1.Hifadhi ya Taifa Kitulo ndiyo
eneo pekee Tanzania lenye ndege aina ya tandawala machaka (Denhams Bustard)
wenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine.
2.Hifadhi hiyo inayopita katika
mikoa ya Mbeya na Njombe ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 2005
ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, msitu wa Livingstone na bonde
la Numbi.
3.Kitulo ina ukubwa wa kilometa
za mraba 442. Awali ilijulikana kama Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredirick
Elton kupita eneo hilo mwaka 1870. Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo
(FAO) lilichukua eneo hilo kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.
4. Ndege aina ya tandawili
machaka hawapatikani sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania zaidi ya Kitulo.
5.hifadhi hiyo ndiyo eneo pekee
ambalo ndege hao hutaga mayai na kuzaliana kwa wingi kabla ya kusafiri kwenda
mabara mengine.
6.Utafiti unaonyesha kuna ndege
aina ya tandawili machaka ambao waliwekwa alama walipokuwa katika Hifadhi ya
Taifa ya Kitulo na baadaye kuonekana wakiwa na alama zao katika hifadhi moja
Australia.
7. Ndege hao wamekuwa na tabia
katika msimu fulani kuruka na kufika katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo kwa
ajili ya kutaga mayai na kuangua vifaranga kutokana na mazingira ya hifadhi
hiyo kuonekana kuwa ni mahali pekee duniani penye hali ya hewa rafiki kwa ndege
hao kuzaliana. Hivyo baada ya kutaga mayai, kuangua vifaranga na ndege kukua,
huruka na kwenda mabara mengine duniani.
8.Utafiti umebaini kuwa katika
Hifadhi ya Kitulo ndege aina ya abdims stock, denhams (tandawili machaka) na
blue swallow ambao wametoka Afrika Kaskazini, Afrika Kusini, Australia na Ulaya
wanaitumia Hifadhi ya Kitulo kama makazi yao katika misimu tofauti.
9.Hifadhi ya Kitulo pia
inasifika kwa kuwa na zaidi ya aina 40 za maua mbalimbali ambayo hayapatikani
sehemu nyingine duniani.
10. Ndani ya msitu kuna miti ya
aina ya cidar yenye urefu wa zaidi ya mita 50 na inakadiriwa kuwa ndiyo miti
mirefu kuliko yote duniani.
©HOOPS KAMANGA
No comments:
Post a Comment
Maoni yako