AFCON) na Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji Wa
ndani(CHAN). Tupange na kuamua Mashindano gani
tunayahitaji kwa sasa na siyo kupambana kupata nafasi katika mashindano yote,
hatutaweza fanikiwa kamwe. Na lazima tuanze na mashindano ya ndani ya bara letu
kwanza yaani AFCON na CHAN.
Mashindano yetu makubwa kushiriki
kwa mara ya mwisho yalikuwa ni CHAN mnamo mwaka 2008 pale Côte D'ivoire.
Mashindano Yale yalikuwa yanafanyika kwa mara ya kwanza yakishirikisha timu
nane tu kutoka kanda mbalimbali za kisoka. Congo DR ikawa timu ya kwanza
kuchukua ubingwa Wa CHAN baada ya kuwafunga Ghana katika fainali. Kipindi hicho
kocha Wa Timu ya Taifa alikuwa Marcio Maximo.
Nawashauri TFF tuanze na
mashindano ya kombe la Mataifa Afrika kwanza(AFCON). Sisemi kama CHAN haina
umuhimu la hasha!! CHAN angalau tumeshiriki miaka tisa iliyopita kwa mara ya
mwisho. Tunatakiwa kuwa na mipando madhubuti na AFCON ndio iwe shabaha yetu
kubwa.
Tunaweza andaa timu kwa ajili ya
kupambana kufuzu kucheza AFCON kwa miaka mitatu au minne ijayo. Timu yetu
inashiriki mashindano ya COSAFA kama waalikwa na CEFAFA pia (ingawa mashindano
yenyewe hayana ratiba maalumu). Tunaweza itumia michuano hiyo kuwa sehemu ya
kuandaa timu imara yenye uwezo Wa kupambana na kupata nafasi ya kucheza AFCON
baada ya kipindi kirefu kupita.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga
Wakati huo tukiwa tayari
tumeshapeleka barua Kule CAF kujitoa kuwania nafasi za kufuzu mashindano yote
makubwa barani Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu au minne.Kwa kufanya hivyi naamini
tunaweza kupata nafasi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika baada
ya muda tutakao jiwekea. Njia mbili zilimshinda fisi, tukubali kuelekeza nguvu
zetu zote katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika.
Timu itakayo andaliwa tuhakikishe
inapata mechi nyingi za kujipima uwezo ndani na nje ya nchi. Tuombe kukutana na
timu za mataifa makubwa kisoka hapa Afrika siyo kila siku iwe Uganda, Kenya,
Malawi, Zambia, Msumbuji, Rwanda au Burundi hapana.
Kipindi cha Maximo timu ilikuwa
inasafiru nje ya nchi na kuomba kucheza mechi za kirafiki pia kipindi hicho
timu yetu ilikuwa inacheza mechi za kirafiki na timu za mataifa makubwa kisoka
hapa Afrika tunaweza tumia mfumo huo ili kujenga timu yetu. Tuhakikishe mechi za
kalenda ya FIFA tunazifuatana vilivyo na ziwe mechi zenye tija ili kujenga timu
yetu.
Tunaweza tukadhani uchache Wa
wachezaji Wa kitanzania wanao cheza soka nje ya nchi ndiyo sababu la hasha!!
Tatizo letu hatuna michuano maalumu ambayo tunaihitaji.
Botswana, Venezuela ni funzo
tosha kabisa. Venezuela wamefanikiwa kufika fainali za kombe la dunia kwa
vijana chini ya umri Wa miaka 20 mwaka huu 2017 na kupoteza kwa goli 1-0 dhidi
ya England. Kabla ya kufika hapo waliandaa
timu yao ya vijana kwa muda mrefu na ilipata mechi za kujipima uweo zaidi ya
arobaini. Hatimaye wakafanikiwa kutinga fainali.
Kwa Taifa changa kisoka kama letu
hatuna budi kuelekeza nguvu katika shindano moja.
Tukiamua tunaweza, kuongeza timu
za ligi kuu kwa madai wachezaji wetu wapate mechi nyingi ilikuwa na timu ya
Taifa imara hiyo peke yake haitoshi. Tuamue sasa mashindano gani tunayahitaji
na tuanze kujindaa nayo mapema na kuelekeza nguvu zetu zote huko.Bila kufanya
hivyo tutaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu siku zote. Wahenga walisema Ukiona vya Elea
ujue vimeundwa.
0674721910.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako